Kufariki ghafla kwa Mwendesha Mashtaka kesi ya Mallya

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
2008-10-16 13:40:56
Na Mary Edward Dodoma

Mwedesha Mashitaka katika kesi ya Deus Mallya, Mrakibu wa Polisi, William Maganga, amefariki dunia gafla wakati akiwa katika harakati ya kuifanyia uchunguzi barua ya dhamana ya Mallya, iliyokuwa na kasoro kadhaa.

Akizungumzia tukio hilo, askari polisi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema Oktoba 7 mwaka huu, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya,Thomas Simba, alimtaka mwendesha mashitaka huyo kuichunguza barua ya dhamana iliyoletwa makahamani hapo na Julius Michael kwa lengo la kumwekea dhamana Mallya.

Uchunguzi huo ulitokana na dosari kadhaa zilizojitokeza kwenye barua hiyo, ikiwemo kukosewa kwa jina la mtuhumiwa lililoandikwa Dinis Maliwa badala ya Deus Mallya na pia mhuri uliogongwa kwenye barua hiyo haukusomeka vizuri.

Kutokana na kasoro hizo, hakimu huyo alitilia shaka barua hiyo na kumtaka mwendesha mashitaka, Maganga kuichunguza kwa makini barua hiyo na kesi hiyo kusogezwa mbele hadi Oktoba 13 mwaka huu, ambapo mwendesha mashitaka huyo alitakiwa kutoa taarifa za uchunguzi wa barua hiyo.

Kwa mujibu wa askari huyo, marehemu Maganga alipatwa na kiharusi ghafla siku hiyo hiyo aliyoahidi kuichunguza barua hiyo na kufariki dunia Oktoba 13 siku ambayo alitakiwa kutoa mahakamani taarifa ya uchunguzi wa barua hiyo.

Kutokana na kifo hicho, kumeibuka maneno mengi toka kwa baadhi ya watu, wakikihusisha kifo hicho na imani za kishirikina.

Lakini mmoja wa wanafamilia ya Marehemu Maganga alipoulizwa kuhusiana na tetesi hizo, alikataa na kusema sababu ya kifo chake ni kiharusi.

Hata hivyo, akiongea kwa sharti la kutotajwa jina lake, alikiri kwamba kuna tabia ya baadhi ya watu kunapotokea kifo, kuwa na maoni yao, hususan watu wanaoamini ushirikina.

Hatma ya kesi hiyo ya Mallya aliyeshtakiwa kwa kosa la kuendesha gari kwa mwendo wa kasi na kusababisha kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya Chadema, Marehemu Chacha Wangwe, itajulikana Oktoba 27 mwaka huu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mwendesha Mashitaka, Mrakibu wa Polisi anayeendesha kesi hiyo kwa sasa, Porcup Urio, kumwomba hakimu anayesikiliza kesi hiyo, kuipangia tarehe nyingine kwa madai kuwa, kumekosekana maelezo ya mtu mmoja wa upande wa mashtaka, ambaye anadaiwa kuwepo safarini.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Simba alimtaka mwendesha mashtaka kukamilisha taratibu zote ili kesi hiyo ianze kusikilizwa mara moja katika tarehe iliyotajwa, vinginevyo mahakama itachukua maamuzi mengine.

My Take:
Well, what can I say. Mauti ndiyo hayo tena. Na hii kesi sidhani kama itafika mahali, kwani the next ni barua kutoweka na yule jamaa aliyejaribu kumpa dhamana Mallya kutokuonekana. Je, Mallya naye atapatwa na ugonjwa wa ghafla na hivyo kesi nayo kuisha? I'll give you 80 percent hii kesi haiendi popote.
 
baadhi ya magazeti leo wameandika hii habari na kuhusisha kifo hicho na deus mallya...ni ufinyu wa fikra!!!!
 
mmmmmh

maneno yamepotea. binafsi nadhani ifikie mahali kesi za ajali za hawa wakubwa zisimalize muda wa mahakama kwani historia inaonyesha huwa hazifiki mwisho lazima kitokee kitu kukizuia,,,,,, hivi ile kesi ya Ajali ya Salome Mbatia ilifikia wapi?
 
No MKJJ,

Kesi itasilikilizwa mpaka mwisho na hukumu itatolewa.wasi wasi wangu ni adhabu atakayopewa Deus kwani shitaka ni kuendesha gari bila leseni na kusababisha kifo. Usije kushangaa akapigwa faini ya 15,000 tu dogo anarudi mtaani. Kufa kwa Maganga kwa mtazamo wangu siamini kama ni nguvu za giza ili kesi ikose muelekeo. Kwani Deus anajua Polisi wana waendesha mashitaka wangapi na atamudu kuwamaliza wote? Vipi kuhusu hakimu, mashahidi na yeye mwenyewe anajua atakufa lini?

Maganga (RIP) siku zake zilifika tu na kwa bahati mbaya tukio limegongna na hiyo kesi. MKJJ, huyo Deus angekuwa amegonga na kumuua mwenda kwa miguu wa kawaida au aliyekuwa akimuendesha ni girl friend wake au rafiki mwingine yeyote hiyo kesi ingekuwa imekwisha siku nyingi sana. Tatizo aliyeuwawa katika ajali ni mtu prominent (MP tena wa CHADEMA).
 
2008-10-16 13:40:56
Na Mary Edward Dodoma

Mwedesha Mashitaka katika kesi ya Deus Mallya, Mrakibu wa Polisi, William Maganga, amefariki dunia gafla wakati akiwa katika harakati ya kuifanyia uchunguzi barua ya dhamana ya Mallya, iliyokuwa na kasoro kadhaa......


Uchunguzi huo ulitokana na dosari kadhaa zilizojitokeza kwenye barua hiyo, ikiwemo kukosewa kwa jina la mtuhumiwa lililoandikwa Dinis Maliwa badala ya Deus Mallya na pia mhuri uliogongwa kwenye barua hiyo haukusomeka vizuri........

.

Mimi namfahamu Denis Maliwa ambaye ni ofisa wa jeshi la magereza. Sisemi kuna uhusiano wowote, nimeshangaa tu. Suala la majina kufanana pia lipo. Na pengine pia ni bahati mbaya tu kuwa huyo mwendesha mashitaka amepatwa na kiharusi kipindi hiki.
 
Mimi namfahamu Denis Maliwa ambaye ni ofisa wa jeshi la magereza. Sisemi kuna uhusiano wowote, nimeshangaa tu. Suala la majina kufanana pia lipo. Na pengine pia ni bahati mbaya tu kuwa huyo mwendesha mashitaka amepatwa na kiharusi kipindi hiki.

Huyo Denis Maliwa yuko kifungoni Mogorogo?
 
yote yanawezekana hasa katika nchi ambayo watu wanaishi kwa shaka na hisia. ndiyo matokeo ya usiri usiri.
 
Lakini si inawezekana kuteuwa mwendesha mashtaka mwingine ?

Uwezekano wa kuteuliwa mwingine upo na atakayeteuliwa you can bet he will favor him!
Am not a doctor ila najua kuna sindano ukimchoma mtu unaweza kusababisha heart attack hamna za kiharusi?
 
My Take:
Well, what can I say. Mauti ndiyo hayo tena. Na hii kesi sidhani kama itafika mahali, kwani the next ni barua kutoweka na yule jamaa aliyejaribu kumpa dhamana Mallya kutokuonekana. Je, Mallya naye atapatwa na ugonjwa wa ghafla na hivyo kesi nayo kuisha? I'll give you 80 percent hii kesi haiendi popote.

Please add my 15% hapo
 
Kafa kwa mapenzi ya Mungu kuna anaebisha?

Mkuu Masatu,

Kwanini isiundwe tume kuchunguza? Maana huo ndo mwendo wetu...hakuna mapenzi ya Mungu hapo ....na Deus naye akifa ghafla itakuwa mapenzi ya Mungu?
 
Mkuu Masatu,

Kwanini isiundwe tume kuchunguza? Maana huo ndo mwendo wetu...hakuna mapenzi ya Mungu hapo ....na Deus naye akifa ghafla itakuwa mapenzi ya Mungu?

Kama ni tume iundwe tume ya kuchunguza kifo cha Wangwe kwanza....
 
Uchunguzi wa kifo cha Wangwe uliishafanyika mkuu, na polisi walishatoa ripoti yao...

Unachanganya tunazungumzia kuundwa tume sio postmortem report. Rejea majibu ya Spika Sitta wakati mjane Mariam Wangwe alihoji kuhusu hilo....
 
Back
Top Bottom