Kuhusu posho ya kusimamia mtihani kidato cha nne 2012 wapendwa,wilaya kilombero kuna ufisadi!!!!!!!!

JULIUS MBIAJI

Member
Dec 13, 2011
76
11
Nimesikitishwa sana na tabia ya viongozi wa Idara ya elimu idara ya sekondari ya kupunguza baadhi ya wasimamizi wa mitihani kwa kisingizio cha mitihani kupungua.Halmashauri nyingine hakuna mambo kama haya na once mtu ameteuliwa kusimamia mtihani basi ni hadi mitihani yote ikamilike sasa kinachofanyika huku ni tofauti.Je BARAZA MNATUSAIDIAJE?Pia mwaka jana waliita watu wengi kwenye semina ili waombe fedha nyingi kutoka baraza na baada ya watu kufika vituoni walipunguzwa kwa kisingizio cha kuzidi idadi ya vyumba haliyakuwa wenyewe ndiyo wanaokagua vyumba vya mitihani.Wakuu naomba mawazo yenu ili tuweze kutatua matatizo haya.Natanguliza shukrani za dhati kwa ushauri wenu na taarifa zaidi kama nitapata kupitia jukwaa hili adhimu.
 
kaka ndio walivyo hao mi mwenyewe walitaka kunifanyia hivyo mwaka jana.mpankuly na msuya ndo mambo yao
 
acha tu naskia malipo eti ni laki tatu YAANI issue ya kusimamia ni full UBABE kuna wakufunzi wamenunua hizo chance kwa am DEO ... Afu msaada tutani hivi inakuwaje kuna walimu wana simamia mitihani ktk Shule za private wameshika wanafunzi wakiigilizia wanafunzi wakaleta UBABE, wasimamizi wachukue hatua Sasa mmiliki wa hiyo Shule anawatishia Hao walimu eti atawaamishia kijijini na hawatasimamia mitihani tena na DEO Yuko upande wake hapo inakuwaje?
 
Wala siyo laki 3.Wengi wetu jana tumelipwa sh 195000.Inafaa kuchukua hatua kumaliza hili tatizo.Hawako makini na maisha ya Walimu na hapa ndiyo mahali pekee pa kutupozea machungu wanatuchezea!!!!!!
 
kaka ndio walivyo hao mi mwenyewe walitaka kunifanyia hivyo mwaka jana.mpankuly na msuya ndo mambo yao
Sasa mwaka huu wamenipunguza mimi na isitoshe mwaka jana waliniteua kusimamia na baada ya kuripoti kituon nikakutana na barua ya kusimamishwa kusimamia mtihani.Hawa hawatutakii mema zaidi wanajinufaisha wenyewe kupitia migongo ya watu.It is high time to nock down these irresponsible leaders and their system.
 
Malipo ya mtihani yanategemea idadi ya sessions. Mfano wanaosimamia kwenye shule za masomo ya science wanaofanya practicals wanapata fedha zaidi kuliko wa upande mwingine.
 
Back
Top Bottom