Kuishi na mke wa aina hii, uwe na moyo kama mwendawazimu!

Tatizo sisi binadamu hasa kizazi hiki tunachanganya ndoa na mambo mengine!
Kwa ufahamu wangu Ndoa sio suala la kutumia akili zetu,bali ni kumhusisha Mungu kwa asilimia zote..Huwezi kuchukua container ukabebesha kwenye tax au tyre la fuso ukafunga kwenye suzuki ukitegemea litafanya kazi .....Namaanisha si kila umwonaye kwa macho yako anaweza kuwa mke/mme wako.

Kabla hata hujawaza Ndoa yakupasa kumwomba Mungu ,Naye atakupa kile uombacho, kwani kile upandacho ndicho utakachovuna.Ukikosea ktk uchumba utaharibu maisha yako yote, Na wengi wetu tunagharamia kutafuta warefu, wafupi, weupe, wenye mali, wasomi,wafanyabiashara na vigezo vingi vya kidunia BADALA ya kugharimia kumwomba Mungu ili atupe msaidizi wa kufanana na sisi ambaye kwayo atakuwa na upenda usio na masharti (yaani mtapendana bila sbb yeyote/unreasonably) sio hadi wageni wawatembelee...

Msaidizi wa kufanana nawe ni yule ambaye anakamilisha mapungufu yako , rejea mfano wangu hapo juu,sasa badala ya kukamilisha mapungufu uliyonayo ndiyo kwanza ataongeza matatizo (kama hayo ya unyonyaji uliyoyasema) kama tunaangalia mambo ya nje!

Na wewe mwenye aina hii ya Ndoa hebu jitathmini kwanza kabla ya kulalamika, maana kwa uzoefu wangu wanaokimbilia kulalamika ndio wanakuwa na mapungufu makubwa na tabia mbaya kuliko wenzao. Kumbuka utapewa mke/mme kulingana na jinsi ulivyo na si vinginevyo!! kuweni makini jamani Msiingie ktk NDOA KUFUATA MKUMBO, pia wengine kabla hata ya ndoa anawaza kuja kuwa na kidumu au nyumba ndogo,sasa kwa hali hii unategemea kutakuja kuwa na ndoa hapo,. Ndio hayo mnabaki ndoa za siku hizi hazidumu.....badala ya kuwa wa kwanza kuzidumisha.

Siku hizi nyingi si ndoa ni sanamu za ndoa.....hakuna kitu!
 
upendo kama ukiwepo kwa mwanamke atafanya yaliyomema lakini kama laana imo ndni ya moyo wake basi hana jipya ni ujinga kwenda mbele wanawake badilikieni ndio maana ndoa nyingi hazidumu siku hizi
 
Nasikiaga eti small houses ndo wataalam wa kufanya hayo mambo kuliko mawife wenyewe sasa sijui ka ni kweli!! Lol!
kama ni kweli walinde ndoa zao,mbona wengi wao ni ambao wameachika
 
Halafu munasema eti wenye watumwa ni waarabu tu kumbe hata nyinyi wabantu mukipata nafasi ya kuwa na watumwa munaitumia vizuri?
dah..........Masikini! Hivi kumvua mpenzio viatu na soksi once in a while ni utumwa!?! Mbona hamshangai kucheza kidali poh, kupigana na mito na ujinga mwingine mwingi ufanywao na wapendanao kama nao ni utoto,utumwa na ukoloni?! Mwe I think bado naelea kwenye ulimwengu wa kufikirika pengine!!!
 
Ndefu hivyo halafu itaendelea!!
Hapo kujifanya mnyekevu pindi anapohitaji kitu ni tabia ya watu wengi. Hata makazini watu wakitaka wapate kitrip lazima utakuta wanajifanya wanyenyekevu kwa wahusika.
 
Hahahahhaha mtambuzi si unyenyekevu tu bana sometimes unajisikia tu umvue mwenzio kwa upendo. Tena kuvua kwenyewe si kwa kuinama bali mke anakaa chini kabisa ananyoosha miguu yake na miguu ya Mr anaiweka kwenye mapaja anavua soksi akimasaji taratibu huku akipiga 'umbeya' na mumewe kumjulia hali, siku yake imekwendaje na kumweleza lililojiri nyumbani mwake na hata jinsi gani alivyommiss au alivyojisikia vizuri alivyopokea simu yake mchana ule..................... hahahahahahah mi ctaki kwa nini lakini mnatukumbushia machungu enyi waja??
Arooooo wee mdada umenikunaaaaa. Lakini kwangu mimi hiyo ni hatari naweza kujishitukia nimeshahonga nyumba ya urithi hivihivi.
 
Ndefu hivyo halafu itaendelea!!
Hapo kujifanya mnyekevu pindi anapohitaji kitu ni tabia ya watu wengi. Hata makazini watu wakitaka wapate kitrip lazima utakuta wanajifanya wanyenyekevu kwa wahusika.

Saasa huo si unafiki?
 
Kwa kuongezea hapo kwenye bold; Watu wanaoa wakiwa na vidumu na vimada tayari; yaani unakuta mtu ameamua kuhalalisha mmoja kati ya wengi na wengine anaendelea nao kama mpango wa kando. Unakuta mtu ametembea na mwanamke/mwanamme mwingine a day before marriage what do you expect???

Tatizo sisi binadamu hasa kizazi hiki tunachanganya ndoa na mambo mengine!
Kwa ufahamu wangu Ndoa sio suala la kutumia akili zetu,bali ni kumhusisha Mungu kwa asilimia zote..Huwezi kuchukua container ukabebesha kwenye tax au tyre la fuso ukafunga kwenye suzuki ukitegemea litafanya kazi .....Namaanisha si kila umwonaye kwa macho yako anaweza kuwa mke/mme wako.

Kabla hata hujawaza Ndoa yakupasa kumwomba Mungu ,Naye atakupa kile uombacho, kwani kile upandacho ndicho utakachovuna.Ukikosea ktk uchumba utaharibu maisha yako yote, Na wengi wetu tunagharamia kutafuta warefu, wafupi, weupe, wenye mali, wasomi,wafanyabiashara na vigezo vingi vya kidunia BADALA ya kugharimia kumwomba Mungu ili atupe msaidizi wa kufanana na sisi ambaye kwayo atakuwa na upenda usio na masharti (yaani mtapendana bila sbb yeyote/unreasonably) sio hadi wageni wawatembelee...

Msaidizi wa kufanana nawe ni yule ambaye anakamilisha mapungufu yako , rejea mfano wangu hapo juu,sasa badala ya kukamilisha mapungufu uliyonayo ndiyo kwanza ataongeza matatizo (kama hayo ya unyonyaji uliyoyasema) kama tunaangalia mambo ya nje!

Na wewe mwenye aina hii ya Ndoa hebu jitathmini kwanza kabla ya kulalamika, maana kwa uzoefu wangu wanaokimbilia kulalamika ndio wanakuwa na mapungufu makubwa na tabia mbaya kuliko wenzao. Kumbuka utapewa mke/mme kulingana na jinsi ulivyo na si vinginevyo!! kuweni makini jamani Msiingie ktk NDOA KUFUATA MKUMBO, pia wengine kabla hata ya ndoa anawaza kuja kuwa na kidumu au nyumba ndogo,sasa kwa hali hii unategemea kutakuja kuwa na ndoa hapo,. Ndio hayo mnabaki ndoa za siku hizi hazidumu.....badala ya kuwa wa kwanza kuzidumisha.

Siku hizi nyingi si ndoa ni sanamu za ndoa.....hakuna kitu!
 
Kuna wanawake ambao wanaitwa wana kisirani na wanyonyaji. Wanawake wa aina hii ndani ya ndoa zao ni vituko vitupu, na mara nyingi kama wameolewa na wanaume waliojitambua ndoa zao huwa hazidumu.

Mara zote mke wa aina anataka kuona mumewe akimhangaikia kupita kiasi na bado asiridhike. Ni vigumu kutabiri mienendo ya tabia zao. Kama anahitaji kufanyiwa jambo na mumewe na anahisi mumewe haweze kumtimizia, anaweza kuamka akiwa na furaha tele, lakini ikifika jioni utamkuta amenuna tu. Na mumewe atakapomuuliza sababu ya kununa, anaweza mkujibu “hamna kitu” , anachotafuta hapo ni kubembelezwa ili apate mahali pa kunzia.
Kwa kuwa anajua kuwa mumewe anamjali, atasema shida yake. “ Yaani hela unayoniachia ya matumizi hapa nyumbani haitoshi kabisa na ninapata tabu sana kupanga bajeti”. Tayari ujumbe umefika, lakini kwa namna ambayo itamfanya mume dhamira zimshitaki. Mume kwa kushtakiwa na dhamira ataongeza fedha. Kama ni mke aliyejiajiri au kuajiriwa anaweza kusingizia kuwa siku hizi biashara hakuna kabisa na hapati mapato ya kutosha au mshahara anaolipwa hautoshi na anafanya kazi, ile basi tu.

Na kauli kama hizi ni za kutarajiwa sana, “Waume wengine wanawasaidia wake zao kama mshahara au mapato hayatoshi, mimi ndivyo ninavyojua”.
Anachotaka ni kumfanya mumewe ahisi kwamba, yeye kama mume ameshindwa wajibu wake na kwamba, kuna wanaume bora zaidi huko nje ambao wanaweza kuwasaidia wake zao pale wanapokuwa na mshahara mdogo au mapato madogo katika biashara zao.
Wanawake wa aina hii huwa hawajiamini kabisa, na hutaka kuonekana ni wa maana, wana uwezo, wanajua na wanatambuliwa. Wanaweza kuwa na kisirani cha hasira za ziada, wambea sana, na wakati mwingine hupenda kujilinganisha sana.
Hawana subira kabisa, wakitaka jambo lao wanataka litimizwe wakati huo huo, ni wasingiziaji wazuri, wakanushaji wa waziwazi wa mambo waliyofanya au kusema.

Ni watu wenye kero mwanzo mwisho.
Pia wanakuwa na upendo wa bandia, pale wanapohitaji kitu kutoka kwa waume zao, watatenda yale ambayo hawayatendi. Atajifanya kumpokea mumewe akitoka kazini, kumuuliza angependa kula kitu gani, kumpangia au kumtafutia nguo za kuvaa asubuhi.
Siku zote hafanyi hivyo, bali hufanya yote hayo pale anapohitaji kitu kutoka kwa mumewe. Utakuta ni mtu wa mbinu na ujanjaujanja tu. Hasa kukiwa na wageni ndio ataonesha anampenda sana mumewe. Hata kama alikuwa hamvui soksi akitoka kazini , kukiwa na wageni atafanya hivyo. Ni wanafiki wa upendo kupindukia.

Itaendelea......................

mpwa niimecheka mpka naamini sasa dhambi zangu za wiki hii zimesamehewa mmhhh kwa ushauri wa aina hiyo kula kona mapema funga macho
ukiona wako hivi ama wanafanya hivi wengi wao wameona kitu ama mmechuma pamoja..ninao kamfano kadogo wakati na google nikawa na kabinti kamoja pale kijitonyama kakaahamia kakihisi kamefika kwa kweli najua nilitenda dhambi nikartubu kalianza kunipelekesha lakini kabla ya hapo kakaanza hny nimepata hii tuchange tununue kaabati kubwa...mara kitanda ..mmh machale yakanicheza mbona speed kubwa nikiwa naendelea nikaanza kununua vyangu na kuweka home kweli bana baada ya miezi sita mwanamke ananza kutaka ndoa kama sitaki achukue vyake aondoke ..aliponikosa alipata scholarship yakwenda finland mshenzi yule akaniambia nimetuma na wewe cert zako kweli jamaa wakaktutumia full mkoba akadai niache kazi nikamwambia aku we kasome ukirudi na mimi niende nakwambia akwenda popote....akanimwagia maji yamoto tena chai nikiwa nimetoka job frm no whr nikamwomba housegirl naomba chakula nikasikia kifuani pwaaaaaaaa kuhamaki kifua kinatetemeka kama naondoka kesho mpwa mbaya akakimbia na gari akihisi sijui nimekufa...nikaenda hosp wakapima wakasema uko feet kabisa nikarudi na canter usiku wa saa nane nikachukua changu nikamwandikia barua ahsante sijafa mungu akusaidie nikala kona..kinachotesa wengi uamuzi wa mapema mpwa
 
Kwa hiyo unatushauri tukitaka unyumba kwa wake zetu, tuwe tunajipendekeza sana na pengine kutoa rushwa........................

unajipendekeza sana ila kwa namna ambayo unaona ni kawaida.
Mwenyewe jifikirie huwa unaanzaje anzaje.
 
Halafu munasema eti wenye watumwa ni waarabu tu kumbe hata nyinyi wabantu mukipata nafasi ya kuwa na watumwa munaitumia vizuri?

Kwa sehemu kama hii JF ni rahisi sana mtu akajieleza kinyume na maisha yake ya kawaida' kwa maelezo yako waweza kuwa mmoja wa hao watumwa'
 
kwa sehemu kama hii jf ni rahisi sana mtu akajieleza kinyume na maisha yake ya kawaida' kwa maelezo yako waweza kuwa mmoja wa hao watumwa'

nakutunukia degree ya jf ya utambuzi na mungu akuweke
wasalaam
pdidy
 
sio nyumba ndogo tu hata wake wakubwa wanafanya hivyo na sidhani kama wananyanyaswa ila wanafanya kwa mapenzi kumvua mume viatu au soksi ni hiari ya mtu
 
unajipendekeza sana ila kwa namna ambayo unaona ni kawaida.
Mwenyewe jifikirie huwa unaanzaje anzaje.

hata sikumbuki kama ninaanzaje ninapotaka jambo hilo, maana wakati mwingine hata jikoni mambo yanakuwa shwari tu, sina eneo maalum la kujidai ni popote pale ambapo tutapata faragha ndani ya nyumba yetu...............
Labda nimuulize mama Ngina wangu kuwa huwa namuanzaje nikitaka, kisha nitakujibu....................LOL
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom