Kuhusu mgomo wa madaktari: John Mnyika

serikali haina pesa...kugoma kwenu hakuna matunda na mtaumiza wananchi bureee, serikali ingekuwa na pesa ingehsawapa pesa mnazodai...nakwambia hawana pesa kabisa...

Zile za kuwapa wale wanaokaa bungeni walizipata wapi?
 
nimemdharau mnyika kupita maelezo...hajawahi kuugua akaona uchungu wa kuugua, wala hajawahi kufiwa kwa kukosa daktari....ni mjinga kupita maelezo....na nikiona mtu anaongeahayo mbele yangu hakika yake nitampiga ngumi nyingi sana...inakera kusikiliza.

Kipi kigumu hapo? anachofanya Mnyika ni kujaribu kuleta tiba ya kudumu, wewe unachofanya ni kuangalia hali ya sasa, bila ya kujali kama itajirudia tena mwakani, na miaka ya baadae. Hiyo ndio tofauti kubwa baina yako na Mnyika.

Kutokana na takwimu zilizopo, allocation ya bajeti ya wizara ya afya kwa mwaka kwa wastani ni sawa na kutenga Dollar 20 kwa kila mtanzania "kwa mwaka", kumhudumia kila Mtanzania anapoenda hospitali, dispensary n.k. Kwa maana hii, kwa kila siku ya mwenyezi mungu, serikali inamtengea kila mtanzania senti 5 (tano) za dollar kwa siku, iwapo kila mtanzania ataenda hospitali au kliniki kutafua huduma ya afya kila siku. Lakini kwa vile watu hawaendi kila siku kutafuta huduma za afya, tuseme basi kila mtanzania anaenda kutafuta tiba mara moja kwa mwezi; hivyo, ina maana kwamba serikali imekutengea wewe na kila mtanzania mwingine dollar moja na senti 66 ($1.66) kwa mwezi. Je, fedha hizi zinatosha kukupatia wewe mtanzania huduma ya maana kila unapoenda kwenye kituo cha afya au hospitali katika Tanzania ya leo? Na usisahau kwamba hizi dollar 20 kwa kila mtanzania kwa mwaka, ambazo ndio nimepigia mahesabu ya dollar 1.66 kwa siku, pia ni humo humo kuna mishahara ya madaktari na wauguzi, ununuzi wa vifaa, ulipaji wa harama za umeme, safari za wakubwa kwenda kutibiwa nje, posho, mishahara ya madaktari na wauguzi, n.k.

Ukiamua kutulia na kuzitazama hesabu hizi kwa jicho la ndege badala ya jicho la samaki ambalo kuona kwake ni kushoto na kulia tu, utagundua haraka sana kwamba, chini ya mfumo wa sasa, sio madaktari, wala wagonjwa wanaonufaika. Hivyo basi ni sahihi kwa wao kugoma sasa, ili kuokoa hali ya kesho, hasa kwa kuzingatia kwamba sekta hii inaendeshwa na fedha za walipa kodi. Na kwa mtazamo wangu, ni hayo ambayo Mnyika na wengine wote bila ya kujali vyama vya siasa, wanavitetea.
 
Serikali isiwapuuze madakitari ni vema ikauchukua na kuutumia ushauri wa Mh Mnyika kwa masilahi ya watanzania wote.
 
Asante kwa kauli hiyo bwana Mnyika. Lakini sijaelewa kidogo, hiyo ni kauli ya chadema iliyotolewa na Katibu wake wa Itikadi Bwana Mnyika au ni kauli ya Mnyika na msimamo wake yeye kama Mbunge kwa niaba ya chadema. Maana nikiisoma naona kama anajielezea zaidi yeye mwenyewe. Ni maoni tu....
 
Watu wengi wamekuwa wavivu wa kufikiri sana...sijui ni kwa nini. Au wamelewa mabaki na makombo ya mafisadi au ndo mafisadi wenyewe..inakera.
Ni kweli wananchi wanakufa kwa kukosa huduma za madaktari. Lakini serikali wanafanya juhudi gani kuumaliza mgomo huo?haitoshi wala haiingii akilini kumwambia mwanao anayestarve kuwa hauna pesa..unatakiwa kuwa na majibu ya maana na kuonyesha nia ya kumpa chakula na sio blabla tu. Kigwangala ni mmoja wa madaktari vijana walioamua kwenda bungeni kula mshiko wa maana ikiwa ni pamoja na posho ya 280000 kwa siku..halafu mkirudi huku mnasema madaktari waendelee na kazi..watoto wa wanasiasa wanasomea st something ila wa professionals wengine kwa wingi wao wanasomea st kayumba na mnaona ni sawa. Si sawa hata kidogo...nchi ina pesa na resource za kutosha,kama nchi imekushindeni achieni madaraka ili wengine waiendeshe. Budget ya posho kwa mwaka huu ni zaidi ya billioni 900 na zingine ndo zinaliwa huko davos halafu mnasema hatuna pesa!!!wananchi wanaojiita wanyonge linapokuja suala la kura wanapigia majambazi na wezi kwa kupewa kofia na khanga..sasa hivi inatakiwa wananchi tuungane tuandamane nchi nzima kwa kuwa tuna pa kuanzia..kama hatuandamani mi naona madaktari waendelee kudai haki zao hata kama ni mpaka 2015 sawa..tutakaobaki tutachagua serikali makini na mambo yatabadilika.
 
Mgomo wa madaktari unaoendelea hivi sasa umedhihirisha kwamba tuna serikali dhaifu yenye ombwe la uongozi. Haiwezekani wananchi wakawa wanakufa kwa kukosa matibabu stahiki na wengine wakipata madhara kutokana na kuchelewa kupata matibabu sababu ya mgomo wa madaktari halafu viongozi wenye dhamana hawachukui hatua sahihi.

Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye mwenye dhamana kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 33 ndiye kiongozi wa shughuli za serikali na ibara ya 35 shughuli zote za utendaji wa serikali zinatekelezwa na watumishi wa serikali kwa niaba ya Rais; ameondoka kwenda nje ya nchi mgomo ulipoanza na hakuna kauli yoyote mpaka sasa toka kwa Makamu wa Rais wala kwa Ikulu.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda badala ya kwenda kwenye eneo la mgomo na kuzungumza na madaktari naye ameishia kuzungumza na vyombo vya habari. Waziri wa Afya Dk. Haji Mponda na Naibu Waziri Dk. Lucy Nkya nao jana wamezungumza na waandishi wa habari badala ya kwenda kukutana na madaktari na kuzungumza nao kuhusu madai yao ya msingi.
Kwa upande wetu CHADEMA tulitoa kauli tarehe 25 Januari 2012 ya kutaka serikali ichukue hatua na tuliona tuipe serikali nafasi ifanye kazi yake hata hivyo serikali haionyeshi kuupa uzito unaostahili mgogoro huu wenye kuathiri hali za wagonjwa na maisha ya wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Tuliacha kwenda katika eneo la mgomo kukutana na madaktari katika siku za awali kuepusha suala hili kutafsiriwa kuwa ni la kisiasa. Hata hivyo, kuchelewa kwa serikali kukutana na madaktari kunahitaji hatua za pamoja. Dhamira yangu kama mwananchi, mbunge katika mkoa wa Dar es salaam na kiongozi wa chama cha siasa naumizwa na hali inayoendelea. Ni vigumu kuweza kuendelea na majukumu ya kibunge na ya kichama katika masuala mengine wakati serikali iko legelege katika suala ambalo linahusu uhai wa wananchi wenzangu uko mashakani.
Hivyo nawajibika siku ya leo kuelekeza nguvu katika kuungana mkono na madaktari katika madai yao ili kuishinikiza serikali kuweza kutuma ujumbe mkubwa kukutana na madaktari leo au kesho. Na iwapo serikali haitakutana nao katika muda huo, itabidi uongozi wa kambi ya upinzani bungeni ukiwa ni serikali kivuli na uongozi mkuu wa CHADEMA ukiwa ni chama mbadala kuweza kukutana nao.
Natambua kwamba uzembe na ufisadi katika serikali kwenye sekta ya afya unaligharimu taifa na maisha ya wananchi. Hivyo, CHADEMA inaitaka serikali kukamilisha kwa haraka majadiliano na madaktari na kutimiza madai yao ili kuepusha madhara zaidi kwa umma.
Nawapa pole wananchi ambao wameathirika na migomo inayoendelea na kuzingatia kwamba mgomo huo umesababishwa na udhaifu katika serikali.
Natoa mwito kwa umma wa watanzania kuwaunga mkono madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya katika hospitali na zahanati za umma kama sehemu ya kuboresha huduma katika maeneo husika.
Madai ya madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya nchini yasiposhughulikiwa kwa wakati na kwa ukamilifu watumishi husika wanaweza wasiwe kwenye mgomo wa wazi kama ilivyo kwa baadhi ya hospitali na zahanati nchini lakini wataendelea na migomo baridi kwa kutoa huduma mbovu au kuacha kazi kwenye maeneo ya umma na wengine kwenda kufanya kazi nje ya nchi wakati kukiwa na uhaba wa watumishi nchini.
Aidha, pamoja na migomo inayoendelea, naendelea kutoa rai kwa madaktari na watumishi wengine wa umma kuhakikisha maisha ya wagonjwa walio katika hali ya hatari yanaokolewa.
Nimezungumza na viongozi wetu wakuu kuhusu suala hili na natoa mwito kwa wadau wote kuunganisha nguvu katika kuisimamia serikali kushughulikia madai ya madaktari na wafanyakazi wengine wa sekta ya afya kwa haraka ili kuepusha madhara zaidi kwa umma.
Wananchi wenzangu wa Jimbo la Ubungo na umma kwa ujumla uzingatie kwamba tangu Mwalimu Nyerere aondoke madarakani mwaka 1985, Serikali ya CCM imeongeza wingi wa majengo mbalimbali kwenye sekta ya afya hata hivyo imeshindwa kusimamia utoaji bora wa huduma za afya katika zahanati, hospitali na vituo vya afya. Kutokana na mfumo mbaya wa usimamizi wa sekta ya afya, misingi imara ya kuimarisha sekta ya afya iliyowekwa baada ya uhuru imevunjwa na kubomolewa ikiwemo katika masuala yanayohusu kujali maslahi ya watumishi wa umma katika sekta hii muhimu.
Hali hii imefanya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa na nakisi ya watumishi asilimia 48% na takwimu zinaonesha kuwa 18% ya wafamasia, 15% ya madaktari, 13% ya madaktari wasaidizi waliacha vituo vyao vya kazi na kwenda kutafuta kazi kwenye mashirika ambayo yanalipa mishahara mikubwa na mizuri. Nakisi hii itaongezeka zaidi iwapo madai ya msingi ya madaktari na watumishi wengine hayatashughulikiwa na serikali itaendelea kuchelewa kushughulikia migogoro na migomo mingine inayoendelea.
Ni imani yangu kwamba serikali ikiwa na dhamira inaweza kuongeza mishahara kwa watumishi wa sekta ya afya ili kuweza kuwavutia wataalamu kubakia nchini badala ya kwenda kugoma au kwenda kutafuta kazi nje ya nchi kutokana na malipo mazuri huko. Hii ni pamoja kuwezesha malipo ya mazingira magumu kutolewa kwa watumishi wa afya wanaofanya kazi katika maeneo na kada maalum.
Kwa sababu hii, leo sitashiriki kikao cha Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kinachoendelea ili kupata wasaa wa kufuatilia kwa karibu suala hili na kuwasiliana na viongozi wenzangu kwa ajili ya hatua zaidi za pamoja.
Wenu katika utumishi wa umma,

John Mnyika (Mb)
 
DSC06696.JPG Madaktari wakiwa kwenye moja ya mikutano yao Don Bosco.
 
kuhamasisha mgomo wa madaktari ni upu.mbavu uliopitiliza....madaktari wanapata mshahara mwingi kuliko wafanya kazi wengine...madaktari sio ndo watu muhimu kuliko wafanyakazi wengine wa kitanzania...bila watu wengine hapa tz madaktari pia wanaweza kupata matatizo mengi,namaanisha kuwa tunaishi kwa kufaidiana na kutegemeana...mimi sio daktari lakini kwa huduma yangu daktari anaihitaji sana bila hiyo anaweza kuishi vibaya na hata kupoteza maisha...mwalimu, polisi, na mfanya kazi yeyote anacho kitu ana contribute kwa taifa na kwa wananchi kwa namna moja au nyingine, aina fulani ya wafanyakazi ikijiona wao ni wa muhimu kuliko wengine hapa nchini ni ujinga usio na dawa....

kwa sasa hivi ninavyoongea serikali haina hela, kila mtu hilo analijua, magari mengi tu ya serikali yamepaki, hawana mafuta kuendesha....katika wakati mgumu kama huu, tunatakiwa kushare poverty, kidogo tulichonacho tunatakiwa tugawane ichoicho hata kama ni kidogokidogo...kundi moja lisitake kupata kikubwa kwa imani kwamba wao ni wa muhimu kuliko wengine....je? daktari ni wa muhimu kuliko walimu na polisi? polisi wanapata sh ngapi, walimu wanapata sh ngapi? secta zingine zinapata sh ngapi?...ujinga huu nimeulaani vibaya sana, kwasababunimeshuhudia kwa macho yangu wagonjwa wakifariki hospitali kwasababu ya mgomo huu..

dhambi hii madaktari wanafanya itawarudia, kama wamesababisha watu wamekufa, wao pia watakufa tu siku moja na watakosa hata wa kuwazika...Mungu ibariki |Tanzania.....

Du sijui kama unaushirikisha ubongo wako wabunge kujilipa 200000 kwa kikao kimoja na kwa Siku wanakaa hadi kikao vitatu wanajilipa na pesa diem anakusanya hadi zaidi ya laki sita kwa Siku ambao ndio salary ya Daktari Hii ni Sawa blandina nyoni Karibu mkuu wizara ya afya analipwa zaidi ya million 12 kwa mwezi Ukiweka na marupupu hapo ya vikao? Acha upuuzi maisha Kama ni magumu wote tushee na isiwe kwa wachache fikiri kabla hujavisumbua violet vyako kwenye keypad/keyboard
 
Wazo jema na lina mashiko sana,ila wasiwasi wangu ni hawa watu wa magamba,wasije wakaanza kuwaambiwa madaktari wanagoma kutokana na msukumo wa CDM,maana tumeona haya kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma nk.Lakini pia tumeona kule mbeya,baada ya mbunge wao kamanda sugu kwenda kuwaatuliza machinga,mkuu wa mkoa akaanza maneno mara mgomo huu sio wa machinga,mara sijui ulipangwa nk...lakini tusifungwe na fikra hasi na majitaka za viongozi na wanachama wa CCM,nadhani CDM waende kama wabunge na viongozi wa siasa wanaotaka kujua ukweli wa mambo hili kuyawakilisha mahala husika hasa bungeni na kwenye mamlaka nyingine za nchi...

Bravo CDM..!!!
 
hapa wanataka kuleta siasa tu.badala ya kukutana na madaktari wamfuate pinda ili aende kujibu hoja za madaktari.hakuna kuhusisha wanasiasa!!!
 
attachment.php

Madokta wakiendelea na mkutano wao Star Light Hotel DSM jana
 
Pamoja kamanda,lakini usisahau jamaa anapenda safari kuliko ibada ndio maana hana muda wa mambo ya msingi.Wao si wanatibiwa nje bana!!!so doctors wakigoma kazi kwetu wapiga kura.Wenzake wametuma mawaziri kwenye huo mkutano wa uchumi yeye kama kawa.
 
Back
Top Bottom