Kuhuishwa kwa katiba.....

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Habari za jioni wanaJF.
Tunatambua kwamba mpaka sasa hakujawa na kauli iliyo wazi kutoka serikalini inayoonyesha kama watanzania watapatiwa katiba mpya.
Leo hii mh.rais ametoa kauli nyingine kuhusu katiba,kikwete amesema tume ya 'kuhuisha' katiba itaundwa.
Tujaribu kujadili huku "kuhuishwa'' kwa katiba maana yake halisi ni ipi?
Nawasilisha...
 
Kulingana na hotuba ya JK aliyoitoa jana katika kilele cha mahadhimisho ya miaka 34 ya CCM, serikali inao mpango wa kuhuisha katiba tuliyo nayo na wala siyo kuandika katiba mpya. Inavyoelekea hata ile hoja binafsi ya mh.Mwanyika aliyotaka kuiwasilisha bungeni tayari imekwisha tekwa na serikali na kuchakachuliwa ili kuiwezesha serikali kuendelea kushika usukani katika zoezi hilo.
 
Mkwere haangalii tv na kusoma yanayotokea Misri na kwingineko, wala hatembelei humu. He is ***** tusubiri tuone anayotaka kufanya kuhusu katiba. Eti ana hasira upinzani wa Dowans which is his fake deal
 
Back
Top Bottom