Kuhusu nyumba za madaktari jk si mkweli

Jiwe Linaloishi

JF-Expert Member
May 24, 2008
3,736
2,137
Kwenye hotuba ya rais mwisho wa mwezi alizungumzia kuhusu ujenzi wa nyumba 700 za madaktari nchini, ukweli ni kwamba huo mradi upo lakini si wa serikali ni mradi unaosimamiwa na kufadhiliwa na GLOBAL FUND kupitia taasisi ya Mkapa Foundation. kwahiyo kikwete kujitapa kuwa ule mradi wa nyumba za madaktari ni wa serikali si kweli ni kudanganya Uma. na ni nyumba za wauguzi wa zahanati na vituo vya afya siyo za madaktari. kana kuna mwenye wasiwasi afike pale Mkapa Foundation atapata ufafanuzi yakinifu.
 
Kiongozi awaye yote siku zote hupewa habari na wasaidizi wake. Kama wakimpatia habari za uongo
hakika kosa si la mtawala. Ila kama kuna habari ya uhakika basi sisi wenye nchi tuna hiyari
ya kuiscan na kuiweka hapa bila woga. Hiyo inamfanya rais ajue kipi ni kipi.

Rais kwa vyovyote vile hawezi kwenda kila mahali na kuulizia ulizia habari. Ila asiwe mvivu, bali
awe na ki system chake cha siri cha kumpatia mambo muhimu.

Nakumbuka watoto wa Mwl. walikuwa wakimpa baba yao viswahili vya mtaani, n.k Ndo maana
Mwl. Nyerere ilikuwa si rahisi kutoa taarifa za uongo. Kuna wakati alifika mahali akauvuta mgomba
ukang'oka kwani alikwisha ambiwa kuwa pale hakukuwa na shamba ila kiini macho. na kuwa ile
migomba ilikuwa imepandwa asubuhi tu ili kumridhisha macho.
 
Kwasababu alishadanganywa mara nyingi huko nyuma alitakiwa awe makini hasa kwenye kipindi chake hiki cha mwisho si kuamini kila kitu anacholetewa ndio maana watu wanamwona dhaifu na mzembe kwa kutokuchukua hatua kwa wakati muafaka. yetu macho
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom