Kuhusu Zoezi la Vitambulisho vya Uraia Kupangiwa Muda wa Ukomo kujiandikisha ni Sahihi?

Dopodopo Kadopo

Senior Member
Jul 23, 2012
120
19
Wadau hili si zoezi endelevu kwa sababu kila siku iendayo kwa mungu kuna raia wanapata sifa ya kupata vitambulisho i.e wanafikisha umri wa miaka 18 na kuna wachina wanaingia kama wawekezaji. Kulikoni kuweka muda wa ukomo wa kujiandikisha?
 
Good observation.
 
Hujaelewa, muda wa ukomo ni kwa sasa, wakishapita nchi nzima utaratibu huo utakua endelevu, ukisema wakae dar tu watu hawataisha maana naamin kila siku watu wanatimiza miaka kadhaa sasa wakifanya kusubiri hawatapiga hatua yeyote, chamsingi wanapita nchi nzima yaani kila mkoa baada ya hapo zoezi litakua linaendelea.
 
kwanini wasianze kuweka ofis kila mkoa kwanza ndio waanze utaratibu wa kuandikisha.
 
Wakuu nimeona kwenye specimen ya kitambulisho cha Taifa kikiwa na 'Expiry date' hatakwa vile vitakavyotolewa kwa wazawa. Kama hivindivyo itakavyo kuwa watanzania wote uraia wao unaexpire hata kama hajaukana?
 
haya sasa yatakuwa makubwa, kwanini kwa wazawa visingekuwa vya kudumu kama vya mpiga kura without expiring date? aah lkn nilisahau sasa vikiwa vya kudumu unajua kaulaji nacho katapungua so ni lazima viexpaye then tutengeneze vingine.
 
Serikali isokua makini kila jambo rafurafu tu hata kama ni zuri;eti mwisho trhe sita;ngoja tuone
 
ikumbukwe kuna watanzania ambao wamesafiri kikazi, wengine wanamalizia kusoma kwenye vyuo vikuu mbalimbali duniani alafu warudi tanzania sasa watu hao watashtakiwa kwa sababu mda wa kujiandikisha umekwisha? aah wapi huwezi kuweka deadline ya kujiandikisha..hawa watu wamefanya hivi ili tu watu waogope wakajiandikishe
 
Hujaelewa, muda wa ukomo ni kwa sasa, wakishapita nchi nzima utaratibu huo utakua endelevu, ukisema wakae dar tu watu hawataisha maana naamin kila siku watu wanatimiza miaka kadhaa sasa wakifanya kusubiri hawatapiga hatua yeyote, chamsingi wanapita nchi nzima yaani kila mkoa baada ya hapo zoezi litakua linaendelea.

Sijaelewa nini ndugu yangu? utaratibu utakuaje endelevu kwa kupita kila mkoa? Hebu niambie hili la vitambulisho vya urai unaweza kulitofautisha vipi na usajili wa vizazi na vifo. Kimsingi hii ingetakiwa iwe idara tu ndani ya rita. Tatizo ni kuwa kila jambo hapa nchini linaendeshwa kwa deals za watu hivyo imekuwa ni mamlaka inayojitegemea. Mbaya zaidi utendaji wake hovyoo kabisa hamna umakini kabisa kwenye kuandikisha watu ukiwa na kitambulisho cha kupiga kura basi wewe inatosha kuitwa rai wa nchi hii. It is just another wastage of resources .
 
haya sasa yatakuwa makubwa, kwanini kwa wazawa visingekuwa vya kudumu kama vya mpiga kura without expiring date? aah lkn nilisahau sasa vikiwa vya kudumu unajua kaulaji nacho katapungua so ni lazima viexpaye then tutengeneze vingine.
Expired date nilazima kwa sababu watu wanakua na kubadilika hivyo kuweka muda ni sahihi kabisa
 
sasa mtu akikua ndio anaexpire kuwa raia? nieleweshe kidogo.

Yaani nina maana watu wanabadilika sura na status zinaweza zikawa zimebadilika.Kwa mfano kama mtu wa miaka 18 anajiregister sasa miaka kumi na tano sura yake imebadilika kabisa na kama ni mwanamke si ajabu akawa ameolewa na kutaka kubadili status yake au ku apdate majina yake au hata status ya uraia wake ukawa tofauti
 
.
umesomeka mkuu.
 
Back
Top Bottom