Zijue namba za magari ya Tanzania! Pamoja na namba maalum za magari ya viongozi, Serikali na Taasisi za Umma kwa ujumla

Chifunanga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
290
98
Wadau, mi kila siku minekuwa nikijiuliza, ila sijapata jibu. Naomba wenye ufahamu wanielimishe kwenye hili.

Hivi hizi herufi kwenye "licence plates" za magari zinamaana gani?

STK
STJ
STH
ST A
ST
DFP
SU - (hii nimesikia ni Shirika la Umma, ila sijui kama ni kweli)
TP - (magari ya polisi yana herufi hizi, ila sijui zinamaanisha nini)
E - (hii naona kwenye msafara wa rais, so nahisi E inasimama kwa neno Escort)
CD - (hii nadhani maana yake inatokana na neno la kifaransa Cors Diplomatique, na inakuwa kwenye yale magari ya maembasy)

Naomba kuwasilisha



------
Ukiona mtaani gari zimeandikwa ktk plate number kama ifuatavyo usiumize kichwa jua ni hivi:

1. Namba za Magari Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu
Namba za magari yanayitumika kumbeba Rais au Makamu wa Rais na Waziri Mkuu haziandikwi namba wale herufi katika kibao chake, bali huwa na nembo ya taifa ya Bwana na Bibi. Kwa Kiingereza magari haya hufahamika kama State Cars,

ikulu.jpg

2. Spika wa Bunge la Tanzania na Naibu wake
Spika wa Bunge pia gari lake huwa halina namba kwenye kibao chake bali huwa na herufi S pekee. Gari la Naibu Spika nalo huwa na herufi NS pekee. Maana ya herufi S ni Spika na NS ni Naibu Spika

Naibu spika.JPG

3. Katibu Mkuu Kiongozi
Katibu Mkuu Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatumia gari ambalo lina kibandiko chenye herufi CS pekee. Ikiwa maana ya CS ni Chief secretary

Katibu Mkuu Kiongozi.jpg

4. Jaji Mkuu wa Tanzania
Gari la Jaji Mkuu wa Tanzania huwa na herufi JM kwenye kibao chake

Jaji Mkuu.JPG

5. Mkuu wa Majeshi (CDF)
Gari la Mkuu wa Majeshi wa Tanzania katika kibao chake huwa hakuna namba wala herufi zozote bali kunakuwepo na Nyota nne kwenye kibao cha gari lake

CDF.jpg

6. Waziri na Naibu Waziri wa Wizara mbalimbali
Magari ya Waziri na Manaibu wao huwa na herufi zinazoonyesha cheo (kama ni waziri au Naibu waziri) halafu hufuatia ana vifupisho vya majina ya Wizara zao. Gari la Waziri huwa na herufi W ikifuatia na kifupisho cha jina la Wizara yake. Gari la Naibu waziri huwa na herufi NW ikifuatiwa na kifupisho cha jina la Wizara yake

waziri.JPG
naibu waziri.JPG

7. Gari za Serikali za Mitaa
Magari ya Serikali za Mitaa, yanayotumiwa kwenye Serikali hizo. Magari hayo kuwa na kibao chenye Herufi SM zikifuatiwa na namba tofauti tofauti.

Serikali mtaa.jpg

8. Magari ya Shirika la Umoja wa Mataifa
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na moja ya shirika la umoja wa mataifa. Mfano shirika la Afya Duniani (WHO). Kibao chenye namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na herufi CD kisha namba tena.

Umoja mataifa.JPG

9. Magari ya balozini Mbalimbali nchi Tanzania
Magari ya Ubalozi nchini Tanzania huanziwa na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD kisha namba. Pia namba hizi hutumiwa na wafanyakazi wa ubalozi husika hata kama ni watanzania. Mfano wa Ubalozi ni Marekani

Balozi.jpg

10. Shirika la Umma. Mfano; TANESCO, EWURA
Magari yanayotumiwa na mashirika ya Umma huwa na kibao (Plate Number) ambazo huanziwa na herufi SU na kufuatiwa na namba tofauti tofauti kwenye vibao hivyo

Shirika umma.JPG

11. Magari kwa ajili ya matumizi ya Miradi inayofadhiliwa na watu to nje ya nchi
Magari yanayotumika kwenye miradi inayofadhiliwa kutoka nje ya nchi kuwa na kibao chenye herufi DFP (Donor's Fund Project) ikifuatiwa na namba tofauti tofauti. Pia tofauti na DFP utakuta mengine yana DFPA

miradi1.jpg
miradi2.jpg

12. Magari ya Police wa Tanzania
Magari ya Polisi nchini Tanzania huwa na kibao chenye kuanziwa na herufi PT (Polisi of Tanzania) halafu hufuatiwa na namba tofauti tofauti mbele yake

Pt.JPG

13. Magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania
Magari ya Jeshi la Tanzania huwa na kibao chenye kuanziwa na namba kadhaa kisha hufuatiwa na herufi JW kisha hufuatiwa na namba tena.

jeshi.JPG

14. Magereza Tanzania
Magari ya Magereza ya Tanzania huwa na kibao chenye kuanziwa na herufi MT kisha hufuatiwa na namba kadhaa mbele yake kwenye kibao cha magari hayo

magereza.jpg

15. Serikali ya Tanzania
Serikali ya Tanzania ina gari zake tofauti tofauti ambzo hutumika kwa mfano Wilayani au hata kwenye halmashauri. Magari haya huwa na kibandiko chenye Herufi za mwanzo STK au STJ au STL na baada ya hapo hufuatiwa na namba kadhaa mbele

stj.JPG
stk.JPG
stl.jpg

16. Magari ya Wakuu wa Mikoa
Wakuu wa mikoa wote nchi huwa na magari ambayo huwana plate number ka tofauti. Gari la mkuu wa mkoa huwa na kibandiko ambacho kuanza na herufi RC na kisha hufuatiwa na herufi ambazo ni kifupi cha mkoa wake. Herufi RC humaanisha Regional Commisioner. Mfano; RC NJB- Mkuu wa Mkoa Njombe

3581ab2af279f4e88b6e5835db373d21.jpg

17. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Serikali ya mapinduzi Zanzibar hutumia magari yenye kibao chenye kuanziwa na herufi SMZ kisha kufuatwa na tarakimu kadhaa. Magari haya hutumika kwenye shuguli za kiserikali hivyo hupewa viongozi wa serikali katika ngazi fulani

smz.jpg

18. JR- Jaji wa Mahakama ya Rufaa

19. JK- Jaji Kiongozi

20. J- Jaji wa Mahakama Kuu

21. CGP-Commissioner General of Prison(Mkuu wa Magereza)

22. CAG - Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali

23. Magari ya watu binafsi
Magari ya watu binafsi nchini Tanzania huwa na kibao chenye kuanza na herufi T kisha tarakimu tatu hufuata na baada ya hapo herufi tatu hufuata. Magari haya ya binafsi yanaweza kuwa ya biashara au la.

Pia kwenye magari ya binafsi ambayo sio ya biashara kunauwezekano kuwa na kibandiko ambacho kina jina mtu binafsi.

7832710ceee8ae678ff885687f150ebb.jpg
56948b739030cda3dfeaca98c548adc1.jpg
382a1430b3f1c04d345a7f8fd38b7832.jpg

NYONGEZA:
Magari yote haya huwa pia na tofauti katika rangi za plate number hizo, rangi hizo zinaingiliana sehemu na sehemu;

1. Magari yenye plate number za Rangi ya Njano
  • Namba za Magari Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu
  • Spika wa Bunge la Tanzania na Naibu wake
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Jaji Mkuu wa Tanzania
  • Waziri na Naibu Waziri wa Wizara mbalimbali
  • Gari za Serikali za Mitaa
  • Shirika la Umma. Mfano; TANESCO, EWURA
  • Serikali ya Tanzania
  • Magari ya Wakuu wa Mikoa
2. Magari yenye plate number za rangi ya Kijani
  • Magari ya balozini Mbalimbali nchi Tanzania
  • Magereza Tanzania
3. Magari yenye plate number za rangi nyeusi
  • Magari ya Police wa Tanzania (Maandishi ya rangi ya njano)
  • Magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania (Maandishi ya rangi nyeupe)
4. Magari yenye plate number za rangi nyekundu
  • Mkuu wa Majeshi (CDF) (Nyota zilizopo huwa na rangi ya dhahabu)
  • Magari kwa ajili ya matumizi ya Miradi inayofadhiliwa na watu toka nje ya nchi
5. Magari yenye plate number za rangi nyeupe
  • Magari kwa ajili ya biashara (Commercial Use)
  • Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
6. Magari yenye plate number za rangi ya bluu
  • Magari ya Shirika la Umoja wa Mataifa
 
Wadau, mi kila siku minekuwa nikijiuliza, ila sijapata jibu. Naomba wenye ufahamu wanielimishe kwenye hili.

Hivi hizi herufi kwenye "licence plates" za magari zinamaana gani?

STK
STJ
STH
ST A
ST
DFP
SU - (hii nimesikia ni Shirika la Umma, ila sijui kama ni kweli)
TP - (magari ya polisi yana herufi hizi, ila sijui zinamaanisha nini)
E - (hii naona kwenye msafara wa rais, so nahisi E inasimama kwa neno Escort)
CD - (hii nadhani maana yake inatokana na neno la kifaransa Cors Diplomatique, na inakuwa kwenye yale magari ya maembasy)

Naomba kuwasilisha

Hizo ST ni namba zinazowakilisha Serikali Tanzania kwa hiyo J K, just ni series, zilianza na ST, zikaja STA, STB....,STH ilvyoisha ilipaswa kuja STI lakini mara nyingi I na O huwa Zinarukwa kwa sababu ya kufanana na moja na sufuri, kama huo utaratibu hautabadilika basi hizo namba zitaenda mpaka STZ

TP Ni Tanzania Police
 
Lakini mbona naona STJ nyingi zinatumika na polisi, na STK zinatumika na wengine (especially wizara)?

Pia Sijawahi kuona wala kusikia STB wala STC. Ila ST zipo....na STA sio STA, mara nyingi huwa ST halafu namba, halafu mishwo ndio A.

Naweza kuelewa kuwa ST = Serikali Tanzania ila hizo herufi bado. Naomba mawazo zaidi, kwa wanaofahamu zaidi.
 
ST # A ni magari ya Ikulu
PT ni Police Tanzania na si TP kama ulivyoainisha
DFP ni Donor Funded Project hii ni badala ya TX
SU ni Shirika la Umma
STA,...STG,STH,STK, STJ,...,STZ ni magari ya Idara nyingine za serikali pamoja na wizara
WN (abc) ni waziri wa nchi
W (abc) ni waziri
S ni Spika
NS ni Naibu Spika
JM ni Jaji mkuu
CAG ni Chief Auditor General
 
Unajua utaratibu wa serikali uko tofauti kidogo na utaratibu wa kikawaida, kweli unaweza kuchanganyikiwa kwa hilo lakini kuna sababu kadhaa
1) Katika series ya hizo namba say ST sio kama hizo namba zote zilitumika, lazima kunakuwa na namba wanaziruka kwa sababu zao wanazojijua (Kusalama), kwa hiyo unaweza kuta wapo STJ , lakini unaweza kukutana na Gari mpya kabisa ina namba just ST

Police kabla ya kuanza kutumia namba zao mpya (PT) walikuwa wanatumia ST, kwa hiyo walishawahi kuwa na STG, STH na sasa yapo machache ya STJ mengi yakiwa ni PT

Hizo unazozungumzia (STB, STC, STD, STE, STF na STG) zilishatumika zamani na zimeshajaa,

STA zilishatumika na zimeisha, lakini kwa sababu zao serikali wameamua kutumia tena ST lakini katika mfumo mwingine, hivyo wantumia STxxxA, and the STxxxB.............STxxxZ
 
wakuu asanteni sana...sasa nimeelewa. oh, one more thing....ST = Serikali Tanzania au ST = STate (state)?
 
ST # A ni magari ya Ikulu
PT ni Police Tanzania na si TP kama ulivyoainisha
DFP ni Donor Funded Project hii ni badala ya TX
SU ni Shirika la Umma
STA,...STG,STH,STK, STJ,...,STZ ni magari ya Idara nyingine za serikali pamoja na wizara
WN (abc) ni waziri wa nchi
W (abc) ni waziri
S ni Spika
NS ni Naibu Spika
JM ni Jaji mkuu
CAG ni Chief Auditor General

Asante sana kwa shule na ufafanuzi mzuri. Ni jana tu nimeona namba nyingine inayosomeka hivi SSM je waweza kujua ina maanisha nini. Mwanzo nilihisi siyo namba ya Tanzania ikabidi nijongee karibu kabisa na hiyo pickup nikaona bendera ya TZ ikiwa imeongezwa kwenye ile plate kuashiria kuwa niya Tanzania.

Msaada kwa hii pia.
 
Sina uhakika kuhusu SSM, ila mi nimeona SM ambayo maana yake ni Serikali za Mitaa (nadhani)

Shukrani hizo walao nafahamu kuwa niza serikali za mitaa na ndiyo magari mengi tuyaonayo hasa wilayani. Hii nimeona nikashangaa nakumbuka ilisomeka SSM ni pick up na sijaona namba nyingine ya kufanana nayo.
 
STK,STJ,STH,STG.......ni namba za magari ya ofisi na idara za serikali kuu(central government). ST stands for Serikali ya TZ na herufi zinafuata ni za kawaida tu.

DFP ni namba za magari yaliyo katika miradi inayofadhiliwa na wafadhili toka nje yaani Donor Funded Project.

SU ni kweli ni namba za magari ya mashirika ya umma kama TANESCO,TTCL,vyuo vikuu vya umma n.k.

ST na ST A ni namba za magari ya ikulu na magari ya makamu wa rais. Yaani ST stands for Serikali ya TZ.

SM ni namba ya magari ya ofisi za serikali za mitaa (local governments),kama halmashauri za majiji,miji,manispaa,wilaya n.k.

E ni kweli ni namba za magari ya ikulu yanayokuaga katika misafara ya viongozi kama rais,makamu wake na waziri mkuu. Bila kusahau rais na makamu wake wa Zanzibar.

SMZ ni namba za magari ya afisi zilizo chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

NS ni namba ya gari la Naibu Spika wa bunge la JMT.

S ni namba ya gari la Spika wa bunge la JMT.

J ni namba ya gari la jaji wa mahakama kuu au mahakama ya rufaa za JMT.

Etc.
 
Lakini mbona naona STJ nyingi zinatumika na polisi, na STK zinatumika na wengine (especially wizara)?

Pia Sijawahi kuona wala kusikia STB wala STC. Ila ST zipo....na STA sio STA, mara nyingi huwa ST halafu namba, halafu mishwo ndio A.

Naweza kuelewa kuwa ST = Serikali Tanzania ila hizo herufi bado. Naomba mawazo zaidi, kwa wanaofahamu zaidi.

uzionee wapi ndugu? umri mkuu. ni kabla ya .com ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom