Kuhusu Utanganyika: Shetani Unayemjua ni Bora Kuliko Malaika Usiyemjua!

hoja yako ni hoja mfu kabisa; kuna kasoro nyingi za muungano ambazo mimi niliyezaliwa miaka ya sabini ninaziona na siwezi kuwa **** kwa kukumbatia makosa ya babu zangu. Waulize Sudan kusini waliozaliwa katika Sudan moja ni kwa nini waliamua kujiondoa, kisha uje tena na hoja yenye maana. Bora malaika nisiyemjua kwa kuwa siku zote malaika ni mwema, kulikoni shetani yoyote. Wewe na mashetani wenzakomnaopendelea muungano kwendeni zenu. Wana uamsho z'bar wana matatizo yao pamoja na njaa lakini sisi watanganyika una hoja za msingi kuidai Tanganyika yetu.

Mkuu umemlima dozi ya nguvu huyu mshamba; nadhani hatarudi hapa.
  • Hapo pa kijani, kuna mifano mingi sana zaidi ya Sudani. Soviet Union ilikuwa dola yenye nguvu duniani lakini wakati ulipotimia wakaona matongotongo ya muungano wao unawachelewesha wakusambalatisha. Kwani walukwenda motoni?
  • Hapo pa bluu kama ana imani ya kweli atakuelewa lakini kama anaabudu mashetani kwake malaika daima ni tishio
  • Hapo pekundu ndo panatisha zaidi. Huyu jamaa kama anamfahamu shetani na bado akaamua kumkumbatia kwa hofu ya malaika hata kama hajawahi kumwona basi ni mtu hatari mno na hawezi kuwa na mawazo yanayorutubusha vuguvugu la mabadiliko tunayohitaji nchi hii.
 
Post union days(Mungu tu epushe), Tanganyika is more likely to fall into religious polarization/strife unlike Zanzibar which is 'religiously' homogeneous being 99 % Islam.
 
Post union days(Mungu tu epushe), Tanganyika is more likely to fall into religious polarization/strife unlike Zanzibar which is 'religiously' homogeneous being 99 % Islam.

Definitely the opposite is what is true and you must be awfully blind not to perceive this vivid reality or you are rather trying to play monkey tricks to yourself. What are your parametric signs suggesting that Tanzania mainland is prone to fall into any tragedy of religious polarization should Zanzibar quit union? What is Zanzibar contributing to weather the so called religious strifle in Tanzania mainland? Haven't noticed the terrible fundamentalism in the isles always restrained by the union? Blind of the move by our avaricous statesmen of getting disseminated into mainland the seeds of of hate and coflict from the isles?

As far as I am concerned should Zanaibar's manoeuvre out of union come true then for sure we witiness the nativity of a second Somalia/Afganstan almost over night and even worse! So comrade, go and deceive those foolish islesmen and none on the elite side of this land!
 
Mkuu, kwa kawaida ukianzisha mada basi unajivika jukumu la kuratibu mjadala in a fair and objective manner. Kama mwanzishaji mada na kwa hiyo mwendeshaji majadiliano hukupashwa kuwa wa kwanza kurusha kauli za kashfa kwa wachangiaji. Hapo pekundu pamekutambulisha kama ifuatavyo:
  1. Una tabia ya udictator na unadhani uonavyo wewe basi ndiyo ukweli. Who are you hata ujidhani kuwa mtazamo wako ndiyo bora kuliko wa wengine?
  2. Wewe yumkini ni tunda na sehemu ya uozo ambao watanzania tunataka sasa kuuondoa. Mwenye akili timamu katu hawezi kukubaliana na kichwa cha habari ulivyokiweka: "Kuhusu Utanganyika: Shetani Unayemjua ni Bora Kuliko Malaika Usiyemjua!" Katika hili shetani ni nani na malaika ni nani? Unataka kusema kwa kuwa chama fulani (kwa mfano) ndo kimetawala miaka mingi hata kama kimepoteza dira na watu wanaona nchi inaenda vibaya tukiache kitawale milele kwa sababu ndiyo shetani tunayemjua? Infalibility ya muungno wa namna hii imeletwa na malaika yupi?
Kama niliyoandika juu yako hapo juu hayakuhusu basi napata mashaka sana kama wewe kweli ni mtanzania na unayeishi ndani ya mipaka ya nchi hii.
Mkuu naona umekuja kushambulia character kuliko kujibu hoja! Wewe Utanzania wako una mashaka zaidi kwa kuwa huoni kuwa tunakoelekea ni hatari kwa mustakabali na mshikamano wa taifa letu! Unafikiri Muungano ukivunjika tu basi matatizo yatakuwa yameisha! Kawaulize UAMSHO kama tatizo lao ni Muungano kuvunjika tu basi, hakuna ajenda nyingine. Na tatizo lako unafikiri ni wale waandamanaji tu, ukweli ni kwamba kuna mkono wa viongozi wa Serikali na msukumo kutoka nje! Watu wadogowadogo kama wewe maskini mmechukuliwa tu na upepo! Pole sana!!
 
Wakuu,
Watanzania wengi wamezaliwa baada ya Aprili 26, 1964 kwa hiyo hawaijui Tanganyika, wanasoma tu kwenye makabrasha. Kama hiyo si sahihi sasa basi Watanganyika walioishi Tanganyika huru iliyodumu kwa miaka takriban 4 (1961-1964)
Nawasilisha!!

Kila nikijiuliza nini ilikuwa mantiki ya kubadilisha jina la Muungano kutoka , Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huwa sipati jibu sahihi.

Mazingombwe Ya Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar yalianza pale ilipopitishwa sheria ya kuridhia muungano na Bunge la Tanganyika na baadae kiini macho kingine ilikuwa kubadili jina la asili la Muungano..Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kulichakachua kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hapo ndio mleta mada anapata nguvu ya kusema Tanganyika haipo.

Lakini mleta mada anapenda mazingombwe.
Bisect jina TanZan ia harafu tuone jeuri ya kusema Tanganyika imepotea utaipata wapi?

Nini usanii wa jina Tanzania?
Tanganyika imehifadhiwa katika jina Tanzania kama lilivyohifadhiwa jina Zanzibar.

Sasa nini kilipelekea Tanganyika kuitwa Bara au Tanzania bara?

Wadanganye hao watoto wetu wanaosoma shule fasta fasta na siku wakibahatika kupitia hapa pia watajua walirushiwa changa la macho.

UAMSHO wametusaidia sana katika kutufanya kulitumia tena jina Tanganyika. Ndio sababu mmeanza kuwabambikizia "ugaidi" na uchomaji moto makanisa"

Hamtaki Muungano wenu wa kero kudadisiwa....Mtu zimeanza kuamka, hamna vya kuwadanganya. Kubalini yaishe!
 
Tanganyika ipi unayoifahamu wewe?
Kabla ya Wajerumani hakukuwa na nchi inayoitwa Tanganyika. Na wakati wa utawala wa Wajerumani kulikuwa na Deutsche Ostafrika, ikiwa na maana ya Afrika Mashariki ya Kijerumani, iliyojumuisha Rwanda na Burundi.
 
Bora MALAIKA na mwenyezimungu atuondolee na atuepushe na shetani maana ndio chanzo au sababu kubwa ya kuleta matatizo yote haya mnayoyaona na mliyoyasikia.

Shetani ndio mchonganishi
Shetani ndio anasababisha kujenga chuki na ubaguzi
Shetani ndio anashawishi viongozi kutokuijali nchi
Shetani ndio mwenye kutenganisha watu
Shetani ndio chanzo cha mafisadi
Shetani ndio chanzo cha kuharibu jamii au kupotosha jamii
Shetani ndio chanzo cha umasikini

Bora MALAIKA kuliko SHETANI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom