Kuficha mvi ni kumtegea nani?

mimi najivunia mvi zangu sioni sababu ya kuzificha kwani nitakuwa ninajihadaa mwenyewe.............pili kwa wale ambao hawapendi ziwe nyingi jibu ni kula kwa kiasi na kufanya mazoezi................tumia njia za asilia badala ya madwa katika kupunguza kuzeeka kwa haraka.........haraka ambako husababishwa na mwili kukosa mazoezi au kuvimbishwa na milo kupita kiasi.......

Kwa hiyo unajivunia kula mno na kutofanya mazoezi au?

Mimi naona bado unajihadaa mwenyewe kwa kujilazimisha na kutulazimisha tuamini kuwa mvi ni busara na shikamoo ni hekima. Ndugu yangu, MVI na KIPARA ni matokeo ya ukosefu wa lishe iliyobalance au kuchoka kwa mwili wako kuzalisha cells zinazohusiana na ukuaji na ubora wa nywele. Kama unaamini mvi ni akili, basi next year utakuwa Head Teacher kwenye moja ya shule za kata wilayani kwako, endelea kuzifuga.
 
Mbona sio mvi peke yake zinazonyesha kua huyu jamaa ni mzee,labda wanaume wengine wanaona haya mvi lakini mie sioni mvi ni aibu kwa mwamume au tatizo lininyime raha ya kula vyangu...

au vipi?
 
Kwa hiyo unajivunia kula mno na kutofanya mazoezi au?

Mimi naona bado unajihadaa mwenyewe kwa kujilazimisha na kutulazimisha tuamini kuwa mvi ni busara na shikamoo ni hekima. Ndugu yangu, MVI na KIPARA ni matokeo ya ukosefu wa lishe iliyobalance au kuchoka kwa mwili wako kuzalisha cells zinazohusiana na ukuaji na ubora wa nywele. Kama unaamini mvi ni akili, basi next year utakuwa Head Teacher kwenye moja ya shule za kata wilayani kwako, endelea kuzifuga.

haya niliyoyawekea nyekundu hivi yanatoka wapi? mada hii siyo ya manufaa ya mtu mmoja.....ni kujadiliana bila ya kuweka taswira binafsi.................hivi Head teacher ndiye mwenye akili na kwani anazo mvi? Mvi zinafugwa au ni sehemu ya maisha kama nywele nyinginezo? Hoja hizi mbona hazina makalio hata chembe......
 
Tusitaifishe mambo binafsi......kuwa na mvi au kutukuwa nazo ni jambo binafsi
Nenda kwenye job interview na mamvi ukione.......

hoja mbili hizi zina migongano..........kama ni suala binafsi kwa nini ubaguliwe kwenye zoezi la kusaili..............ingawaje wenye vyeo kila mahali naona ni wenye mvi..................au zile zilizochakachuliwa....
 
Nilishakujibu kuwa kupendeza ni mtizamo wa mtu. Wewe unaweza kuona unapendeza na mvi mwingine akaona hapendezi.

Na kama kupendeza kwako siyo ishu, mbona uliuliza kama ukiwa na mvi unakuwa hujapendeza? Wewe umeona mvi zinakupendeza sasa juu ya nini uulize wenzako wanataka wapendeze ili iweje

haya sijayasema ni yako..........putting words in my mouth is not smart........
 
Kwa hiyo hapa unawaza kutongozwa au?

Hivi binti yako akitongozwa na kijana unapata faida gani ambayo akitongozwa na mzee utaikosa? Mi nilidhani suala ni binti yako kuwa makini na wazee na vijana!

atawatofautishaje? kama na wazee wa rika langu nao bado wanajitia poda usoni na utosini kumhadaa mwanangu.......lol
 
Kila binadamu ana mtazamo wake na maamuzi yake kulingana na kitu roho yake inapenda na kupata amani.

Wakati mwingine mvi zinakosesha amani (kwa wazee) kila ukijiangalia unaona mvi, hii inakukumbusha kuwa wewe umeshakomaa vya kutosha na kilichobaki ni kuvunwa tu! (kufa) kwa maana hiyo, ni heri uzipotezee mvi kwa kuzitia rangi ili zisikukumbushe kila mara kuwa wewe ndio umefika mwisho pamoja na kwamba ukweli unabaki pale pale. Hii inasaidia kujiona uko sawa na wengine huondoa mawazo kwamba muda wako umeisha.

Elewa mawazo haya si kwa wote. Kuna wengine hata akijiangalia hawazi chochote kuhusiana na mvi zake. Mazingira tunayoishi yanaweza kuchangia kuziona mvi ni mvuruga amani moyoni au kutojali kuona mvi. Uzee mbaya mweeeeeeh!
 
we mtoa mada huna jipya,, mjini hakuna wazee bana kuna watu wazima tu.. ni sawa na wewe tukuulize ukioga unamtegea nani? si ubaki na uchafu tu
 
Mvi ni dalili ya ukubwa, na mtu anaye ukataa ukubwa ujuwe ni f a l a tu.

Ukubwa pia huambatana na kupungua kwa nguvu za kiume na makunyanzi, navyo mnavishangilia au mnabadili nutrition kusave purpose?

Matusi ya nini? Mimi sidhani kama mtu kukataa mvi ni kukataa ukubwa. Lini ulimsikia mtu aliyebadili nywele akikataa miaka yake? WEKA TOFAUTI YA KUKATAA MVI NA KUKATAA UKUBWA.

Na nikukumbushe kuwa kuna watoto wa umri wenu nao wana mvi, na wao ni wazee?
 
atawatofautishaje? kama na wazee wa rika langu nao bado wanajitia poda usoni na utosini kumhadaa mwanangu.......lol

Kwa hiyo una certificate kwa ajili ya mwanao kuhadaiwa na vijana ila inakuuma mwanao akihadaiwa na wazee.

MWAMBIE MWANAO AACHE UHUNI, wazee au vijana wote ni uhuni. Mwambie asipende kuvuliwa chupi. Na ukiona mtoto wako anadanganyika namna hiyo, usipigane na waongo, pigana na tabia ya mwanao ya kujifanya dust bin
 
Nina shida moja maishani mwangu. Inalazimu uwe na akili kidogo kunielewa na lazima ukusidie kunielewa. Rutashubanyuma na Fazaa hebu tumieni akili zenu kidogo kabla ya kuleta hisia zenu mbele. Naomba mfikirie jambo moja kwa kutumia akili halafu mjijibu wenyewe:

Moja kati ya sifa za mtu mzee ni KUNG'OKA MENO. Ikiwa leo mtu ameng'oka meno na akaamua kuweka ya bandia, hii inatafsirikaje, body repair au kuwahadaa vijana?

Ikiwa nyumba yako imefubaa na kushika UKUNGU na wewe ukaamua kupiga rangi upya, mnataka itafsirike kuwa unawahadaa wapita njia kuwa nyumba yako si ya zamani au unaiweka nyumba yako kwenye muonekano mzuri?

Moja kati ya hormone imbalance zinazoambatana na uzee huleta tatizo la KUTOKWA NA MACHOZI, je kutumia hormone replacement ili machozi yasitoke ni kuhadaa vijana?

Mvi ni matatizo tu na sio sifa. Ni sawa na kipara. Lack of nutrition or distribution. Kama wewe unaona zinakupendeza basi si lazima iwe kwa wote. Na hiyo ndio tofauti kati ya mtu na mtu. Yupo ambaye hata nje kwake hafagii kwa kuwa tu kutofagia hakubomoi nyumba na yupo ambaye maua yasipokuwepo uwanjani kwake anasikia vibaya.

Mpo ambao gari lako likichubuka rangi unaona ni sawa tu lkn tupo ambao hata vumbi tu katika gari linatujera kwani siku zote tunapenda kuona magari yetu yaking'aa. Kwa hiyo msilazimishe watu na kuwaita ma fa la eti tu kwa sababu wao wameona si busara kuishi na mapengo ili wasifiwe kuwa wao ni wazee
 
[h=2][/h]
mvi si uzee..mbona vijana wadogo cku hizi wana mvi kibao kichwa kizima

Suala la uzee sijui latoka wapi lakini mada yaelekea wengi hamjaisoma...........pitieni maoni ya huyo mdada kwenye mtandao halafu changieni...
 
Moja kati ya sifa za mtu mzee ni KUNG'OKA MENO. Ikiwa leo mtu ameng'oka meno na akaamua kuweka ya bandia, hii inatafsirikaje, body repair au kuwahadaa vijana?

mifano hii haioani................meno kutokuwepo ni sawa na kipara...........lakini mvi nazo ni nywele huwezi kusema zimeng'oka pale............
 
Kwa hiyo una certificate kwa ajili ya mwanao kuhadaiwa na vijana ila inakuuma mwanao akihadaiwa na wazee.

MWAMBIE MWANAO AACHE UHUNI, wazee au vijana wote ni uhuni. Mwambie asipende kuvuliwa chupi. Na ukiona mtoto wako anadanganyika namna hiyo, usipigane na waongo, pigana na tabia ya mwanao ya kujifanya dust bin

haya yanatoka wapi mbona waenda nje ya mada...................nani kakwambia anavuliwa chupi?
 
Ukubwa pia huambatana na kupungua kwa nguvu za kiume na makunyanzi, navyo mnavishangilia au mnabadili nutrition kusave purpose?

Matusi ya nini? Mimi sidhani kama mtu kukataa mvi ni kukataa ukubwa. Lini ulimsikia mtu aliyebadili nywele akikataa miaka yake? WEKA TOFAUTI YA KUKATAA MVI NA KUKATAA UKUBWA.

Na nikukumbushe kuwa kuna watoto wa umri wenu nao wana mvi, na wao ni wazee?

tukubali tusikubali lenye mwanzo halikosi mwisho......................hata ukijichakachua mwisho wako siku ya siku utafika tu..........
 
we mtoa mada huna jipya,, mjini hakuna wazee bana kuna watu wazima tu.. ni sawa na wewe tukuulize ukioga unamtegea nani? si ubaki na uchafu tu

Tangia lini mvi zikawa ni uchafu?
 
Kila binadamu ana mtazamo wake na maamuzi yake kulingana na kitu roho yake inapenda na kupata amani.

Wakati mwingine mvi zinakosesha amani (kwa wazee) kila ukijiangalia unaona mvi, hii inakukumbusha kuwa wewe umeshakomaa vya kutosha na kilichobaki ni kuvunwa tu! (kufa) kwa maana hiyo, ni heri uzipotezee mvi kwa kuzitia rangi ili zisikukumbushe kila mara kuwa wewe ndio umefika mwisho pamoja na kwamba ukweli unabaki pale pale. Hii inasaidia kujiona uko sawa na wengine huondoa mawazo kwamba muda wako umeisha.

Elewa mawazo haya si kwa wote. Kuna wengine hata akijiangalia hawazi chochote kuhusiana na mvi zake. Mazingira tunayoishi yanaweza kuchangia kuziona mvi ni mvuruga amani moyoni au kutojali kuona mvi. Uzee mbaya mweeeeeeh!

wazungu husema.........."only the truth will set you free"..............ukijidanganya mwenyewe ni kwa muda mfupi tu ni vyema ukakubaliana na ukweli wako kuwa saa zimesogea kuelekea majogoo.......................
 
Back
Top Bottom