Kujamba (kutoa ushuzi) kuna faida kiafya?

Japo imekaa kiutani, lkn kuna kitu muhimu sana hapa.

Nishawahi kula mkong'oto (kipindi nikiwa dogo) kwenye sahani kisa nilijamba.

Lakini nilimuuliza mama yangu, kwanini kanipiga.

Japo nilikua mdogo kipindi hiko lkn niliamini nimeonewa sababu nilijua kujamba sio kosa.

Na mpaka leo nimeendelea kuamini hivyo japo watu wengi (hasa wazee) watakuona ni mtovu wa nidham.
 
Jamba Wewe ila asijambe mwingine kinanuka vibaya aisee hasa ukute uko na mamaa alafu ajambe wanaume huwa hatuvumilii aisee.
 
I like this ! Nimecheka sana leo kwani umenikumbushia consultant mmoja wa kizungu alikuja kutufanyia kazi ofisini kwetu, sasa sisi huwa tukijisikia ku-pumua tunaenda mbali na upeo wa masikio na pua za wenzetu (sometimes washroom), ila yeye alikuwa anaviachia tu tena kwa sauti kuuuuuubwa du!

Hivi na mimi niulize, kujamba kunaitwaje kwa kiingereza vile?

Kujamba = Fart
 
Kujamba raha dogo,haswaaaa tena namshauri bosi wako ale mayai mawili ya kuchemsha,maharage bakuli 1,maziwa mgando na pepsi
 
Jamii nyingine ukijamba unapongezwa hasa wakati wa kula...
Ukicheuwa hata chakula wenzio hawali tena!!
 
- Tushirikishane huu ujumbe -

Kwanini tunajamba? kwanini "ushuzi" unanuka? Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi wetu, lakini inaweza kukufanya ujisikie vizuri kujua kwamba ni tendo la kawaida sana kwa mwili wa binadamu kutenda.

1.Kujamba ni nini hasa?
Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa, ambayo inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi. Baadhi ni hewa tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa. Hewa ingine husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu kutoka kwenye damu, na baadhi ya gesi huzalishwa na kemikali katika utumbo au bakteria. Kwa kawaida "ushuzi" unakua na asilimia 59 ya gesi ya nitrogen, asilimia 21 ni hydrogen,asilimia 9 ni carbon dioxide, asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen.

Asilimia moja tu ya "ushuzi" inaweza kuwa hydrogen sulfide na mercaptans, ambayo ndio ina sulfur ndani yake,sulfur ndo hufanya "ushuzi" utoe harufu mbaya. Kujamba huambatana na sauti, hii ni kutokana na "vibration" katika njia ya haja kubwa. Ukubwa wa mlio wa kujamba hutegemea "presha" inayosukuma gesi itoke nje na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.

2. Kwa nini Ushuzi hutoa Harufu mbaya?
Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa mtu, vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio usababisha hili. Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama soda, maharage, kabichi na mayai.

3.Watu hujamba hadi mara 14 kwa siku
Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa siku. Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi cha miaka 6, anaweza kuzalisha nishati ya kutosha kutengeneza bomu la atomiki.

4. Ushuzi husafiri kwa mwendo wa futi 10 kwa sekunde.
Harufu ya ushuzi huanza kusikika sekunde 10-15 baada ya mtu kujamba, hiyo ni kwa sababu inachukua muda mrefu kwa harufu kufikia pua.

5.Kujizuia Kujamba Inaweza Kuhatarisha Afya Yako.
Madaktari hawajakubaliana moja kwa moja kama kujizuia kujamba ni hatari kiafya. Baadhi ya wataalam wanafikiri kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, hivyo kujizuia kujamba haitakuletea madhara. Wengine wanadhani kwamba kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa gesi, na pia inaweza sababisha bawasili (hemorrhoids).

6.Kwa Baadhi ya Tamaduni, Kujamba Sio Ishu
Wakati tamaduni nyingi zikichukulia tendo la kujamba lifanywe kistaarabu, kuna baadhi ya tamaduni hawaoni haya kujamba hadharani, na pia hufurahia tendo hilo. Mfano kabila la Yanomami huko America ya Kusini kwao husalimiana kwa kujamba na China unaweza kupata kazi ya kunusa ushuzi! Katika Roma ya zamani Mfalme Claudius akihofia kwamba kujizuia kujamba inaweza kuwa hatari kiafya, alipitisha sheria kwamba ni ruhusa kujamba kwenye "banquets".

7. Ushuzi Unawasha Moto
Kama ilivyoandikwa hapo juu. Methane na hydrogen inayozalishwa na ushuzi inaweza sababisha moto.

8. Mchwa Hujamba Kuliko Wanyama Aina Zote
Ni ngumu kuamini kuwa mchwa ndo anawajibika na matatizo yetu ya "Global Warming". Mchwa huongoza kwa kujamba kwa wanyama na hiyo huzalisha gesi ya methane.

9.Ukiubana Ushuzi, Utakutoka Usingizini
Hata ujitahidi kuubana vipi, ushuzi utatoka mara utapokua umepumzika, hasa ukiwa umelala.

10. Watu Hujamba Hata Baada ya Mauti Kuwafika
Maiti huendelea kutoa gesi hadi masaa matatu baada ya mtu kufariki dunia, hii huambatana na milio ya kujamba. Hali hii husababishwa na misuli kusinyaa.

UKIPATA MUDA JAMBA

REFFERENCES
www.health.co.uk
 
Ha ha haaa...weee jamaa wewe sorry em niulize hivi Nitrogen ina matumizi gani duniani ili tuivune kwa wingi maana inaonekana composition yake ni kubwa kulinganisha na nyingine kwenye ushuzi!
 
- Tushirikishane huu ujumbe -

Kwanini tunajamba? kwanini "ushuzi" unanuka? Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi wetu, lakini inaweza kukufanya ujisikie vizuri kujua kwamba ni tendo la kawaida sana kwa mwili wa binadamu kutenda.

1.Kujamba ni nini hasa?

Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa, ambayo inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi. Baadhi ni hewa tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa. Hewa ingine husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu kutoka kwenye damu, na baadhi ya gesi huzalishwa na kemikali katika utumbo au bakteria. Kwa kawaida "ushuzi" unakua na asilimia 59 ya gesi ya nitrogen, asilimia 21 ni hydrogen,asilimia 9 ni carbon dioxide, asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen.

Asilimia moja tu ya "ushuzi" inaweza kuwa hydrogen sulfide na mercaptans, ambayo ndio ina sulfur ndani yake,sulfur ndo hufanya "ushuzi" utoe harufu mbaya. Kujamba huambatana na sauti, hii ni kutokana na "vibration" katika njia ya haja kubwa. Ukubwa wa mlio wa kujamba hutegemea "presha" inayosukuma gesi itoke nje na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.

2. Kwa nini Ushuzi hutoa Harufu mbaya?

Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa mtu, vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio usababisha hili. Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama soda, maharage, kabichi na mayai.

3.Watu hujamba hadi mara 14 kwa siku

Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa siku. Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi cha miaka 6, anaweza kuzalisha nishati ya kutosha kutengeneza bomu la atomiki.

4. Ushuzi husafiri kwa mwendo wa futi 10 kwa sekunde. Harufu ya ushuzi huanza kusikika sekunde 10-15 baada ya mtu kujamba, hiyo ni kwa sababu inachukua muda mrefu kwa harufu kufikia pua.

5.Kujizuia Kujamba Inaweza Kuhatarisha Afya Yako.

Madaktari hawajakubaliana moja kwa moja kama kujizuia kujamba ni hatari kiafya. Baadhi ya wataalam wanafikiri kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, hivyo kujizuia kujamba haitakuletea madhara. Wengine wanadhani kwamba kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa gesi, na pia inaweza sababisha bawasili (hemorrhoids).

6.Kwa Baadhi ya Tamaduni, Kujamba Sio Ishu

Wakati tamaduni nyingi zikichukulia tendo la kujamba lifanywe kistaarabu, kuna baadhi ya tamaduni hawaoni haya kujamba hadharani, na pia hufurahia tendo hilo. Mfano kabila la Yanomami huko America ya Kusini kwao husalimiana kwa kujamba na China unaweza kupata kazi ya kunusa ushuzi! Katika Roma ya zamani Mfalme Claudius akihofia kwamba kujizuia kujamba inaweza kuwa hatari kiafya, alipitisha sheria kwamba ni ruhusa kujamba kwenye "banquets".

7. Ushuzi Unawasha Moto
Kama ilivyoandikwa hapo juu. Methane na hydrogen inayozalishwa na ushuzi inaweza sababisha moto.

8. Mchwa Hujamba Kuliko Wanyama Aina Zote

Ni ngumu kuamini kuwa mchwa ndo anawajibika na matatizo yetu ya "Global Warming". Mchwa huongoza kwa kujamba kwa wanyama na hiyo huzalisha gesi ya methane.

9.Ukiubana Ushuzi, Utakutoka Usingizini

Hata ujitahidi kuubana vipi, ushuzi utatoka mara utapokua umepumzika, hasa ukiwa umelala.

10. Watu Hujamba Hata Baada ya Mauti Kuwafika

Maiti huendelea kutoa gesi hadi masaa matatu baada ya mtu kufariki dunia, hii huambatana na milio ya kujamba. Hali hii husababishwa na misuli kusinyaa.

UKIPATA MUDA JAMBA

REFFERENCES
www.health.co.uk
Mada hii ni nzuri sana
 
Natumaini mnaendelea vyema
Jamani msaada tafadhali mdogo wangu tumbo linamuuma sana na vichomi kwa ndani halafu anajamba sana utadhani tumbo limeoza akipumua (kujamba) inakua ni harufu kali kama kitu Kilichooza jee ana tatizo gani?
Hadi anaogopa kukaa na mtu karibu yake
 
Mwamlisha nini kwani huyo kijana toba ya rabi visivyosagika vikatokaaa aaaah?!!!

Hebu mpe simu niongee nae.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom