kujiandaa kuwa mjamzito nini kinahitajika

Smile

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
15,347
11,610
ni nini kinatakiwa kiafya kwa mwanamke anayejiandaa kubeba ujauzito ili kuepuka matatizo kipindi cha ujauzito?
 
Inategemea Bebii, ila cha msingi inabidi akubali kuwa sasa anabeba mimba na hormones zake zitabadilika kiasi na apokee mabadiliko yatakayofuatia. Mimba huwa zinatofautiana kati ya mama na mama, kwaahiyo baadhi ya dalili ni unique haiwezekani kudesa kwa mwingine. Atulize akili, ahakikishe kakiasi ka kumsukuma kipindi hicho chote kinapatikana maana huwa wanapenda kubadili ladha ya chakula mara kwa mara na mazoezi ya hapa na pale, otherwise kama inawezekana ahakikishe upendo wa baba unazidi.............
 
ni nini kinatakiwa kiafya kwa mwanamke anayejiandaa kubeba ujauzito ili kuepuka matatizo kipindi cha ujauzito?

Kijuujuu....Ujauzito ni kipindi ambacho mwili wa mwanamke unakuwa challenged to the fullest, hivyo ni kipindi kinachohitaji maandalizi. Unahitaji maandali yafuatayo (wengine wataongezea kwenye hiyo list):
- Utayari wa kisaikolojia wa kubeba ujauzito, kuzaa na kuwa mama
- Utayari wa kimwili (kuna uzito ambao unashauriwa kuongezeka na kwa kasi gani)
- Utayari wa kilishe (kuna vyakula ambavyo unashauriwa kula)
- Utayari wa kifedha (oooh yeah unahitaji pesa ya kutosha)
- .......
 
Miezi mitatu ya Mwanzo, kutapika ni suala la kawaida ingawa linakera kwa Wajawazito wengi.
Kuna vyakula ambavyo mwanamke mjamzito hataki hata kuviona au kusikia harufu yake.
 
Kijuujuu....Ujauzito ni kipindi ambacho mwili wa mwanamke unakuwa challenged to the fullest, hivyo ni kipindi kinachohitaji maandalizi. Unahitaji maandali yafuatayo (wengine wataongezea kwenye hiyo list):
- Utayari wa kisaikolojia wa kubeba ujauzito, kuzaa na kuwa mama
- Utayari wa kimwili (kuna uzito ambao unashauriwa kuongezeka na kwa kasi gani)
- Utayari wa kilishe (kuna vyakula ambavyo unashauriwa kula)
- Utayari wa kifedha (oooh yeah unahitaji pesa ya kutosha)
- .......
Mimi ningeshauri kwanza utayari wa wote wawili as it takes two to tango hasa kisaikolojia maana yaliyosemwa na wote ukiwa na mwenza maisha yanakuwa mswano.
kwenda kliniki ya mama na mzazi mapema iwezekanavyo itasaidia sana kuona viashiria vya hatari mapema zaidi na kupata ushauri ya jinsi mimba inavyoendelea kiutaalam zaidi.
Haya wengine endeleeni...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom