Lily Flower
JF-Expert Member
- Oct 16, 2009
- 2,553
- 1,197
Mvi ni dalili ya ukubwa, na mtu anaye ukataa ukubwa ujuwe ni f a l a tu.
Sikubaliani na wewe ndugu kuna watu wako early 20s na wana mvi nyingi kichwani.
Mvi ni dalili ya ukubwa, na mtu anaye ukataa ukubwa ujuwe ni f a l a tu.
atawatofautishaje? kama na wazee wa rika langu nao bado wanajitia poda usoni na utosini kumhadaa mwanangu.......lol
Sikubaliani na wewe ndugu kuna watu wako early 20s na wana mvi nyingi kichwani.
Awatizame usoni ataona makunyanzi ha ha ha
akiaziachia mvi hutampenda mtu wako?
]Kwani nani kakuambia ndugu yangu amezificha najaribu kukuambia kwamba sio wote wenye mvi ni wazee.
Siyo mvi tu wengine wanaficha vipara vya asili kwa kunyoa vipara kichwa kizima. Mimi msimamo wangu ni kuwa sifichi mvi wala kipara. I like it when my kids start searching for grey hair on my head and they get excited when they see some.
mtu anaweza kuwa 50+ lakini mambo anayofanya ni ya 20+. Hivyo kwa wale wanaopaka rangi mvi ziwe nyeusi hawataki kukubaliana na hali halisi.
wahahribifu wa mazingira utawaona tu.............ni vigumu kujificha.......
si kila mtu ana lengo kama unavyodhani sura ya mtu ndiyo inayotafsiri umri wa mtu na si nywele nyeupe kwani mzee wa miaka hamsini hawezi akaonekana wa thelasini, wengi wao wanapata mvi mapema sana kama vile kurithi, n.k
Nilikua sijui kumbe Mvi ni uzee??????
Nashukuru kunijulisha kua nimezeeka
kuna faida gani kuficha mvi huku makunyanzi yanakuumbua kuwa siku zimesogea................lol
Wewe una matatizo ya kisaikolojia unataka maoni ambayo yakufariji. Kwani kama maini yako yameoza hutachana nywele kwa kuwa wewe unakaribia kufa?
Umaridadi ni tabia. Kwa namna yako ya maongezi nina mashaka hufagii nyumbani kwako na nyumba yako imefubaa kwa ukungu na majani yameota mpk nje mlangoni.
Personally sioni shida na mtu kupaka Super Black, Peacock au hair dye yoyote, provided hamuathiri mtu mwingine...naamini hizo dye hazitoi harufu..
Mtu awe huru kufanya anachotaka, kwanini kupaka kwangu peacock kumshughulishe mtu mwingine?
Sikubaliani kuwa kitendo hicho tafsiri yake ni kuukataa umri, au kutaka mahusiano na wasichana wadogo..si kweli!
Mimi nina Meneja wangu ambaye ni Mlokole full, tena wa ukweli(REFER HOJA YAKO KUPENDA DOGODOGO), ambaye akiacha kutumia hizo hair dye hakika utasema kuwa hiki kibabu kinatafuta nini ofisini, lakini akipiga dye, looooh, ni kjana mwenzetu kabisa, na outlook yake nzima inabadilika kabisa, anakuwa nadhifu sana na very attractive and presentable as an office bearer.
Hii inampunguzia gossips na hivyo he feels good, hence perfomance na efficiency yake inarudi kuwa at maximum.
Kuna watu ambao akiona mvi kwa mtu tu, bila hata kujishughulisha kuwaza kuwa huyu mtu atakuwa na umri gani, basi autasikia anakuita BABU!...this is so disguisting...!
Maturity haiko kwenye mvi jamani...Kuna mkusanyiko wa matendo mengi ambao unamfanya mtu automatically aonekane amepiga mileage!
Mtu kama EL alianza kupata mvi toka ana umri mdogo sana. Sasa mtu kama huyu asingalikuwa ana fedha za kumfanya soap-soap, au tuseme angalikuwa ni masikini mchovu, angeonekana ana miaka 99.
Lakini kwa vile anapaka mafuta mazuri deodorants na perfumes, basi mvi zake hazionekani kuwa kero.
Mi sioni shida na hii makitu, naifananisha na mafuta ya ngozi ambayo inamfanya mtu aonekane na ngozi laini kuliko uhalisia..Sasa sijui kama mtu anayepaka mafuta naye anataka kubeba visichana mtaani!