Kuhusu Joseph Mungai

Sikuwa mkubwa nyakati hizo nilikuwa na miaka 7 tu.
Nilimwona wakati akipiga Kampeni za Ubunge kwa mara ya kwanza huku kauramba shati la Haki ya Mungu( Lile lisilo na kola)

Hivyo ndivyo nilivyokuwa utotoni.
Sasa nikiweka picha ya mwaka huu utatoa comments gani!

Shati la HAKI YA MUNGU siyo? Unakuwa kama unaapa na kupeleka kidole shingoni ehhh?? Umenivunja mbavu.

Juu ya picha umenikumusha wimbo wa twanga pepeta sijui? Jamaa anasema "mnasema nimekunywa bia, na mimi sijanywa bia, nikinywa je, itakuwaje...?" Yaani kama hiyo ni ya utoto, ya ukubwani je? :) Wengine hubadilika ukwani.
 
Naona tuna watu wanaokuwa watawala Tanzania na huku wana ukazi Marekani, au familia zao zinakaa Marekani! Hicho kinanishangaza!

Inaelekea Balali alikuwa Gavana wa BoT na huku ni mkazi wa Marekani! Gray Mgonja naye inaonekana kama alikuwa mkuu sana wa shughuli zote za fedha lakini familia yake inakaa Marekani. Sasa si inakokaa familia yako ndiko iliko roho yako?

Na Mungai naye ni mzalendo wa Marekani aua anapapenda tu? Hizo fedha za kwenda huko mara kwa mara alizipata kutokana na jasho la wananchi wanaotembea kutoka Kimara hadi Kariakoo kwa kukosa nauli, au ni za urithi?

Ni heri kuwa na expatriate ministers kuliko kuwa na hawa ambao mioyo yao haiko Tanzania.

Mungai seemed to have been a good Minister of Education. I have no problems with mundane matters such as his combining Physics with Chemistry. It so happens that a lot of Chemistry is Physics, and vice versa. Indeed Cambridge University offers Combined Science as a major subject in its international high school curriculum. It was OK, but not essential, to combine the two subjects.

I am saddened by the fact that a man who seemed hard working and principled has turned out to be just another promiscuous politician, and of dubious integrity.
 
Mkuu Kiungani,

- Heshima mbele kama kawaida, hii habari ni ina 100% truth, ingawa sina uhakika na Mungai kuwemo kwenye list ya Kisutu, inawezekana kabisa kua he knows something we do not kuhusu kuhusika kwake na ishus za kupelekwa Kisutu,

- Sasa ni vyema kua hapa JF tumeiweka wazi kuwa mkuu anajaribu kukimbia maana yasije yakawa kama ya Balali tena, halafu tukaanza kutafutana uchawi, mkuu huyu anakimbia tunamuona.

Mkuu Kiungani, saaafi sana tuendelee kumfuatilia huyu Mungai, na kuweka hapa habari zake, hapo tupo pamoja mkuu.
 
Salaam nyingi waku!

Nadhani tunaelekea kuzuri with the whole nation atleast aware of some greedy animals killing the future of the nation silently. Its unfortunate kuwa baadhi ya mafisadi ni baba zetu,wajomba< baba wadogo, sugar daddies(vibuzi) and we stand to benefit in some way. The worst part of the drama is when the longtime victims now change into whistle blowers,prosecutors,judges and analysts< then tunambiwa,

mjadala wa epa sasa basi !

Msitumie kagoda kisiasa

its time to mind your own business

ndiyo maana watanzania hatuendelii, kzi kuzungumzia maisha binafsi ya watu .

Guys correct me if am wrong. Hawa jamaa 2010, who will they want to vote for them ?

Waliotumia kagoda kuiba fedha , si walitumia marafiki zao wenye influence ya kisiasa? Wahusika wengine si tumekuja kuwafahamu kama wanasiasa? So kwa nini tusitumie kagoda kama political weapon?

We can only mid our business, if it was properly handled, it was okay to come and ask for votes from us, misuse public office incompetently, now all the ill-acquired wealth becomes a private matter of the mjomba.

" tooooo late!!!!"

we will leave no stone unturned. Alut continua
 
WaTanzania huwa hatutaki kutenganisha watoto/mtoto kutoka kwa baba/mama yake! And we Tanzanian suffer a lot from that view. Children grow up and lead separate lives, and I think that's how it should be. You grow up, you move on with your life, don't we all?

In this case, if one is living in Tanzania and his/her grown-ass children happen to be making a living in USA or anywhere in the diaspora, what then is the problem? I have known a lot of cases where a child of a politician, famed businessman/woman etc in Tanzania where he/she will be told "...si umwambie mzee atengeneze fresh mambo?" or something of that nature - the sad part being this child is a 40 years old!

Associating anyone's money with the public sweat when we don't know shit how that money was made I think is utter stupidity! Find out where and how one made his/her money first and foremost. Has one been accused of wrongdoings, ufisadi, uwizi, uhujumu uchumi etc? With concrete proof? Is joining chemistry and physics, for example, a proof that he is a fisadi, mwizi etc? Just wondering aloud......

Hivi huyu mtu akirudi tutaandika nini hapa........?????
 
Kuku wa kienyeji hawachagui chakula. Kwa dada zetu wanaangalia sura?. Wewe unauliza, mbona Mungai ni handsome boy. Mheshimiwa Wasira alikuja hapa India mwezi uliopita. Akiwatembelea wabongo eneo fulani, dada mmoja wa kibongo akacomment "jamani huyu baba ni ugly akikutokea ni lazima utakimbia". Mwingine akamjibu "kalagabaho wenzio kule bongo wanamgombanio!".

Hahahaaaaaaaaaaaahahahahaaaaaaaaaaaa!!!!! Pig
 
hivi bao tulilopigwa wakati wa alliance air, mungai nae alikuwa kwenye board na kwenye umiliki, namkumbuka na bw gideon Kaunda?
 
hivi bao tulilopigwa wakati wa alliance air, mungai nae alikuwa kwenye board na kwenye umiliki, namkumbuka na bw gideon Kaunda?

Ni sahihi kabisa, hao wawili walikuwa "ndio wenyewe" wa hilo Shirika la mseto wa Afrika ya Kusini, Uganda na Tanzania ambalo ndilo "lilikumbatiwa kifisadi" na Serikali na kuilazimisha ATC chini ya Ole Kambainei KUSITISHA SAFARI ZA KIMATAIFA (IOPS) kwa manufaa yao na makaburu. Iwapo kweli tunataka kuifanyia postmortem ATC/ATCL ni budi tuanzie hapo.

Jamani, hivi kwa nini Nyang'anyi na Mattaka hawakuachishwa kazi baada ya kuvuruga safari za Mahujaji mwaka wa jana na kuisababishia Serikali kupoteza mabilioni ya shilingi ili kuwakwamua hao Mahujaji? ATCL kamwe haitafanikiwa iwapo Uongozi uliopo sasa hautafukuzwa kazi, yaani Mwenyekiti, Bodi yake, MD, Wakurugenzi wote na hao akina Mark Manji. Kisha iwachague viongozi wenye utaalamu na uzoefu uanaotakiwa, na wawe waadilifu ambao nao waje na Menejimenti mpya yenye kujua watendalo na waendako ndipo Serikali ifanye cash injection ya maana (inayotosheleza kulipa hayo madeni, kuendeleza Shirika na hatimaye kumpata "financially sound partner who is very conversant with the Aviation/Airline industry". Sio utajiri tu ndio unaweza kuendesha airline - ona mashirika makubwa yanavyofilisika, sembuse 3rd world operators!

KAZI KWAKO JK, TUSAFISHIE ATCL NA ULIFUFUE LIPAE IPASAVYO.
________________________________________________

KIATU CHANGU KIPANA LAKINI KINANIBANA!
 
Huyu ni fisadi group ya wakina Mramba na Yona alikula rushwa hata kwenye kuuza shamba la Kapunga; Alilonunua Mahesh Patel wa Export Trading!! Inawezekana kakimbia kwani anajua ubunge Mufindi hapati tena pengine akagombee kwao Ukikuyu Kenya!!
 
Ni kweli Mungai alisoma St. Michael's and st. George's pale iringa form 5 lakini alifukuzwa kwahiyo hana High School Certificate!!!Ninavyokumbuka ni kwamba baada ya hapo bwana mmoja mkikuyu mwenzie alimuajiri kuuza vyerehani kwenye kampuni moja ikiitwa Singer.
 
Bulesi...what next after SINGER....?

Huku kumjadili Mungai kama si Mtanzania ni Hoja nyepesi sana...so angekuwa MTZ tungemuachia???...Kimsingi ajadiliwe kwa Ufisadi wake...Wao waliofanya UFISADI bado watz...wanaokula rushwa hadi sasa ni hao wa-tz waliopo ktk "Position"...sasa tuwaache...?Hawa wabunge si ndio wametoa rushwa warudi Bungeni...au...?

Utakuwa mchezo Mtamu pale Watuhumiwa hawa wa UFISADI wakisema na KURA waliiba vipi...?Hapo SINEMA litakuwa tamu....
 
Hii kali ya mwaka. Sasa kilitokea nini baada ya kuunganisha PHYSICS NA CHEMISTRY?.


PHYSICS + CHEMISTRY = SCIENCE (According to Dr. Mungai sorry Uncle!!!!)
 
Just a curiosity

Go to Goooogle and type : Mungai - CIA Agent

It seems there millions allegations that the Name Mungai is linked to CIA!!!

- - - -

Over and Out
 
tunaomba utoe utafiti then uweke habari hapa wazi badala ya kusema tetesi. ukisha sema tetesi maana habari haina uhakkika ila umeweka kupamba thread yako tu, ni bora usiweke hizo tetesi kabisa

Why not? Thread hii inamjadili Mungai kwanini nianzishe thread nyingine ya huyo huyo Mungai, sioni busara kuanzisha thread halafu kumpa kazi mod ya kuunganisha na hii. Ukumbuke tetesi ni tofauti na uvumi, hii habari sio uvumi ina ukweli lakini sikujua details zake kwa undani, ndio maana nikawaachia member wanaojua waeleze zaidi, na wanaojua wameeleza zaidi. Dhambi iko wapi hapa? Au unataka tuanzishe threads kwa style yako??
 
Mungai ni mmoja wa matajiri wenye rasilimali kubwa hapa nchini. Kama ni Marekani labda kuhamishia tuu hiyo nyumba ndogo na yeye kuendelea kwenda kulamba tuu asali ila mzinga amechongea Mufindi Tea Estate na TATEPA. Jamaa anaijua hela, ni jeuri na kiburi cha kina Mkwawa, ni bora afe kuliko kuikimbia nchi.

Pia kwa Mungai ninayemfahamu mimi ni mzee wa Totos dogodogo kuku wa kienyeji, akihamia huko Marekani kuku hao apate wapi?.

Kama fisadi Mungai ni mzee wa Totos dogodogo kuku wa kienyeji, ina maana yeye ni nguruwe mwitu?? ......
 
Ni kweli Mungai alisoma St. Michael's and st. George's pale iringa form 5 lakini alifukuzwa kwahiyo hana High School Certificate!!!Ninavyokumbuka ni kwamba baada ya hapo bwana mmoja mkikuyu mwenzie alimuajiri kuuza vyerehani kwenye kampuni moja ikiitwa Singer.
Kwa hiyo hawa ndo wale baadhi ya vihiyo vigogo wa CCM ambayo wamekuwa wanaenda na upepo na kunadi nchi yetu miaka nenda rudi! Ama kweli "wajinga ndiyo waliwao"
 
I am saddened by the fact that a man who seemed hard working and principled has turned out to be just another promiscuous politician, and of dubious integrity. [/COLOR][/SIZE][/FONT]

Ndugu Moshi,
Sababu hizi ndizo zinazoifanya Tanzania kila leo inarudi nyuma na wala si kwenda mbele.
Sababu hizi ndo zinawafanya watanzania hodari kama ninyi mkimbie nchi na kwenda kuendeleza nchi za watu wengine!
Sababu hizi ndizo miaka nenda rudi, tangia tupate uhuru zimekuwa zinakwamisha nchi yetu kwenda mbele, na pia zimekuwa zina "frustrate" wanamapinduzi wengi kama ninyi na wengi wengi tusomao maoni yao humu kwenye JF kuwa msitake kabisa kujihusisha na siasa za nchi yetu ambazo zimeoza na zinatoa wadudu!
Sababu hizi ndo zimenifanya niache hata kusoma magazeti yetu hususa ya kisiasa, au kufuatilia maamuzi ya serikali yetu. Sababu hizi ndizo ambazo zimesababisha Jambo Forums, pamoja na Forums nyingi zilizotangulia kabla ya hii kuwa maarufu, kwani tunatoa hasira zetu huku tumefichama!
Tangia tupate uhuru tumekuwa tunaletewa sababu nyingi na tofauti ambazo zinafanya tusiendelee, tatizo ni kuwa wengi wazitoazo ni walewale, kutokana na ujinga wa Watanzania tumekuwa tunazikubali, au zikiwa recycled sisi tunaamini kuwa ni sababu mpya! Leo waziri wa elimu anakwambia matokea ya darasa la saba ati mazuri kwani asilimia 70 wameenda sekondari! Je, mwaka 2008 bado unamzuia kijana wa miaka 13 au 14 aisendelee na shule ya sekondari kwa kumwambia ati amefeli?
Viongozi wetu wengi ndiyo wamekuwa makaburu kuliko wale makaburu wa kusini mwa afrika na sisi bado tumekaa kimya tu.
Leo hii jiji la Dar ati bado halina maji ya bomba, na wizara ya maji na nishati ipo na mawaziri wake! Its a JOKE, a BIG JOKE! Tuna wizara ya madini, ila madini yetu hata kusafishwa yanasafishiwa nje ya nchi (eg S.Africa). Tuna wizara ya mawasiliano na uchukuzi shirika letu la ndege ni nyanya!, mabasi ya abiria yanaua mamia ya abiria kila mwaka! Tuna Wizara ya Afya- Kipindupindu kimepiga kambi nchini! Tuna wizara na mawaziri wa mambo ya ndani na sheria, kile leo askari wetu wanakamtwa wakiwa majambazi au wamekodisha silaha zao kwa majambazi!
Samahanini waungwana, hasira ndizo zinazoandika sasa wala siyo mimi na nitaachia hapa! Bungeni ni kama Sinema za vikaragosi- tunaambiwa ati tuna vyama vingi!
 
Back
Top Bottom