Kite Munganga
Platinum Member
- Nov 19, 2006
- 1,773
- 952
Mungai aja juu
2008-11-24 16:48:04
Na Emmanuel Lengwa, Jijini
Mbunge wa CCM wa jimbo la Mufindi Kaskazini, Mheshimiwa Joseph James Mungai, ambaye Ijumaa wiki iliyopita alilipukiwa na mkazi mmoja wa Jijini, akimtuhumu kwamba ni fisadi, ameeleza kusikitishwa kwake na kauli hiyo, na akasema madai hayo siyo ya kweli.
Tuhuma hizo zilielekezwa kwake na Bw. Renatus Mkinga wakati akichangia mada kwenye kipindi cha Kipimajoto, kinachorushwa `live` na kituo cha luninga cha ITV.
Katika madai yake, Bw. Mkinga alidai kuwa Mhe. Mungai akiwa Wizara ya Elimu na Utamaduni, ulitokea wizi wa fedha zaidi ya shilingi bilioni tatu , mali ya wizara hiyo.
Akadai kuwa punde tu wizi huo ulipotokea, mfanyakazi mmoja wa Wizara hiyo ambaye Bw. Mkinga hakumtaja jina, aligundua na kutoa taarifa ili hatua zaidi zichukuliwe.
Bw. Mkinga alizidi kudai kuwa badala ya Waziri Mungai kufuatilia taarifa hizo, alikanusha kuwa hakuna wizi uliotokea na kuchukua hatua ya kumtimua kazi mfanyakazi huyo aliyebaini upotevu wa fedha.
Hata hivyo Mhe. Mungai leo amenusha madai hayo.
``Kamwe sijawahi kutuhumiwa kwa jambo lolote hilo lililosemwa silijui wala halijawahi kunitokea,`` amesema Mheshimiwa Mungai.
Amesema wakati akiwa Waziri wa Elimu na Utamaduni, aliiongoza wizara hiyo kwa uadilifu na uzalendo mkubwa kwa maslahi ya taifa na hakuwahi kufanya hujuma ya aina yeyote.
Kipindi hicho ya Kipimajoto kinachorushwa na ITV kila Ijumaa, wiki iliyopita kilikuwa kikijadili mada ya ``Nini kifanyike kupata suluhu ya migomo ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu