Kuhusu simu za kichina TECNO HD Series

Unafikiri hii simu ninayozungumza iko kama hizo zinazopiga kelele??

Za kelele sio kama hazipo ila sio kwa brand ya TECNO hususan toleo hili la HD. Ni mchunguzaji mzuri wa simu na nina interest hasa katika maswala haya.

I have to admit hizi simu za TECNO HD series nimezikubali.

Ok,
Ukiandika meseji au kama hapa JF unapost kitu, baada ya nukta hua inaanza na herufi kubwa??
Pili wakati wa kutuma meseji inakuuliza kama unataka kusevu au kutuma moja kwa moja?
Katika vyote jamaa zako wameshindwa hapo tu!!!
 
Ok,
Ukiandika meseji au kama hapa JF unapost kitu, baada ya nukta hua inaanza na herufi kubwa??
Pili wakati wa kutuma meseji inakuuliza kama unataka kusevu au kutuma moja kwa moja?
Katika vyote jamaa zako wameshindwa hapo tu!!!

kuhusu kuandika msg na kuanza kwa herufu kubwa wakati wa nukta inakataa inakuja herufi ndogo mpaka ubadilishe mwenyewe. ila kila unapotuma msg haikuulizi kuhusu ku isave inajisevu yenyewe kama simu nyingine.
 
kuhusu kuandika msg na kuanza kwa herufu kubwa wakati wa nukta inakataa inakuja herufi ndogo mpaka ubadilishe mwenyewe. ila kila unapotuma msg haikuulizi kuhusu ku isave inajisevu yenyewe kama simu nyingine.

Hayo mawili ndio yanayoniuzi kwenye mchina!!
Anyway, we endelea nazo tu kaka,
Mradi umezipenda haina mbaya!!
 
daaah mimi najua mchna anajua sana kutengeneza vitu almost vitu vingi ikiwemo hata iphone vimekuwa designed ni u.s but production ni china.
Tatizo la simu za kichina ni operating system wanayo tumia. Mimi nikikutana na simu ya mchina inayotumia android au symbian mbona ntanunua kwa roho safi.
O.s wanazoweka kwenye simu zao ovyo sana hiyo techno hd sijaitumia lakini am sure itakuwa inatumia o.s zao zile zile na je ina internal memory ya ngapi au 300kb kama kawaida yao
 
Ndugu yangu mmeingiza makontena mangapi?naona mnajitahidi kuzitangaza endeleeni labda mnaweza mkauza mzigo wote!

Mkuu nilinunua 98,000 ila maduka mengine mpaka 110,000 unatakiwa utembee maduka mengi upate kuelewa bei nzuri.

Nimenunua bei hiyo kwa Tanga lakini kwa dar nina hakika itakuwa pungufu ya hapo.
 
To be honest sio kila anachotengeneza mchina ni kibovu kuna vengine vina ubora unaostahili.

Najua mkuu unazungumza hivyo kwa kuwa hujawahi kuitia mkononi hiyo simu ninayozungumzia ila katika pita pita zako madukani ijaribu kidogo then utarialize in terms of quality.

Pikipiki yangu mchina aina ya sanya ambayo pia imechukua soko kubwa hasa mwanza kutokana na kuwa na ubora unaostahili.

Kwa msimamo huu sio kwanba nakataa kabisa kwamba mchina sio fake ila kuna baadhi za bidhaa wanazotengeneza zina ubora unaostahili.

Hili halina shaka kwani naamini wadau wengi wataniunga mkono.
Mimi toka nimeanza kutumia simu nimekuwa mraibu mkubwa wa simu za nokia toka hungary au finland lakini kuna rafiki yangu mmoja kanunua TECNO phone,aisee nimeipenda.Image resolution nzuri,sauti yake inarekebishika vile upendavyo which means haina makelele labda upende mwenyewe,ina support internet vizuri sana,jamaa kaiangusha mara kibao lakini mzigo upo fresh kabisa.
 
Wadau naomba kuwakilisha kama ifuatavyo:

Nilikuwa natafuta simu aina ya samsung double line, nilipofika dukani muuzaji akaanza kunisifia kuhusu toleo jipya la TECNO HD na akanipa modeli HD 51 kwa kweli i was so impressed na performance yake kila kitu basic kipo na camera yake ni 1.3 mega pixel lakini quality ya picha yake it's amaizing very clear.

Simu inakuja na battrey 2,earphone,charger pamoja na cover yake original. Baada ya kuanza kuzifuatilia kwa umakini nikakuta watu wengi wanatumia hii brand ya TECNO katika simu za kichina kushinda brand yoyote ile. Nchi ya jiran kenya hususan Mombasa zimeteka soko kubwa la watumiaji wa simu.

Ukiacha mambo mengine ina kamata internet bila ya matatizo yoyote na ina java ambayo unapata software nyingi za ku down load kwenye neti.

Wenye experience zaidi watujuze kuhusu hizi simu na upatikanaji wake kwa wingi hasa hizi HD series
Ni kweli mkuu uliyo ya sema tena ni nzuri kuliko hata baadhi ya sumsung mfano mimi natumia sumsung GT-C3222 hii simu haifai kabisa kwa watumiaji wa internet kwani haikuruhusu kuistall software nyingi tu mfano opera mini baadae nikaona nichukue Tecno nijaribu daah ziko fresh sana mpaka najiuliza kwanini hizi simu zinauzwa bei ya chini sana yaani ni mara nne ya sungsung ambayo ilikuwa inanisumbua.......asante mchina ulie tengeneza Tecno
 
Mchina ni mchina tu!!
kuna jamaa mmoja akiuzaga gari anaanza kukuambia lina kiti, kiti, una adjust, adjust mbele na nyuma, lina side mirror, side mirror una adjust, taa zaidi ya moja, yaaani makorokoro kibao ambayo ni ya kawaida tu mkuu!!
Simu inategemea na matumizi na hobby yako.
hahahahahahahahah hii kali lakini kwa Tecno mkuu mchina amejitahidi nimetumia mchina lakini kwa hizi Tecno nimewakubali...zingine ulikuwa ukinunua usipo angalia hata siku mbili haimalizi mara mic imekufa net ndiyo usiseme kabisa.....
 
Back
Top Bottom