'kuishi kwa dada'

kuishi kwa dada si mbaya kama unaishi pale ili ujipange kuwa na kwako.

Hasa hawa vijana walio mashuleni na vyuo au wale wanaotafuta kazi sioni ubaya kabisa kuishi hapo sababu kila mtu anahitaji msaada kutoka mahali fulani at a certain point.

Tatizo linakuja pale mtu anapoishi kwa dada, na yeye anajichulia kama mtoto wa pale aliyechekechea, hana wazo la kutafuta maisha yake, yaani yeye sahani ya chakula na kubaki home anasimamia mahausi girl wa mtaa.

Kuna mwingine anaenda mbali na kuoa akiwa anaishi kwa dada na kuzaa watoto akiwa hapo hapo. Au mwingine hata kama hajaoa lakini mwanamme above 35yrs tunategemea uwe na kwako hata kama ni chumba cha kambi ya fisi kinakupa heshima zaidi kuliko kukaa masaki kwa dada, tena ukute dada naye yuko single leo ana bakari kesho Joseph basi inakuwa tabu tupu.

Afu mwanamme akishakuwa mkubwa sana akiishi kwa dada anaanza kujiona ana haki hivi ya ku-impose rules zake, leo naye atataka aje na demu wake, kweli uje ukamulie kwa dada?? Akizuiwa inakuwa nongwa.

Kwa wakaka mnaokaa kwa dada zenu, muwe mnajiongeza kupata akili ya kujitegemea.
 
acha tu nipite.....

maana sidhani kama kuna mtu anapenda kuishi kwa dada au kaka yake au ndugu yoyote....
nadhani ni ugumu na matatizo ya dunia....
sema kwa vile mtu hatembei na bango la matatizo yake mtu huwezi kuona wala kujua zaidi ya kunyoosha vidole...

hivyo acha nisonge mbele.....

Ningekua situmii TECNO.
 
Ni kwamba hata sabuni ya kuogea mwenyewe na colgate ni vile vya watoto na hg kule bafu la common, nini kuchangia chumvi

Mmh, kweli undugu kazi. Huyu ana dalili kubwa kuwa siku asipokuta sabuni bafuni naye atatoa taarifa kuwa '''sabuni ya kuogea imekwisha'''.....
 
kuishi kwa dada si mbaya kama unaishi pale ili ujipange kuwa na kwako..Tatizo linakuja pale mtu anapoishi kwa dada, na yeye anajichulia kama mtoto wa pale aliyechekechea, hana wazo la kutafuta maisha yake, yaani yeye sahani ya chakula na kubaki home anasimamia mahausi girl wa mtaa.Kwa wakaka mnaokaa kwa dada zenu, muwe mnajiongeza kupata akili ya kujitegemea.

What if the same person stays with his brother?..would it be okay?..or?..what so special with sisy's home!
The way u put it sounds like to stay on your sisy's home is kinda of a shame act!..ryte?
 
Mimi navyoona kukaa kwa Dada au kaka sio mbaya kama walivyopita wenzangu, hapa swala ni umekaa kwa lengo gani kama ni kula lala amka kula lala iyo Noma na si kwa Dada na Kaka tu Bali hata kama ni kwa mzazi wako pia, we utakaa kwa Mdingi mpaka lini na Madingi wengine Ikifika saa 12 geti lafungwa sasa check apo imekaa vipi Dume zima unapangiwa muda wa kuludi home.All in all si mbaya kukaa kwa ndugu ila iwe kwa muda flani tu baadae unasepa.Naweza thubutu kusema kua kijana anaejitambua vzr hawezi kubali kuwa kula kulala, lazima atakua na uchungu wa kutafuta ili nae awe na kwake na si kuegesha kwa ndugu kila siku.
 
Sijui unatoka kwenye tamaduni gani
Ila nikakotoka mie mwanamme hatakiwi kumtegemea dada yake kwa aina yeyote, ni aibu kubwa sana.

Siku zote mwanamme anachukuliwa kiongozi wa familia, hata baba ataondoka anayekabidhiwa majukumu ya familia ni kijana amkubwa aliyepo wa kiume hata kama kuna dada zake wakubwa zaidi yake.

Sasa hii kimjini mjini unapoamua kumbeba kaka kwa sababu umesimama kabla yake inabidi ajue kabisa ni 'favor' na 'aibu' kiaina kukaa kwa dada bora kwa kaka ambaye ni mwanamme mwenzie.

Hujawahi sikia baadhi ya makabila dada mkubwa anampigia goti mdogo wake wa kiume sababu tu ni mwanamme kwa hiyo ni 'mkubwa' katika maamuzi ya familia???

Hivyo vitu kama goti si hivi hivi vinakuja na majukumu yake kama hayo ya kutotegemea dada zake
Kaka mkubwa hawezi mpigia goti mdogo wake wa kiume, kwa mdogo akikaa kwa kaka yake ni sawa.

What if the same person stays with his brother?..would it be okay?..or?..what so special with sisy's home!
The way u put it sounds like to stay on your sisy's home is kinda of a shame act!..ryte?
 
jamani hayo ni mambo ya kawaida ,ila kama unakaa kwa ndugu usibweteke maana kuna wengine wakaaa kupitiliza mpaka wanakuwa kerooooooooooo
 
Back
Top Bottom