Kuhusu Ndege Airbus Aliyoongelea Rais Magufuli

John Kachembeho

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
560
386
Airbus Prices.PNG


Tuiangalie hii A320
Kwa mujibu wa bei mpya za January 2016 zilizotolewa na Kampuni la Airbus, ndege hii mpya kabisa ina bei ya dola za kimarekani milioni 98. Hii ni sawa na takribani shilingi za kitanzania Bilioni 210 (Katika Trilioni moja unapata ndege 4 kama hii unabaki na chenji).

Ndege hii ina uwezo wa kubeba abiria 150 katika madaraja mawili (Mfano Business class na Economy class), lakini kwa mbananisho inaweza kubeba hadi watu 180 kwa mara moja.

Je nia, uwezo na sababu za kumiliki ndege kama hii ndani ya shirika letu la ndege tunazo??
Wakati wa kuamua na kutenda...
Airbus Prices.PNG
Airbus-1.PNG
Airbus-2.PNG
Airbus-3.PNG
Airbus-4.PNG
Airbus-1.PNG
Airbus-2.PNG
Airbus-3.PNG
Airbus-4.PNG
 
Tumalize kwanza matatizo ya huduma muhimu ndo tuje kusumbuaana na mambo ya ndege
Wananchi wote wapate maji safi na salama
Watoto wamalize la 7 WANAJUA kusoma na kuandika
Tukimaliza hayo na mengineyo muhimu tuje sasa tuulizane ni ndege ipi tununue hii au ile
 
1. Fedha za Escrow zingetosha kununua ndege moja na Salio lingebaki.


2. Fedha za Vitambulisho feki vya Uraia ikiongezwa kidogo ingetosha kununua hii ndege.


3. Posho za Wabunge zikiongezewa hela kidogo zinatosha kununua hii hela.


4. Fedha za Safari za Nje kwa mwaka Jana tu zingetosha kununua hii ndege na fedha zikabaki.



Uwezo tunao wa kununua Airbuss tunao.. Nia ya kununua hatuna.. Sababu za kununua tunazo..
 
Mimi Ni UKAWA ila Namuunga Mkono Mh. Rais kununua ndege hizi, endapo serikali itaziagiza yenyewe bila kupitia kwa Agent najua bei hiyo itashuka sana na najua huwa kuna discount ikiwa nchi inanunua ndege Zaidi ya moja.

Mungu mbariki Mh. RAIS, wale wenye nia mbaya na Mh. Rais wetu uwaadhibu haraka na mapema Zaidi.
 
Tumalize kwanza matatizo ya huduma muhimu ndo tuje kusumbuaana na mambo ya ndege
Wananchi wote wapate maji safi na salama
Watoto wamalize la 7 WANAJUA kusoma na kuandika
Tukimaliza hayo na mengineyo muhimu tuje sasa tuulizane ni ndege ipi tununue hii au ile
Hivi una akili sawa sawa kweli?
 
Mkuu 90% ya wana JF ni wana ukawa tokea zamani, ila jf wanajielewa sana . Nyundo wanaiita nyundo na si msumeno, magu akifanya japo jema la maslahi tutakubali, nina uhakika huyu mbana matumizi hatatumia mawakala
Mimi Ni UKAWA ila Namuunga Mkono Mh. Rais kununua ndege hizi, endapo serikali itaziagiza yenyewe bila kupitia kwa Agent najua bei hiyo itashuka sana na najua huwa kuna discount ikiwa nchi inanunua ndege Zaidi ya moja.

Mungu mbariki Mh. RAIS, wale wenye nia mbaya na Mh. Rais wetu uwaadhibu haraka na mapema Zaidi.
a
 
Mbananisho umesema kutoka 150 hadi 180!!!! Haya maisha ya kuzoea daladala za Ubungo Kariakoo unayaleta hadi kwenye ndege!!!!

Mbananisho unafanyika katika mashirika ya ndege ya bei nafuu, mfano FastJet. Sio mbaya sana ila bila mbananisho ni comfortable zaidi!
 
Utakavyojua watanzania walivyokuwa wezi iweke sasa kwenye mpango wa manunuzi uone kitakachotokea.Kama haikuletwa ya mwaka 1979 (repaired)basi serikali itanunua kwa $250 million pesa nyingi zikijumuisha upembuzi yakinifu na posho za wataalamu.
Kaka huu upumbavu ndio unaoturudisha nyuma, kwanza hapo lingeenda jopo la watu kwenda kuikagua ndege, ilihali hawana utaalamu,wangekaa wiki moja na kulalahotelini
 
Apige chini wale mazoba pale ATC kwanza....

Arudishe vijana wetu wengi (Pilots) wanaorusha ndege kule West Africa na South Africa...

Atafute kichwa kimoja (asilete uchama hapa) na napendekeza alete Kijana ambaye anaweza kimbizana na fitna na mihangaiko ya kutafuta masoko (sio wa kukaa pale Aviation House tu)..

Tununue Airbus mbili tu kwanza na vindege viwili vidogo... Uwezo huo tunao, tukitenga Trillion 1 tu naamini ATC itaamka..

Ila cha muhimu zaidi, hakikisheni kule Zanzibar mnakumaliza salama na kuwe na utulivu.. Kununua hizi Airbus tunatarget kukuza utalii wetu na almost 70% ya wageni wanaokuja nchini ni watalii na 60% kati yao lazima waende Zanzibar kupumzika kabla ya kurudi kwao... Mkipuuzia ya Zanzibar na mkanunua hizo ndege tutegemee hasara tu...
 
Mambo my sister kipenzi,
Ni kweli jana nilisikiliza hotuba ya Magu kasema wafanyakazi wote wa ATCL waondoke hawezi kuwakabidhi ndege zake mpya
Kuna cheche zimeanza kuwa huko ATCL.
We subiri kidogo tu utaanza kuona moshi
Ukiona moto juu ya Paa . Basi kila kitu kimesafishwa.

Nisiseme sana .[/QUOT
 
Back
Top Bottom