BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,006
Waungwana leo nimelazimika kuwakumbusha hotuba ya Mh Dr Slaa pale Mwembeyanga siku tatu hive kabla ya uchaguzi. Alisema "kuchagua CCM ni maafa" na "CCM ni sawa na kikundi cha Taleban cha huko Afghanistan". Kauli hizo ni za kweli kiasi gani hasa kwa hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii takribani miezi miwili tu baada ya uchaguzi. Tujadili hali halisi ya watanzania kuelekea mwisho wa mwaka kwa kuzingatia matukio ya hivi karibuni.
Naomba kuwasilisha
Naikumbuka hii hotuba ya Dr Slaa. Na kweli hakukosea maana maafa hayo yanaanza taratibu baada ya miezi michache tu toka kumalizika kwa uchaguzi kwa kupandishwa bei ya umeme kwa 18.5 na hii itafanya bei ya bidhaa mbali kupanda sana ikiwemo pia vyakula na kuongeza hali ngumu ya maisha kwa Watanzania walio wengi. Sasa tusubiri kwenye majaliwa tuone hali itavyokuwa mbaya zaidi baada ya miaka 5.