kufukuza wanafunzi udsm ni suluhisho?

Kidzogolae

Senior Member
Apr 20, 2008
133
2
Hivi, Nani amewaambia Jumanne magimbi na Mukandara kuwa kufukuza wanafunzi ni solution? Hivi, fuju huwa inajibiwa kwa fujo?kama ndo hivyo, mbona tumeone failure nyingi sana kwa US kufikiri ataleta fujo Iraq na AFgh kama solution, lakini hadi leo wamarekani wanazidi tu kuliwa hela kufinance vita na kuuliwa wanajeshi. Kama wanafunzi wamefanya fujo, nini maana ya kufukuza wanafunzi wengi hivyo? is it a solution?kuna manufaa gani kufukuwa wanafunzi ambao walikuwa kwenye udhamini wa selikali, kodi za watz zilikuwa zinawasomesha kwa miaka miwili au mitatu au minne....halafu hawajamaliza, kwahiyo zile hela za mkopo ndo zimefaidisha nini sasa wakati mpewa mkopo anafukuzwa shule?

Kila siku hapa, moja ya vitu ambavyo watz wanaogopa kutoingia East africa community, pamoja na kwamba kuna factors zingine, ni kutokuwa na ulinganifu wa tananch waliosoma na wasiosoma. watz tumesoma wachache kuliko wenzetu. Na hapohapo tunaendelea kufukuza wanafunzi at 300, wote hao wamefukuzwa, na walikuwa wamepewa mkopo/bumu toka kodi za watz wakulima. uo mkopo umezalisha nini sasa?kuna faida gani kufukuza wanafunzi? wale wanafunzi wengine wana watoto, wanafamilia kabisa na mandevu kibwena, unafikiri wanaweza kuandamana au kugoma bila sababu? sasa mbona we are not address the root cause?

Huu uprefesa wa jumanne magimbi na sauti yake ya ajabu, na kiburi cha mukandara na sura yake laini, uko wapi?let them show that they are professors and they can solve a problem bila kufukuza wanafunzi. kwani wao hawana akili? tukifukuza wanafunzi, ambao sisi wenyewe tulikuwa tunawasomesha tumefanya nini?kuna faida gani?si hasara kwetu sisi wenyewe kwasababu ile elimu tuliyokuwa tunawalipia pale chuo haijatufaidisha sisi watz? mbona hawa watu wawili wanashindwa kuelewe?hawa ndo maprofesa wa kusomea madirishani. ni moja ya ufisadi wa taratibu. au tuwapeleke tena shule wakasome. du! hii ni aibu tupu kwa mukandara na jumanne magimbi.
 
Back
Top Bottom