Kufuga kuku nyumbani

Dr wa ukweli

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
900
264
mimi siyo mtaalamu sana wa mifugo, mke wangu anataka kufuga kuku nyumbani, tatizo eneo letu ni dogo kiwanja kina ukubwa wa 30 kwa 20 tumejenga 20 kwa 15 nyumba ya kulala, imebaki sehemu ndogo ya uwani kama 20 kwe 10, je panafaa kwa kufugia kuku wengi kama kuku 500 au 1000 na hakuna madhara (kuishi karibu na kuku) kwa binadamu au kuku wenyewe?? naomba ushauri kabla sijamkatalia au kumkubalia (kuku wa mayai au majogoo ya kienyeji)
 
U will regret unless uwe na maximum ya kuku 10. Nashauri utafute eneo kubwa pembezoni mwa jiji ufuge idadi hiyo ya kuku!
 
  • Thanks
Reactions: LAT
layer cages 1.jpg

Dr. wa Ukweli

kwa utaalamu huu wa kutumia chiken cages unaweza kufuga .... lakini bado utasumbuka na disposal ya mbolea
 
Itakuwa karibu sana na nyumba ya kuishi hivyo kusababisha vumbi jingi, nime-experience kuwa hawa kuku wanatimua sana vumbi hivyo wanahitaji eneo la kutosha na sio karibu sana na makazi ya watu(haswa wanapokuwa kwa idadi kubwa kama uliyoitaja)
 
inashauriwa kuku mmoja awe na eneo si chini ya mita moja.
Kwa hiyo stock yangu, nje ya mabanda lazima iakisi eneo sio pungufu ya mita moja kwa kila kuku
 
mkuu hizi kages zinapatikana wapi? na za kutosha kuku miatano natakiwa niwe na kiasi gani cha fweza??

natanguliza shukrani

ngoja nikuwekee hii info hapa hapa jamvini na kwa faida ya wote
 

Attachments

  • Chicken cages details and price-1.doc
    327 KB · Views: 330
Ufugaji ni kati ya shughuri inayoharibu sana mazingira so kuwa makini unapoamua kufanya biashara hiyo
 
30787[/ATTACH]

Dr. wa Ukweli

kwa utaalamu huu wa kutumia chiken cages unaweza kufuga .... lakini bado utasumbuka na disposal ya mbolea


Disposal ya mbolea si issue sana kama utakuwa na matumizi yake,kwa mfano kuzalisha Bio gas kwa matumizi ya nyumbani ambayo mabaki yake inakuwa mbolea,mind you hizi cages hutumii maranda,so you have to remove fresh manure every day,ambayo yanakuwa na high content of Amonia.here is where bio gas plant comes into picture.......the bio gas plant act as digester to remove toxic gases.......SIMGAS wanaweza kukushauri pia kuhusu waste!
 
Cage kama hii niliiiona kwenye picha inagharimu sh ngapi? na inakaa kuku wangapi?

Je ni ideal kwa kuku wa nyama au mayai?

Je inaweza kuweka kuku wa kienyeji?
 
mi naona kama hizi cages hazimpi kuku uhuru wa kutembea hapa na pale, kuku kama wa kienyeji ndio kabisa wanakua tofauti na mazingira waliyozoea, labda kwa kuku wa nyama ambao hawahitaji movements za hapa na pale
 
ngoja nikuwekee hii info hapa hapa jamvini na kwa faida ya wote

ninawasiwasi na hii dhana ya kizungu, banda la mbao la miguu4x8 linalaza kuku wazima wa kutaga mayai 200.
na apo utakula faida ya sh7,200 kwa siku ukishatoa garama zote manisha 210,000 kwa mwezi. kama unaanza anza na kuku 50-100-200-300, kuanzia mia300 kwenda juu mpaka uwe mzoefu otherwise utalia.
Muhimu ni usafi wa kila siku na kutoa mbolea/mavi ambao yananuka sana,
 
Dah, nahitaji kujifunza kitu hapa. Kwa wafugaji wanaofugia kuku wa kisasa majumbani. Mbolea zake na yale maranda yakitolewa huwa wanatupa wapi?
 
Kama una tatizo la eneo la kutupa uchafu/mbolea ya kuku,ng'ombe au nguruwe kwa wafugaji wa DSM tafadhali tuwasiliane.
 
  • Thanks
Reactions: SMU

Similar Discussions

Back
Top Bottom