O-man
JF-Expert Member
- Nov 17, 2011
- 323
- 65
Yupo kijana ameniletea hii changamoto. Mke anadai talaka baada ya ndoa (ya Kiislamu) isiyozidi miaka miwili. Hiyo kwake si hoja kwa sababu mke ameamua hata baada ya vikao vitatu vya usuluhishi. Baba anataka mto wake wa kiume wa miezi 8. Mke anasema asubiri mpaka atimize miaka 18 na katika muda huo awe anapeleka matunzo ya sh. 150,000 kwa mwezi. Hii imekaaje wakuu?