Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini na Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM Dr Wilbroad Slaa amesema ameshangazwa na kushtushwa na bajeti ya serikali ya mwaka huu.
Dr Slaa amesema serikali ya CCM imefikia mwisho wa kufikiri kwa kuomba misaada na mikopo kwa wahisani kwa lengo la kukidhi fungu la matumizi ya serikali.Dr Slaa amesema hakungekuwa na tatizo kama mikopo na misaada ingeelekezwa kwenye maendeleo kama ujenzi wa viwanda nk.Dr Slaa alihoji unakopa ili mlipane mishahara na marupurupu?
Dr Slaa alishangazwa pia na serikali kutegemea vinywaji kila mwaka katika kuongeza kodi na kusema huko ni kukosa ubunifu.Mbona hawaangalii madini? Alihoji kiongozi huyo.
Dr Slaa aliponda pia uamuzi wa kuanzisha kodi maalum kwenye plate namba za magari zenye majina ya watu na kusema huko ni kuleta matabaka katika nchi na kuhalalisha mafisadi kutamba na fedha zao haramu.
Source:Tanzania Daima Jumamosi