Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,923
Inaelekea kuwa ccm inafanya juu chini kukwamisha ujumbe wa kumkomboa Mtanzania kufika vijijini. Natumaini kuwa sote ambao tu wazalendo na tunaelewa ni kitu gani kinachoondelea, tuna ndugu, marafiki na jamaa zetu huko vijijini.
Tuna bahati kubwa kwamba tunaishi katika wakati ambapo teknolojia imepiga hatua kubwa, tofauti na miaka ya zamani. Teknolojia ambayo imesambaa sasa nchi nzima ni ile ya simu za mikononi na uwezo wa kutuma sms.
Kwa mantiki hiyo basi, ninatoa ushauri kwa wazalendo wote wanaochukia ufisadi, kusambaza ujumbe wa kumkomboa Mtanzania, kwa kila ndugu, jamaa na rafiki anayeishi vijijini, (huko ambapo mafisadi wanasema wananchi hawawezi kupata habari za upinzani) ili wapige kura kwa kujua ni nani atakayewafaa na ni nani anawadanganya.
Mimi binafsi nimeshaanza hivyo kwa kutuma sms,na hata pale inapowezekana kupiga simu na kuwaeleza hali halisi. Kutokana na maongezi yangu hayo, nimeweza kuwaelimisha jamaa zangu juu ya hali halisi iliyopo nchini mwetu, ufisadi unaondelea ambao unasimamiwa na kuendelezwa na chama tawala. Wengi wameelewa uhusiaono kati ya ufisadi huo na hali mbaya inayowasibu huko vijijini. Kutokana na juhudi zangu hizo, hao nilioongea nao wameamua kuchagua kwa busara zaidi katika uchaguzi ujao. Kwa kifupi, hawadanganyiki tena.
Kwa pamoja tunaweza.