Kuhusu utaratibu

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Matarajio yangu mko njema wadau wenza.
Katika jamii tunamoishi husussan uswahilini, hua hapakosekani jamaa zako wawili-wa3 ambao mambo yanapokwenda mrama mfukoni basi aidha wewe utamtokea mmoja kt ya hao, kupata karadha ya muazimo wa vijisenti , mambo yako yakikaa sawa una'refund.

Aidha suala hili hua ni mtambuka na hao jamaa zako nao wakwamapo hukutokea wewe, maisha yanaenda.

Kwa upande wangu mimi itokeapo jamaa kanitokea na dharura ya senti ndogondogo mathalani sh elfu 5 mpaka laki 1 , hua napenda muamala huo ubaki kwangu tu na huyo niliempa, hua sipendi nilifikishe hilo hadi kwa wife wangu, kwani nahisi kufanya hivyo ninalinda staha ya jamaa yangu.

Naweza kumfahamisha wife walau hiyo amount ntakayomuazima huyo jamaa yangu itavuka laki 1.
Hivi karibuni nimegundua mmoja kt ya jamaa zangu hata akikuazima elfu 10, basi ni lazima afikishe taarifa kwa mkewe.
Kitu hiki kifupi mimi kikanikwaza na nikaweka azma ya kutomtokea tena jamaa yangu huyo.
Nisingekwazika kama angefanya hivyo kwa amount kama ya elfu 50 kwenda mbele.

Wadau nachotaka kushare nanyi hapa ni KUHUSU UTARATIBU kua alivyofanya huyu jamaa yangu ndiyo utaratibu ? Pengine mi ndiyo nna mapungufu ? Jengine nalotaka kujua je kukopa kwa Shemeji yako (mke wa swaiba wako) bila kumuarifu mumewe ni sawa hakuna tatizo lolote?
Naomba kutoa hoja .
 
duh,ngoja wanandoa waje wakujibu. couz me nikitaka kukopa / kukopwa pesa cna wa kumtaarifu wala kumuomba ruksa!
 
Judgement, apo kimtazamo tuko sawa helo ndogo ndogo haina sababu 'kumchoresha' mshkaji kwa wife au mpenzi wako mnamalizana kiume
apo kwen kumkopa shemeji inategemea pia na kanuni zinasemaje kati yako na shsmjio, kama zinakubali basi haina shida mnaazimana tu kwa nia njema kabisa!

huo ndo mwongozo wangu
 
Last edited by a moderator:
Ni ulimbukeni.....pesa kama hiyo unabana tu moyoni umwambie mwingine ili iweje...Aidai kwa niaba yako?

Samahani natoa maoni tu sijaoa
 
Judgement, apo kimtazamo tuko sawa helo ndogo ndogo haina sababu 'kumchoresha' mshkaji kwa wife au mpenzi wako mnamalizana kiume
apo kwen kumkopa shemeji inategemea pia na kanuni zinasemaje kati yako na shsmjio, kama zinakubali basi haina shida mnaazimana tu kwa nia njema kabisa!

huo ndo mwongozo wangu
Kaizer mwanzo wa ndogo ni kubwa so pesa ni pesa anapaswa kuwa mkweli wi-fi wake
 
Kiongozi Kaizer!
Nithubutu kusema comment yako imenipa faraja, kwamba siko pekee katika mrengo huu wa kulinda staha ya swaiba, hasa inapohusu amount ya karadha ndogondogo.
 
Last edited by a moderator:
Kaizer mwanzo wa ndogo ni kubwa so pesa ni pesa anapaswa kuwa mkweli wi-fi wake
ummu kulthum, tunaposema ndogo na kubwa ni very relative hata kwa mwengine elf kumi ni kubwa , ndo maana hapa tukaainisha kabisa kiwango gani tunamaanisha 'hela ndogo' na kipi hela kubwa (>100,0000).

sasa kama ndo ivo kila nikinunua hata pipi si itabidi nimwambie? lol
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom