Kuhamia Dodoma: Bajeti kuvurugwa ili kuhamisha maelfu ya watumishi, wadau wasema bunge hakuna fungu

Swala sio negative side hapa tunataka tuelezwe mpango wa kuhamia dom haukuwepo kwenye bajeti na mpango kama huu lazima fungu lake lijadiliwe bungeni hizo pesa nani kajadili na zitatoka wapi hata jambo hili ukiuliza unaambiwa bavicha kama ni hivyo basi bavicha wanaakili na uzalendo kuliko vijana walio kwenye vyama vingine
Kama waona bavicha wana akili basi hii ni hatari, bajeti ambayo wamekuwa wakiiponda, wanataka kujua kuhusu nini sasa hivi kwa kuuliza maswali??
Unataka muelezwe kitu ambacho mlikisusia wenyewe?? Kuna aliyewafukuza bungeni kuijadili bajeti??
 
Kama waona bavicha wana akili basi hii ni hatari, bajeti ambayo wamekuwa wakiiponda, wanataka kujua kuhusu nini sasa hivi kwa kuuliza maswali??
Unataka muelezwe kitu ambacho mlikisusia wenyewe?? Kuna aliyewafukuza bungeni kuijadili bajeti??
Wao wanakosoa ili kuwaonyesha uozo wa serikali ya kisanii inavyofanya kazi.
 
Hii ni awamu ya 5, tunakwenda kwa kauli za short cut "Anaetaka kuendelea na kazi aende Dodoma na kwa gharama zake mwenyewe hakuna pesa ya uhamisho, kwani hata Dar wengi mlikuja kutoka mikoani kwa gharama zenu kuja kutafuta kazi na mkapata.
Heeee! Yelewiiii
 
Ofisi ya PM ilihamishiwa Dodoma wakati wa Sokoine (~miaka 34 iliyopita) lakini PM mwenyewe hakuhama hadi leo! Kiutaratibu, ofisi zote za kibalozi na za mashirika ya kimataifa yenye hadhi ya kibalozi zinapaswa kuwa pale makao makuu ya serikali yalipo. Balozi zenye majengo makubwa na ya kudumu kama Marekani, Kenya, Zambia na nchi za Umoja wa Ulaya (EU) hazina namna itabidi watafute viwanja na kujenga upya Dodoma!
Hii issue inaweza kufa kifo cha Mende.
 
Nani kakwambia yalifutwa??yalipunguzwa ila sio kufutwa (tafuta bajeti usome)..u can't run ofc bila matumizi mengineyo...kakwambia ana hama na ofc nzima??wanakaa dodoma mwezi mzima kwa ajili ya bunge,we unadhani ofc yake yote nayo inakua imehama??
Kumbe hahami na ofisi nzima. Ndio style gani ya kuhama hio ? Kupunguza OC kwa kiasi kilicho punguzwa ni sawa na kufuta tu. Hapa kwetu wakuu wanalia labda kama waziri mkuu anaupendeleo maalum.
 
Baada ya Mh. Rais kutangaza serikali kuhamia Dodoma katika kipindi chake hiki cha miaka mitano, tayari idara na wizara mbalimbali zimetangaza kuhamia Dodoma ndani ya kipindi hiki cha bajeti hii. Moja ya wizara hiyo ni wizara ya kilimo ambayo imetangaza kuhamia Dodoma wiki ijayo.

Pia, ofisi ya waziri mkuu imepanga kuhamia Dodoma mwezi September mwaka huu.

My take:
Hivi Bajeti hii tulipanga hii mihamo ya kuhamia Dodoma? Kama hatukupanga pesa zinatoka wapi?
 
Mi nashindwa kuelewa. Yani usishangae wizara ya afya ikikuambia itahamia Dodoma kesho
Kweli ifike wakati tujiulize hivi hiyo bajeti ambayo imeanza july 1 ina kasma ya kuhamisha wizara na idara kwenda Dodoma?
 
ukihoji hili utaambiwa unapinga jitihada za rais kuleta maendeleo.
Hii nchi watu wamekua vichwa panzi.
 
Back
Top Bottom