Kuhitimisha Siku ya Kifua Kifuu Duniani.

Mar 30, 2016
17
7

UJUMBE MFUPI WA TAARIFA KUMALIZA TB.

Tanzania imekua ikirekodi takribani wagonjwa 63000 kila mwaka wa Kifua kikuu (TB) kwa miaka mitano ikifanya nchi yetu kua ya sita kati ya nchi zinazoongoza kwa ugonjwa wa TB barani Afrika hii ni kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Ikisababishwa na bakteria aitwae Mycobacterium anaesambazwa kwa njia ya hewa kifua kikuu ni moja kati ya magonjwa yenye athari kubwa yasambazwayo kwa njia ya hewa. Wakati mara nyingi ikiathiri mapafu, Kifua kikuu huweza kuathiri sehemu zingine za mwili pia. Dalili za Kifua Kikuu ni kama Kifua kisichoisha, makohozi yenye damu, kutokwa na jasho kwa wingi wakati wa usiku, homa pamoja na kupungukiwa na uzito.

Takwimu zinaonyesha mgonjwa mmoja wa Kifua kikuu nchini Tanzania huweza kuambukiza watu 10 hadi 15 kwa mwaka. Kwa mujibu wa Wataalamu hii ina maana wagonjwa ambao hawamalizi dozi au kupona kabisa wataleta ongezeko la wagonjwa wa Kifua Kikuu hapo baadae. “Kama watapata dawa ama dozi nusu nusu au wakikatisha matibabu katikati, hii itasababisha bakteria wa Kifua Kikuu kua sugu kwa dawa na hata kusababisha kifo” alisema Dk. Raj P Singh, ambae ana uzoefu mkubwa wa kutibu maradhi ya njia ya hewa na wagonjwa wa Kifua Kikuu katika Hospitali za Apollo kwa Zaidi ya miongo miwili sasa.

Kwa miaka mingi, watafiti wa Kifua Kikuu nchini Tanzania wametoa tahadhari kua wagonjwa wanaoshindwa kumaliza dozi ndio wanaoongeza mzigo wa wagonjwa wa Kifua Kikuu waliosugu kwa matibabu nchini na ongezeko la maambukizi ya gonjwa hilo katika Jamii.

Shirika la Afya Duniani, WHO inafanya bidii kupunguza idadi ya wagonjwa ambao hawajatibiwa ikiwemo wale ambao hawamalizi dozi zao, ikiwa sehemu ya hatua hii Hospitali za Apollo zimefanya juhudi katika kutoa taarifa za Kifua Kikuu, kufwata matibabu na kupata matokeo bora Zaidi. Hospitali za Apollo Hyderbad pamoja na shirika la kimataifa la vita dhidi ya kifua kikuu na magonjwa ya mapafu lijulikanalo kwa jina la The Union (International Union against Tuberculosis and Lung Disease) wameanzisha programu ya kudhibiti Kifua Kikuu ambayo itatuma ujumbe kuwakumbusha wagonjwa kuhusu umezaji wa dawa na pia itawataarifu mamlaka husika juu ya taarifa za wagonjwa.

Akiongelea uzinduzi wa programu hiyo Ms. Sangita Reddy, Meneja Mkurugenzi Hospitali za Apollo alisema wagonjwa watapata ujumbe kuwakumbusha, ujumbe wa sauti na wa maneno hata ushauri ili wasisahau kumeza dawa walizopewa za Kifua Kikuu. Program maalumu imeundwa ambayo itapeleka taarifa zote za mgonjwa kwenye tovuti iliyoandaliwa maalumu kwa ajili ya wagonjwa wa Kifua Kikuu. Vilevile program hiyo itasimamia kufwata kwa matibabu sahihi kwa wagonjwa.

Program hiyo, itakuwa ikiwakumbusha wagonjwa kupitia ujumbe wa maneno kumeza dawa, pia hufuatilia maendeleo ya mgonjwa. Kwa mujibu wa Dr. Sarabjit Chadha Mkurugenzi wa huo, nusu ya wagonjwa wa Kifua Kikuu wanatibiwa katika sekta binafsi ya afya, mara nyingi hamna namna ya ufwatiliaji kwa wagonjwa. Programu hii huchukua taarifa muhimu ya mgonjwa, humpa taarifa mgonjwa juu ya ugonjwa huo. Hutuma ujumbe wa maneno kumkubusha kuhusu dawa na kupima afya pamoja na kufuatilia kupitia kupitia kifaa maalumu kijulikanacho kama IVR kila baada ya siku tatu na washauri wa Hospitali za Apollo huwasiliana nae kupitia simu ya mkononi kama inabidi ambao hawafuati matibabu na kuwashauri waendelee na matibabu.

Dr. Chadha anatoa wito kwa sekta za Afya nchini Tanzania kufuata muundo huu kwani hwkuweka karibu na mgonjwa na husaidia mgonjwa kupata matibabu hivyo kusababisha wagonjwa wote wa Kifuu Kikuu kupona kabisa.

Mfumo huu hauna budi kuanzishwa Tanzania pia, kutokana kasi ya teknolojia nchini inavyoongezeka ni muda sekta ya Afya ikafanya mapinduzi ya haraka. Hii ni ya kuchukuliwa kwa uzito na Mamlaka ya Mawasiliano kuungana na sekta ya afya kuwasaidia wagonjwa nchini Tanzania kupiga vita ugonjwa huu, kuungana kumaliza Kifua Kikuu TB.

Dr. Sai Praveen Haranath Mshauri na mtaalamu wa upumuaji na mapafu Hospitali za Apollo, Jubilee Hills, Hyderabad, India anatoa tamko kua kifua chochota kinachodumu kwa Zaidi ya wiki mbili kinatakiwa kupimwa. Watu wanaoambukizwa Kifua Kikuu huweza kukaa kwa muda mrefu bila matatizo yeyote ila huweza kuonekana pindi kinga ya mwili inapokua imepungua au mtu anapokua anakunywa dawa ambazo hupunguza kinga mwilini au kuizuia kutofanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa.

Lengo kuu ni kuhakikisha kua watu wanapata taarifa na kueleweshwa kuhusu ugonjwa Kifua Kikuu kua una tiba, ila pia wale wagonjwa wanaopata dawa wanamaliza dawa hizo ili kuhakikisha maambukizi yanapunguzwa. Pia hii itapunguza idadi ya wagonjwa waliokua sugu kwa dawa.
 

Attachments

  • image 1.JPG
    image 1.JPG
    19.5 KB · Views: 58
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom