Kufanya haya mwanaume haipendezi. . . (Mwendelezo wa sisi ni wanaume bwana!)

haipendezi mwanaume kuwachunga na kuwafuata fuata dada zake, wakati yeye anasarandia dada za wenzake na anasahau kila mwenye dada hakosi shemeji....
 
haipendezi mwanaume kumpiga magumi mkeo.....mwanamke hapigwi ngumi, anapigwa na kitenge cha wax maana kanga ina maneno....
 
haipendezi mwanaume kuongea na simukwa saurti kuuuuuubwa mpaka nyumba ya kumi wanakusikia
 
inakera sana dume zima linamuachia mkewe kuwa mmbeya wa mtaa mzima na kubwabwaja kama masanja
 
haipendezi kabisa kumuona mwanaume anajitolea kwa kila hali kutafuta maisha halafu mkewe anashinda saluni, bar na kugawa kwa watoto
 
haipendezi mwanaume unakula nyama choma bar huku nyumbani kwako wameshindia ugali kwa matembele
 
yani inatisha kweli dume linaosha magari wiki nzima huku mama yuko nyuma ya nyumba hata kusaidia kutafuta income hakuna zaidi ya kupigwa kwiki mabandani
 
Back
Top Bottom