Kuibuka kwa 'BIBI' Tabora kunaashiria nini?

Apta Kayla

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
324
71
Ameibuka mama anaetoa tiba ya kikombe huko Tabora kwa gharama ya TSH 500, ni muumini wa kikristo {haikutajwa kanisa gani} anatoa maombi kabla ya kikombe. Watu wengi wameonekana kwenye foleni wakisubiri tiba.

Source ITV Hapa na Pale leo.

Je, hii inaashiria nini? WaTZ wengi tuna magonjwa sugu yaliyoshindikana hosptalini?

Wa TZ tumepoteza imani na tiba za Hospitali zetu, au .....?
 
Ameibuka mama anaetoa tiba ya kikombe huko Tabora kwa gharama ya TSH 500, ni muumini wa kikristo {haikutajwa kanisa gani} anatoa maombi kabla ya kikombe. Watu wengi wameonekana kwenye foleni wakisubiri tiba. Source ITV Hapa na Pale leo.
Je, hii inaashiria nini? WaTZ wengi tuna magonjwa sugu yaliyoshindikana hosptalini?, Wa TZ tumepoteza imani na tiba za Hospitali zetu, au .....?

Uhuni tu na wataibuka wengi, wamesoma akili za watanzania, na watatuchezea sana
 
Hii ndiyo fashion mpya, unanunua legitimacy kwa lebo ya "muumini wa kikristo" na maombi, then unaendeleza uganga wa kienyeji na uaguzi.

Kisha unawachaji watu shs 500 tu ili waje wengi, watu wenyewe hawana kitu.

Wakija kushtukia ushatengeneza kibunda na kupunguza unemployment, aidha, ushasaidia watu kwa "placebo effect".

What's not to like? Ingenious, serikali yenyewe haina mfumo wa afya wa kuwapa watu matumaini, so what's wrong with a little miracle here and there.

You just gotta love it.
 
Njaa iliyojaa makanisani. Unavyoona utitiri wa makanisa yenye waumini watatu-kumi ni dalili za njaa na utapeli uliojaa huko mf:- "DECI" nk
 
Duh, jamani kuna mwanamke tabora naye anatoa tiba kwa mtindo wa babu wa loliondo kwa chaji ile ile ya sh. 500 na watu kibao wanakunywa.

Source: Itv
 
Ameibuka mama anaetoa tiba ya kikombe huko Tabora kwa gharama ya TSH 500, ni muumini wa kikristo {haikutajwa kanisa gani} anatoa maombi kabla ya kikombe. Watu wengi wameonekana kwenye foleni wakisubiri tiba. Source ITV Hapa na Pale leo.
Je, hii inaashiria nini? WaTZ wengi tuna magonjwa sugu yaliyoshindikana hosptalini?, Wa TZ tumepoteza imani na tiba za Hospitali zetu, au .....?

Kazi ipo kwa viongozi wa dini waliokwisha kunywa kwani inaweza tokea na wao wakaanza kuoteshwa na kuanza kazi ya tiba, mwaka huu kanisa lote mtageuka waganga wa sh 500 mia5, hakika shetani atawachezea sana. Tubuni na mrejee kwa Mungu mtasalimika na fikra potofu za eti kikombe cha babu
 
Habari wana jf,nipo hapa nacheki taarifa ya habari ya TBC 1naona habari kuu ni kuibuka kwa mwana mama huko Tabora aitwaye Margareth Mutalemwa anayetibu watu wenye magonjwa sugu kama vile UKIMWI,kisukari,mkanda wa jeshi na mengineyo,anatibu kwa kuwapa wagonjwa kikombe ambacho bei yake ni sh 500.Mama huyo anasema ameambiwa na Mungu atoe dawa hiyo kwa watu mbali mbali wenye magonjwa mbali mbali. Source.TBC 1 taarifa ya habari ya saa 2 usiku.
 
Duh, jamani kuna mwanamke tabora naye anatoa tiba kwa mtindo wa babu wa loliondo kwa chaji ile ile ya sh. 500 na watu kibao wanakunywa.

Source: Itv

Mkuu nami pia nimeiona hiyo story(kupitia TBC1)! Yaani sielewi matukio haya mwisho wake utakuaje! Ni kweli ni miujiza ya Mungu yule tunaemwabudu na kumwamini au kuna something else?
 
Nimeona pia ITV taarifa ya saa 2 - huyo mama kawachanganya viongozi wa serikali huko na pia viongozi wake wa dini
 
naona mngeachana na babu kwani yuko remote area na huyo wa tabora yupo town kwahiyo huduma zote muhimu nahisi zipo. mbali na huyo pia kuna dogo wa mbeya naye tayari anaendelea kufanya mambo ya kiuganga pia kuna mwingine media zinampotezea yupo Rombo kwahiyo mpaka sasa tuna waganga wanne na mkristo mwingine arusha eti kamuona Mungu na mwingine kaoteshwa eti 21-may ni mwisho wa dunia, mwaka huu akina kibwetere wataibuka wengi na watapata support ya kanisa.
 
Hata mimi nimeona lakini nahisi utazuka mlolongo mkubwa wa watu wa mfano wa babu kwa madhumuni ya kuchakachua huduma ya babu. Nadhani muda pekee ndiyo utaoeleza nani mkweli nani muongo au wote ni waongo?
 
Nimeona pia ITV taarifa ya saa 2 - huyo mama kawachanganya viongozi wa serikali huko na pia viongozi wake wa dini

nakwambia hiyo bado trela picha lenyewe bado, siku utakapo ona mzee wa upako/maaskofu wa kkkt nao wameanza kugawa gawa dawa ndio picha litakuwa limekolea.
 
nahisi hawa wa vikombe walikuwa wengi sema walikuwa hawajitangazi tu..sasa kuona babu katoka na kila mtu nae anataka kutoka kwa tsh 500...time will tell
 
Jamanie tumecho shwa na hawa matapeli, kama ni mkia hata kenge anao tuangalie niwanani unakata zaidi.
 
Back
Top Bottom