Kufariki kwa Mwandishi wa Habari Makubo; Je kuna mkono wa mtu?

Solomon David

JF-Expert Member
Mar 1, 2009
1,148
16
Awali - kuna habari kuwa mwandishi wa habari wa Tarime ambaye amehusika sana kwenye kutoa habari za uchafuzi wa mazingira uliofanywa na kampuni za madini tarime amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo (moyo umepasuka).

Update:

Kuna taarifa nilizopata muda mfupi uliopita kuwa familia ya marehemu Makubo inahisi kuwa kuna mkono wa mtu umehusika kwenye kifo cha ghafla na cha mazingira ya kutatanisha cha ndugu yao.

Inasemekana kuwa mazishi hayatafanyika mpaka uchunguzi maalumu ufanyike kuhusu kifo cha Makubo.

Zaidi ya yote - RIP Haruni Makubo.

Watu wa Tarime na watanzania wamepoteza mtu muhimu sana kwenye vita ya kutafuta haki dhidi ya kampuni kubwa la madini.
 
I am trying to get in touch na ndugu mmoja ambaye amekuwa akifanya kazi kwa karibu sana na marehemu na issue yenyewe.Kama ni kweli basi Tanzania na watanzania tutakuwa tumeanza kuvuna matunda ya mwekezaji huyu.
 
Poleni ndugu, jamaa na marafiki. Tumempoteza mpashanaji wetu wa habari. Mungu ampumzishe kwa amani. Alluta continua!
 
I am trying to get in touch na ndugu mmoja ambaye amekuwa akifanya kazi kwa karibu sana na marehemu na issue yenyewe.Kama ni kweli basi Tanzania na watanzania tutakuwa tumeanza kuvuna matunda ya mwekezaji huyu.

Si walau ungeanza kwa kutoa pole kabla ku politicise msiba

RIP Makubo
 
He must have died a natural death as he was following Barickgate issue as did Stan Katabalo when folowing Loliondogate. Though he has perished into the thin air, his legacy will live on as that of Stan Katabalo.
RIP Makubo!.
 
Last edited by a moderator:
Kufariki kwa ugonjwa sio kuuwawa? Anyway Mungu amrehemu ndugu Makubo.
 
Nawapa pole ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu. Nami nimezipokea taarifa za msiba huo kwa mshtuko mkubwa na masikitiko.

Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi.

Amina.
 
Mwandishi wa Habari Leo afariki dunia, ni Makubo Haruni.
Na Nashon Kennedy,Mwanza

MWANDISHI wa habari mwakilishi wa gazeti hili wa mkoa wa Mara, Makubo Haruni (45), amefariki dunia.

Haruni alifikwa na mauti majira ya saa tatu, usiku wa kuamkia jana, wakati akiwa njiani kupelekwa kutibiwa katika Hospitali ya Dk. Winani, iliyopo mjini Tarime.

Kwa mujibu wa kijana mkubwa wa Haruni, Marwa Makubo, akizungumza kwa njia ya simu kutoka Tarime alisema kuwa marehemu baba yake alirejea nyumbani Mtaa wa Songambele, majira ya saa mbili usiku juzi na kwamba baada ya dakika chache alianza kulalamika kuwa anajisikia moyo unampasuka.

"Baba alifika akiwa na hali isiyokuwa ya kawaida na baadaye akaanza kulalamika kuwa moyo unapasuka," alisema Marwa.

Aliongeza kuwa alimsogelea na kuanza kumpukutishia upepo kwa kutumia nguo, lakini marehemu aliishiwa nguvu, na ndipo akasaidiana na majirani kumkimbiza hosipitalini ambapo hata hivyo mganga wa zamu aligundua kuwa alikuwa ameishakata roho.

Marwa alisema kwamba siku nne kabla ya kifo cha baba yake , alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa malaria, lakini kufikia juzi alikuwa amepata nafuu baada ya kutumia dawa.

Kaka wa Haruni, Mussa Haruni, aliliambia gazeti hili kuwa mwili wa marehemu ambao jana ulikuwa unahifadhiwa chumba cha maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime, utasafirishwa kwenda kijijini Muriba kwa mazishi baada ya taratibu za mazishi kukamilika.

Marehemu makubo alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Muriba, wilayani Tarime na baadaye katika Shule ya Sekondari ya Ikizu, wilayani Bunda, mkoani Mara. Ameacha mke na watoto wanne.
MWISHO. (Habari Leo)
 
Tanzania tuna matatizo na vifo vya kutatanisha haswa kwa watu mashuhuri maana ninaowakumbuka ni kama Mh.Malima,Mh.Kolimba,Mh.Dr Omar Ali Juma,Mh.Chifupa,Mh.Chacha Wangwe,Mh.Sokoine na Mh.Ditopile ,yaani hao ambao ni baadhi tu kwa ninaowajua vifo vyao vimekuwa gumzo kubwa hapa mjini ,hivi tunahitaji Scortland Yard au FBI na CIA kuchunguza vifo vyao ,serikali ya CCM imekuwa haiaminiki tena na vyombo vyake vinatia mashaka katika kufanya jambo kwa uwazi na haki ,haswa kwa kutokufikia uchunguzi uliokamilika na wenye kuwekwa wazi kwa wananchi ,just watakwambia amekufa kifo cha kawaida. na vile vile kwa CCM kufikia kuvitumia vyombo hivyo katika kufanya hujma za uchaguzi ni wazi kabisa kuna katika safu ya CCM watu ambao wanaweza kuuwa na vyombo hivi vikawakingia ubavu. Tunahitaji Chama mbadala ili yote haya yaondolewe na ikiwezekana uitishwe uchunguzi mpya kwa wote hao hata kama tutafilisika kwa kukodi mashirika ya nje kuja kutufanyia uchunguzi.

Sina zaidi ila nikusema wafiwa wawe na subira na haya tunayokwenda nayo yana mwisho kwani hakuna lisilokuwa na mwisho ,iko siku hukohuko CCM atatokeza kiongozi shujaa asie na uswahiba na si mnafiki na unafiki na ambae ataridhika na cheo chake,ataridhika na mali yake na ataridhika na umasikini wake na kusimamia haki itendeke na kuona haki iliyosawa inatendeka kwa kila Mtz bila ya kujali itikadi ya Chama Chake.
RIP Makubo.
 
Raha ya milele umpe Ee bwana,na mwanga wa milele umuangazie!
APUMZIKE KWA AMANI,AMINA

We will be missing you Harun,you will always be in our minds!
 
Tanzania tuna matatizo na vifo vya kutatanisha haswa kwa watu mashuhuri maana ninaowakumbuka ni kama Mh.Malima,Mh.Kolimba,Mh.Dr Omar Ali Juma,Mh.Chifupa,Mh.Chacha Wangwe,Mh.Sokoine na Mh.Ditopile ,yaani hao ambao ni baadhi tu kwa ninaowajua vifo vyao vimekuwa gumzo kubwa hapa mjini ,hivi tunahitaji Scortland Yard au FBI na CIA kuchunguza vifo vyao ,serikali ya CCM imekuwa haiaminiki tena na vyombo vyake vinatia mashaka katika kufanya jambo kwa uwazi na haki ,haswa kwa kutokufikia uchunguzi uliokamilika na wenye kuwekwa wazi kwa wananchi ,just watakwambia amekufa kifo cha kawaida. na vile vile kwa CCM kufikia kuvitumia vyombo hivyo katika kufanya hujma za uchaguzi ni wazi kabisa kuna katika safu ya CCM watu ambao wanaweza kuuwa na vyombo hivi vikawakingia ubavu. Tunahitaji Chama mbadala ili yote haya yaondolewe na ikiwezekana uitishwe uchunguzi mpya kwa wote hao hata kama tutafilisika kwa kukodi mashirika ya nje kuja kutufanyia uchunguzi.

Sina zaidi ila nikusema wafiwa wawe na subira na haya tunayokwenda nayo yana mwisho kwani hakuna lisilokuwa na mwisho ,iko siku hukohuko CCM atatokeza kiongozi shujaa asie na uswahiba na si mnafiki na unafiki na ambae ataridhika na cheo chake,ataridhika na mali yake na ataridhika na umasikini wake na kusimamia haki itendeke na kuona haki iliyosawa inatendeka kwa kila Mtz bila ya kujali itikadi ya Chama Chake.
RIP Makubo.

Serikali ya CCM imerithi mbinu za mauaji kama haya kutoka kwa waingereza. Kumbuka ktk utawala wa tony bair yule mkurugenzi wa bbc aliyeripoti siri za njama za vita kati ya marekani/uingereza na irak alivyouawa. Mambo ya loliondo gate, Kolimba(tena huyu aliuawa kwa mercuric oxide gas kwenye mic), n.k.

S ajabu kwamba hata huyu mwandishi kwa kuripoti uchafuzi wa mazingira huo tarime ameonekana anajua siri nyingi na angezianika baada ya ripoti kujadiliwa bungeni kwa hiyo imeonekana ni bora aondoke mapema na huenda alikataa mlungula.
 
Back
Top Bottom