‘Kufuli’ la Kajala lazua gumzo

Nyundo Kavu

Senior Member
Dec 6, 2011
186
85
HIKI ni kituko! Msanii wa muvi, Kajala Masanja amezua gumzo kufuatia kila anapokwenda kuwa na ‘kufuli’ kwenye mkoba ambalo mwenyewe anadai ana matumizi nalo.
Chanzo chetu ambacho ni rafiki wa msanii huyo kilichoomba hifadhi ya jina kilitutonya kuwa, Kajala amekuwa na tabia ya kutembea na nguo hiyo ya ndani na wakati mwingine kuitumia kujifutia jasho.
“Nilishawahi kuishudia ile nguo ya ndani, ina rangi ya maziwa hivi. Siku moja tulikuwa maeneo flani tunapiga stori, mara akaitoa na kujifutia jasho,” alisema mtoa habari huyo.
Akasema mbali na kuitumia kwa matumizi hayo, siku moja alipomtembelea nyumbani kwake alishangaa kuitumia nguo ileile kujifutia uso, hivyo kumfanya amfikirie tofauti.
Katika kuweka mambo sawa mwandishi wetu alimtafuta Kajala na mahojiano yalikuwa hivi:
Ijumaa: Unadaiwa kutembea na kufuli lako kwenye mkoba na watu wanalihusisha na mambo ya kishirikina, wewe unalizungumziaje hilo?
Kajala: Hee! Hayo ni maamuzi yangu bwana, kwani kuna tatizo gani?
Ijumaa: Lakini kwa nini utumie kufuli kujifutia jasho, kwani umeshindwa kununa kitambaa? Huoni kwamba unawafanya watu wakufikirie tofauti?
Kajala: Wanifikie vyovyote, hayo ni maamuzi yangu.
Ijumaa: Unadhani ni busara kuitumia nguo hiyo katika matumizi ambayo siyo sahihi?
Kajala: Ndugu yangu kama huna lingine la kuzungumza na mimi niache niendelee na mambo yangu.

‘Kufuli’ la Kajala lazua gumzo - Global Publishers
 
Waigizaji wa bongo bwana akili zao zimejaa ushirikina tu kuwa ndio njia pekee ya mafanikio na c kitu kingine dah ndo mana maendeleo sifuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom