Kujadili Muungano si chokochoko!

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Kuna baadhi ya wananchi wanahoji baadhi ya masuala ya muungano na wanaomba ujadiliwe katika pande zote mbili za muungano. Hilo likijitokeza wanaambiwa wanaleta chokochoko. Binafsi naamini kwamba kufanya hivyo ni haki yao ya msingi ya kujadili masuala yanayohusu maisha yao.
 
Ni haki ya msingi sana kuujadili huo Muungano kwani ndio unaoleta malalamiko makubwa bana ya watu wa pande zote.
 
To be more specific ni kuwa Muungano haujadiliki ila kero na misingi ya muungano should be discussed ili udumu na uwe na manufaa kwa pande zote
 
To be more specific ni kuwa Muungano haujadiliki ila kero na misingi ya muungano should be discussed ili udumu na uwe na manufaa kwa pande zote

Kweli haujadiliki lakini si kwa sababu ulizozitoa Mkuu.

Muungano huu ndio kero, uvunjike tu, hauna manufaa.

Ikiwa kwa miaka 47, kero hazikutatuka, ije iwe sasa?
 
ukiwa unajadili mustakabali wa nchi iitwayo Tanzania, lazima muungano uujadili kwa sababu vinginevyo hujaigusa hiyo jamhuri. na kwa vile kwa sasa tuna jadili katiba, ambayo ni ya hiyo jamhuri, lazima muugnano ujadilike, upende usipende
 
Kweli haujadiliki lakini si kwa sababu ulizozitoa Mkuu.

Muungano huu ndio kero, uvunjike tu, hauna manufaa.

Ikiwa kwa miaka 47, kero hazikutatuka, ije iwe sasa?
Nakubaliana.

Tutengane.

Zanzibar wanaona wanamezwa.

Tanganyika wanaona wanatwishwa mzigo.

Muungano na uvunjwe!


 
Muungano ni lazima ujadiliwe tena kwa undani, siyo juu. Hautaki kupigwa brush huo. Nahisi Wananchi wengi wa Tanganyika hawajuwi hasa huu Muungano una lengo gani. Wanabebeshwa mzigo wasioujuwa.Ni tofauti sana na wananchi wengi wa Zanzibar. Wao wanaelewa Muungano una malengo gani.

Wasiotaka kujadili Muungano, ama wana maslahi binafsi au ni wale waliondamwa na mizimu ya Butiama. Kwao wao Nyerere ni mtume kwa hivyo hana makosa.

Kwetu sisi wengine, Nyerere ni binadamu kama binadamu wengine, amejaa makosa. Kwa hivyo kuyarejea makosa ya Nyerere itakuwa ni ujinga, uzembe na kuongozwa na mawazo mgando.
 
Back
Top Bottom