Kufungua tawi la chadema udom

Ahsante sana miradibubu. Mimi ni mwalimu UDOM na ni mfuasi wa Chadema. Ningependa sana kujiunga kwa kuwa na kadi lkn naogopa maana uongozi wa wanajikomba sana kwa JK. Nisijetengwa. Wamekimbilia kumpa Degree na sasa wanajenga JK Square kama Nyerere Square. Tuko pamoja. Je tawi linaanzishwa na wanafunzi au wakufunzi?
Bigup and goodluck!!
Tawi litaanzishwa na wote kwa pamoja wafanyakazi na wanafunzi usihofu hata kidogo
 
Lazima ile kwao walidhani chuo kikiwa Chimwaga basi ni cha CCM. Kama hawataki kuumbuka waachane na wasomi waendelee tu na KILIMO MWISHO watapata japo asilimia 20% ya kura 2015.

Vijana kazeni buti, Tawi hilo liwafundishe vijana waende vijijini wakaelimishe wazazi wao kwamba CCM ni mzoga haufai. Tunataka pia muondoe aibu ya mji wa DODOMA kuwa ngome ya CCM huku kuna jamii ya wasomi wengi kiasi hicho. iweni chachu ya mabadiliko Dodoma. Tunataka manispaa ya Dodoma na jimbo lake 2015 tuwachie wakatawale huko kijijini.

Mzumbe na SUA mpo wapi mbona morogoro nako aibu tupu hakuna hata jimbo moja la upinzani? Tena majimbo mengine yanachukuliwa na wazee hata hawajasoma bwana! Acheni kukaa kimya kama mmekula ubwabwa wa bibi(CCM)i jaribuni kufikiri kama hawa madogo wa UDOM ili muukomboe mji wa Moro!
 
kufungua matawi siyo issue, nyie walokole mkumbuke ccm, cuf vilisha kuwa na matawi mengi mpaka nje ya nchi, sasa nyie mnaanza kujigamba na kita cha udom


mnatikiwa kuleta democrasia ndani ya chama chenu cha mtandao, badala ya kupeana madaraka, ubunge kikabilakabila na udiniudini!!


Kinachochosha hapa jf, chadema wakifanya utumbo wowote imekuwa news, huu ni ulimbukeni na kutokomaa kisiasa kwa chama hiki na wafuasi wake

Tehe tehe teheeeeeee, ama kweli mfa maji haachi kutapatapa, watu wanazungumzia strategies wewe unasema wanajigamba na UDOM, CCM wameshakata tamaa.

Wewe ni miongoni mwa watu ambao ni fake great thinkers, huwezi sema unashangaa wana CHADEMA kucomment kwenye ishu kama hii, J.F inawawakilisha watanzania maana wakati wa kuji register hakuna sehemu unayoulizwa kuwa wewe ni CCM au CHADEMA, ukiona members wengi wa jamiiforums ni chadema basi ujue ndio hali halisi kwamba watanzania wengi wenye akili timamu ni wafuasi wa CHADEMA.

Big up wana UDOM, idadi yenu ni kubwa sana, Taifa linategemea ukombozi kutoka kwenu.
 
Safi sana, inaleta matumaini sana maana wasomi wakiwa mstari wa mbele ni rahisi kuwaelimisha waliolala. CCM ni chama cha wasio jua ukweli wa mambo sasa sijajua kama watawaambia nini wasomi? Surport yetu iko kwenu Wana UDOM.
 
Waaah.hilo ndo tulitaka kusikia maana siku zote ccm udom ingawa wapo kiduchu wanajigamba.Kwa taarifa yenu nyie wenye mawazo eti udom wote ccm polen sana na mtambue udom km chuo kikuu chadema au upinzani ndo wengi ila ccm kama ada yao wanajipendekeza kwa jina la chuo.kama ccm hawaamin hilo wawaombe redet au synnovet waje watafiti waone kuwa udom na ccm kwa90% ni kama mwarabu na kitimoto.na nyie ccm wa udom mkome kuwa mnatoa taarifa zenu kwa jina la chuo,bali sema ccm udom wasema....pia tunawaomba viongozi wa chadema mkoa na taifa wawe karibu nasi ili tuwamwage mafisadi.
 
Salaam kwenu nyote wapenda maendeleo wa dhati hapa Tanzania. Ninayo furaha kubwa kuwataarifu kwamba sisi wanajumuiya ya Chuo Kikuu Cha Dodoma ambao ni wafuasi wa dhati wa CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO- CHADEMA, tumeamua kufungua tawi letu ambalo litaendelea kutuunganisha na kuweka pamoja nguvu zetu ili kuleta mabadiliko ya kweli.

Tawi hili linakusudiwa kuwa hapo maeneo ya mjini ambapo tutapangisha ofisi nzuri na tutawajibika kuilipia pango kwa muda wote. Litafunguliwa mwanzoni mwa mwezi januari 2011.

CHADEMA ina wafuasi wengi sana katika hiki chuo tofauti sana na wengine wanavyodhani.

Ninaomba kutoa uthibitisho wa hili kama ifuatavyo:

1. Wakati wa kampeni uongozi wa Chuo uliamua kutoa mabasi yanayotumiwa na wafanyakazi ili yawapeleke wafanyakazi kuhudhuria mkutano wa Kikwete uliofanyika hapa Dodoma.Tofauti na uongozi wa chuo ulivyotarajia mabasi yale hayakupata watu katika njia zote yalikotumwa.

Kwa mfano, katika eneo la Kisasa wanakoishi walimu mabasi mawili yale makubwa hayakuambulia hata mwalimu mmoja, njia ya Nkuhungu basi la watu 65, lilipata watu wawili tu na njia ya Mipango basi lilipata mtu mmoja tu.

2. Katika chaguzi zote za uongozi hapa chuoni ni kosa kubwa sana kwa mgombea kubainika kwamba yeye ni mwa CCM.

Kwani kitakachompata ni kukosa kura, mifano ni hii hapa kuna kijana anaitwa Tery yule alisoma risala ya kipuuzi siku Kikwete amaetangazwa kuwa mgombea wa CCM.

Risala hiyo ilipewa jina la risala ya wanafunzi wa elimu ya juu, huyu Tery aligombea nafasi ya uraisi wa serikali ya wanafunzi, kamuulizeni kilichompata ni nini, kwani kura hazikutosha.
Mfano wa piili unawahusu Wahadhiri walioenda kugombea kwa tiketi ya CCM, katika majimbo ya Manyoni mashariki na mwingine katika jimbo lililokuwa la Samwel Chitalilo, wote hawa waligombea uongozi wa UDOMASA - CHAMA CHA WANATAALUMA UDOM, walikosa kura si kwa kukosa uwezo bali tu kule kufungamana na CCM.

3. Serikali ya wanafunzi kushikiriwa na vijana machachari wa Chadema.

4. Mijadala mikali katika mabasi na maeneo ya ofisi inayowahusisha wafanyakazi wa chuo yote imekuwa ikiipinga CCM kwa kiwango kikubwa na kuifagilia CHADEMA.

5. Kipindi cha kampeni wafanyakazi wengi na kwa uwazi waliiunga mkono CHADEMA, kutokana na hali hii hakuna mwana CCM aliyekuwa tayari kuitetea ccm hata kwa wale walioenda kugombea kwa tiketi ya CCM hawakuweza kukabiliana na nguvu kubwa ya Chadema.

6.Kauli ya kikwete kuwaasa wana UDOM wasitumiwe na wanasiaasa baada ya kubaini kwamba CHADEMA ina nguvu kubwa sana hapa mpaka imefikia hali ya kuhitaji kufanya mkakati madhubuti wa kudhibiti halii hii kupitia uongozi wa juu wa chuo na kuleta makada wa CCM kuja kunusuru hali.

7. UDOM kuwa ndani ya kata iliyochukuliwa na CHADEMA- kata ya Dodoma Makulu, kuna mchango mkubwa sana wa wana UDOM katika kufanikisha hili.

8. Wafanyakazi wa UDOM kusafiri kwenda mlimani yaani UDSM kumpigia kura mnyika hili ni kundi kubwa sana la vijana waliomaliza chuo hivi karibuni ambao wameajiliwa hapa UDOM, ilikuwa ni uzalendo wa hali ya juu sana kufanikisha hili na pasipo malipo yoyote zaidi ya kupigania haki ya WATANZANIA.

Hivyo basi kutokana na hoja hizo nane tumebaini kabisa ya kwamba Wana CHAADEMA tupo wengi sana na hivyo tunahitaji sehemu yetu itakayotuunganisha na kutupatia nafasi ya kujadiliana mambo yetu, tawi hili litakuwa kiungo muhimu kati ya Walimu, wanafunzi na wafanyakazi wengine waendeshaji.

RAI YETU
Rai yetu kwenu ni juu ya kuhitaji kuungwa mkono katika mchakato huu, si uhitaji wa mali bali hasa mchango wa mawazo na ushauri kwani ni suala nyeti na ambalo halitawafurahisha wengi lakini tumeamua kufanya haya si kwa kushawishiwa na uongozi wa juu au wa mkoa wa CHADEMA.

Pia kwa Wana CHADEMA wenzetu tunaomba tusaidiane klupambana na propaganda mbaya inayojaribu kuaminisha watanzania wote kwamba wafanyakazi na wanafunzi wote wa Udom ni CCM, ninajua wengine mnafanya hivyo kwa hasira baada ya kuzidiwa na nguvu ya propaganda na wengine ni kutokana na kukosa taarifa sahihi.

Tunatambua kwamba CCM wanawagawia kadi wanafunzi hadi mabwenini tena kwa kuwaandika majina pasipo ridhaa yao na kuwaomba wawape picha passport size wawaletee kadi.
Pia wameweka viongozi wao wa matawi katika mabweni, licha ya jitihada hizi wanazozifanya bado upinzani una nguvu kubwa kwani wanafunzi wanaelewa nini ccm inafanya, na wale wachache wanaojiunga na ccm hapa chuoni ni kutokana na mtazamo potofu wa kudhani kwamba mtu hawezi kuajiriwa mpaka uwe na kadi ya CCM.

Mtazamo huu tumepambana nao sana tena kwa kutoa mifano tukionesha watu walioamini hivyo huku mpaka wakati huu hali zao bado ni mbaya sana.

Kimsingi huu ni mtazamo potofu amabao unawatafuna baadhi ya wasomi wetu katika vyuo vingi na hao ndio wanakuja kuwa watu kama Benson Bana kwani hata anavyoongea amejaa kujipendekeza zaidi ili akumbukwe, nadhani mlimuona jana kwenye kipima joto ITV,alivyokuwa anajikanyaga kuonesha namna ambavyo watanzania wana hali nzuri mpaka kufikia uwezo wa kuendesha magari.

Ninaomba msitishwe na matamko yanayotolewa na baadhi ya watu yakihusisha sisi UDOM, mengine ni propaganda za ccm, mengine ni ya kutungwa na vijana wa CCM ambao wanasoma hapa na hata makao makuu CCM wanafahamu kwamba wapo hapa, hivyo basi ni lazima waoneshe kwamba wanafanya kazi kubwa.

CHADEMA itaendelea kustawi hapa Udom hata kama viongozi wa ngazi ya juu wangefanya nini.

Mungu ibariki CHADEMA , Mungu ibariki Tanzania na Viongozi wote wa CHADEMA​


HAKUNA KItU CHA NAMNA HIYO WEWE UTAKUWA MOJA WAPO YA WANAUSALAMA FEKI
UNATENGENEZA STORi
 
kwa hiyo move mlichobakisha ni kuhakikisha mnafuata sheria za Chuo na nchi na kubwa kuliko ni kukomaa class koz hawa jamaa wakiwaspot huwa wanakuwa wasumbufu kdg. hapo tutegemee Viongozi wa ukweli.....hope first class n Upper 2nd will come out of u GUYS.....Mimi personally nawapa HEKO..........Kuleni Tano zangu fasta.....sambazeni elimu kwa wenzenu......
 
Hila kumbukeni sheria za vyuo vikuu msije kujiingiza kwenye matatizo ya kufanya siasa ndani ya chuo. Inaweza kuwaweka pabaya. Someni sheria hizo kwa makini.
 
HAKUNA KItU CHA NAMNA HIYO WEWE UTAKUWA MOJA WAPO YA WANAUSALAMA FEKI
UNATENGENEZA STORi
Achana na haya mawzo mgando kama una mtu hapa UDOM muulizie juu ya haya mambo yote manane niliyoyataja na ukiona kwamba ni feki basi na usubiri hii januari tuone nini kinafanyika. N inakuomba usipaniki tulia kwani wana Udom wenye akili timamu tumeamua kuonesha makucha yetu, Tunasema tupo tayari kwa lolote
 
Maamuzi makubwa vijana, hiyo inatutia moyo kazeni buti nijuavyo mimi wanaharakati wengi ni wakali darasani kwahiyo mtu yeyote asiwatishe. Itapendenza tawi hilo akilifungua tundu lissu. Chadema ina mkakati wa kufungua matawi mengi zaidi kwa fujo. Hongereni saana
 
Ningependa kushiriki na kuwa mmoja wa kufanikisha kufikia malengo ya chama katika kuendeleza na kukuza mustakabali wa chama...
For more information:
CR of B.Sc Mineral processing engineering-FIRST YEAR AT UDOM !!!!!
 
Ningependa kushiriki na kuwa mmoja wa kufanikisha kufikia malengo ya chama katika kuendeleza na kukuza mustakabali wa chama...
For more information:
CR of B.Sc Mineral processing engineering-FIRST YEAR AT UDOM !!!!!
Sawa mkuu tutakupa taarifa na tunaomba uzidi kuwaambia na wenzako katika hiyo skuli yenu wewe utakuwa ni mjumbe katika kufanikisha azima hii
 
Miradi bubu big up sana. Nipo dodoma, tutaftane, labda naweza changia chochote katika hilo.
 
hongereni vijana, wekeni mkazo kupambana na wanafiki wanaojipendekeza kwenye teule za jambazi kikwete
 
Haya ni mapambazuko yenye kutia matumaini, moyo huo wa kimapinduzi mkiuelekeza kwa vijana wanaosoma kwenye shule za yeboyebo pindi mpatapo nafasi, CCM haita himili NGUVU YA UMMA 2015. Ni aibu kwa kijana wa kisasa kukumbatia CCM inayofilisi nchi hii.

Hongereni sana kwa kulitambua hilo mapema na kuweza kuunganisha nguvu zenu pamoja kwa manufaa ya Taifa.
 
Achana na haya mawzo mgando kama una mtu hapa UDOM muulizie juu ya haya mambo yote manane niliyoyataja na ukiona kwamba ni feki basi na usubiri hii januari tuone nini kinafanyika. N inakuomba usipaniki tulia kwani wana Udom wenye akili timamu tumeamua kuonesha makucha yetu, Tunasema tupo tayari kwa lolote

miradibubu usibishane na mpu***vu, huyo tunamjua, anatapatapa maana sikuzao zinahesabika. Nyie hapo UDOM jiwekeeni mikakati ya kimaendeleo ili siku moja umma:peace: ushike madaraka ya nchi yao. siyo sasa hivi Mafisadi:spy: ndo yaliyo shikilia nchi!
 
Wana-JF nadhani propaganda ya CCM kwa kuwasingizi vijana hawa Vyuo Vya Dodoma huenda ikakigharim sana chama hicho tena kwa kipindi kirefu mno katika vyuo vyetu vyote nchini na KUCHUKIWA ZAIDI NA ZAIDI.

Mpaka hapa nimejifunza ya kwamba uongo una gharama kubwa katika jamii yenye uwezo wa kupembua mambo!!

Hongereni, kama hivyo vivyo ndivyo hali halisi!!
 
Itabidi sasa wajenge(ccm na waarabu wao) chuo kingine. Udom imekombolewa

kazeni buti vijana.

Heshima yako Ng'wanangwa. Mkuu unahasira kweli. Hiyo komyuta yako naihurumia! Kwamba wakajenge anaother University! Hii kali...
 
Big up sana kwa hiyo strategy.Tupo wengi hapa Udom tatizo ni kuwa harakati zipo chinichini mno kwa wasio na taarifa kushiriki.Naomba mbuni njia nzuri ya kutupa taarifa wanachama juu ya maendeleo ya chama ikiwamo ushiriki wa vikao.Mfano juzi sikujua hama tuna mkutano uliofanyika maeneo ya makulu kwa kukosa taarifa huku nikiwa mwanachama hai.Kwahiyo miradi bubu kama we ni kiongozi au upo karibu na viongozi tafuteni njia sahihi ya kutupatia taarifa bila kuvunja sheria za chuo.Nipo college of Education,nasubiri kwa hamu uzinduzi wa tawi letu.Pamoja sana
 
Back
Top Bottom