Kufungwa kwa Maduka ya Dr.Remi mjini Bukoba kwapelekea bidhaa kupanda bei

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,045
Wanajamvi,

Kwanza habari za mwaka mpya?

Ni kwa takribani mwezi mmoja sasa maduka ya mfanyabiashara maarufu mkoani Kagera-Bukoba (Dr.REMI) yamefungwa na hayatoi huduma.

Mfanyabiashara huyu kwa muda mrefu amekua akiingiza bidhaa za matumizi ya kila siku tokea nchini Uganda na alikua agent wa kampuni ya Mukwano.

Tangu maduka yake yafungwe bei za vitu kama sabuni, chumvi, mafuta n.k vimepanda bei.

Kufungwa kwa maduka yake kunausishwa na skendo ya siasa kati yake na Dr. Kamala ambaye inasemekana ndo alikuwa mmiliki halali kwahiyo baada ya kuhitilafiana mambo ndo yakawa hivyo.

Je,viongozi wa mkoa hasa wabunge mnasaidiaje wananchi waendelee kupata bidhaa hizi kwa bei kama ya mwanzo au kama mikoa mingine.?

Naomba kuwasilisha.
 
aliyeyafunga ni nani na ni wa chama gani? Na huyo dr Remmy ni wa chama gani? Na nivipi siasa inaingia hapo?
 
Wanajamvi,

Kwanza habari za mwaka mpya?

Ni kwa takribani mwezi mmoja sasa maduka ya mfanyabiashara maarufu mkoani Kagera-Bukoba (Dr.REMI) yamefungwa na hayatoi huduma.

Mfanyabiashara huyu kwa muda mrefu amekua akiingiza bidhaa za matumizi ya kila siku tokea nchini Uganda na alikua agent wa kampuni ya Mukwano.

Tangu maduka yake yafungwe bei za vitu kama sabuni, chumvi, mafuta n.k vimepanda bei.

Kufungwa kwa maduka yake kunausishwa na skendo ya siasa kati yake na Dr. Kamala ambaye inasemekana ndo alikuwa mmiliki halali kwahiyo baada ya kuhitilafiana mambo ndo yakawa hivyo.

Je,viongozi wa mkoa hasa wabunge mnasaidiaje wananchi waendelee kupata bidhaa hizi kwa bei kama ya mwanzo au kama mikoa mingine.?

Naomba kuwasilisha.

Hebu toa habari kamili kuwa yeye ndo ana ugomvi na dr kamala au dr kamala na wapinzani wake kisiasa?
 
Zilizo chini yakapeti ni kwamba,wakati Dr.Kamala akiwa mbunge na waziri wa Afrika mashariki alimtumia Dr.Remi kama kivuri kuweza kufanya biashara na Mukwano.Mali zilikua zinapita mpakani bila shida na kuingia BK.Makonteina na maroli kibao.
Baada ya Dr.Kamala kutemwa kwenye Ubunge jimboni Dr.Remi akamugeuka Kamala nakusema hana chake pale.
Siku si siku Kamala akachaguliwa kuwa Balozi ndo skendo ikaanza.Remi kaambiwa kuwa ana madeni kibao ya TRA mpaka maduka yakafungwa mpaka leo hajurika yupo wapi.
 
huyu dr.remmy alikua anatuuzia sana vifaa vya magari kipindi hicho mi kondakta wa bukoba kishanda..alikua anauza vifaa vya magari kwa bei poa sana..duka lake moja liko karibu na TRA bukoba, kama amefungiwa basi hali ni mbaya sana..huyu ni zaidi ya jimmy.
 
Zamani niangalia 'talk show' zilizoonyesha watu walioanza ujasiliamali wa vitu vidogo kv kuuza ubuyu na kisha kuwa mabilionea, nilidhani hata Tanzania wapo. Kumbe wengi ni Dr. Remy Type!
 
Back
Top Bottom