Kufaulu STD 7 kwenda shule za serikali imekuwa rahisi sana

Ulimakafu

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
29,026
10,673
Siku hizi shule ya msingi moja kufaulisha wanafunzi wote au 50%+ siyo tatizo tena kama ilivyokuwa siku za nyuma,maana ilikuwa kufaulu mpaka uchemshe sana bongo.Hofu ni kwamba quality ya wanafunzi hao wanaojiunga na shule za sekondari sasa ni chini sana.Ndio maana wazazi wenye nazo wanawapeleka watoto wao private schools ambako hata mtihani wao wa kujiunga ni mzito kuuzidi huo wa serikali.
 
Wakati hule mie naingia form 1 yalikuwa masomo matatu kwa 50 maks kila somo=150 na kufaulu ulitakiwa mvulana kuanzia 80 maks na waschana 70/75 lakini leo masomo 5 =250maks lakini cha ajabu watoto wanapelekwa form1 kwa maks below 50

hapo ndo hesabu inapogoma kuingia kichwani kama Tanzania tuna elimu ama tuna watu wanaoingia na kushinda madarasani na kbaya kuliko vyote ni pale unapowakuta hawa wanaopelekwa darasani kwa ufaulu wa 1/8maks wanahudumiwa na walimu wasiozidi 3 shule nzima...huwa najikuta nashikwa na tumbo la kuhara

Mimi naona Tanzania sahv elimu imetushinda na tunachokfanya ni kujarbu ujinga,ngoja tuone mwisho wake nini.
 
50/250=1/5=20% ndiyo ya kujiunga na form 1?Kichekesho cha mwaka,mbaya zaidi hizo 20% zinaweza kuwa za kudesa au saidia ufaulu wa shule.
 
tuna kazi kweli kweli.
halaf ati utasikia serikali inatafuta mchawi ni nani pindi matokeo ya kidato cha nne yanapotoka eti kwanini wanafunzi wamefeli kiasi hicho.pambafu zao serikali yetu ni ya kinafki inataka kujifanya inajali wananchi angali ndo inawaangamiza. crap crap craaaap. we sikilizia matokeo ya kidato cha nne mwaka huu ndo utajua!
 
nyie mnataka watu wasissome? kwani kufaulu sana ndio kigezo cha hekima na uadilifu? hnyie mliofaulu sana na kwenda special skuli mko wapi sasa hivi? si mmekuwa mafisadi na kupenda siasa tu
 
Primary ukijua kusoma na kuandika with some basic math inatosha, sioni maana ya kumzuia mtu kuendelea na elimu kama hana matokeo mazuri primary.
 
.Ndio maana wazazi wenye nazo wanawapeleka watoto wao private schools ambako hata mtihani wao wa kujiunga ni mzito kuuzidi huo wa serikali.

sijaelewa hapo. Kwani mtihani wa darasa la 7 kuingia form one unatofautiana kati ya shule za serikali na binafsi au?
 
sijaelewa hapo. Kwani mtihani wa darasa la 7 kuingia form one unatofautiana kati ya shule za serikali na binafsi au?

Dada polepole nazani anamahanisha interview za kuingilia private schools like marian galz zimekuwa ngumu kuliko national examination,

Wadau sio kufaulu la saba tu, nowdays hadi kufika university sio ishu, its too easy as life is change, madogo wanashinda bar tu kukata kilaji wanapata maksi mbovu but wanachaguliwa varsity na wakifika huko ni bia tu na mademu wakati wakisubiri migomo itokee
 
Zamani watu wengi walikuwa wanafaulu ila shule zilikuwa chache. Halafu kuna mjumbe mmoja amesema wanachukuliwa hadi chini ya marks 50, hiyo sio kweli hata kidogo. Mwanafunzi akiwa chini ya marks 100 hachukuliwi hata kama amepata 99. Sema kiwango cha elimu kinachotolewa ndio utata mtupu.
 
@tz guy, nakubaliana na wewe kabisa. Watu walikuwa wanafaulu sana ila nafasi hawapati. Kuna shule nyingi za sekondari mpya. Mnataka watu wasipelekwe kusoma?
Watu waliofaulu kimagendo ndio huona na wenzao wote wanafaulu kimagendo. Elimu ya sahv imekuwa ngumu sana ndio maana madogo kila kukicha wanatafuta tuition centres maana darasani pekee hapatoshi.
Cha kulilia hapa ni ubora wa elimu ila si kweli kwamba watu wanapelekwa sekondari wakati hawajafaulu, vinginevyo utuwekee matokeo ya hao waliofeli std 7 halafu wakachaguliwa kwenda sec.
 
Tatizo ni sera mbovu za elimu zinaondeshwa na nchi, zimejikita zaidi katika kuangalia quantity of education inayotolewa na sio quality of education provided na tukiendelea kuendesha elimu hii kisiasa zaidi tutaendelea kuwa na wahitimu wa hadi kidato cha nne wasiojua kusoma wala kuandika, inashangaza kuona mwanafunzi yuko sekondari lakini hajui kusoma wala kuandika, kazi kwa wadau wa elimu, viongozi wetu hawana uchungu na elimu, watoto wao wako wapi? "Ukitaka kuona utamu wa ngoma cheza" je wao hucheza nasi?
 
Private schools wapo kibiashara zaidi na ili kushinda ushindani lazima watoe elimu bora ambao huanzia katika enrollment ya pre-form one na kuendelea, lakini ktk shule zetu hizi za "kajamba nani" mkuu wa shule anaambiwa ukifaulisha chini ya kiwango unashushwa cheo, jitihada azifanyazo ni kuvujisha mitihani ili atetee ungwa....kwa hilo unadhani kuna wmanafunzi atakaye feli? Tumbo jamani watu wanatetea matumbo yao, hakuna elimu hapa, utasikia tumefaulisha kwa zaidi ya % hamsini badala ya kusema tumevujisha mitihani kwa zaidi ya % 50.
 
Tatizo ni sera mbovu za elimu zinaondeshwa na nchi, zimejikita zaidi katika kuangalia quantity of education inayotolewa na sio quality of education provided na tukiendelea kuendesha elimu hii kisiasa zaidi tutaendelea kuwa na wahitimu wa hadi kidato cha nne wasiojua kusoma wala kuandika, inashangaza kuona mwanafunzi yuko sekondari lakini hajui kusoma wala kuandika, kazi kwa wadau wa elimu, viongozi wetu hawana uchungu na elimu, watoto wao wako wapi? "Ukitaka kuona utamu wa ngoma cheza" je wao hucheza nasi?
Kweli mkuu.
 
Back
Top Bottom