Kufa Kufaana, Hata Msiba Wa Kanumba!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,464
113,537
Wanabodi,

Japo binafsi yangu sii mpenzi wa bongo movies ila huu msiba wa Kanumba umeigusa familia yangu haswa wife na girls wetu watatu ni wapenzi wakubwa wa bongo movies.

Baada ya wife kunisindikiza msiba wa Regia mpaka kwenye mazishi Ifakara leo ni zamu yangu kumkampany kwenye msiba wa Kanumba hivi ninavyoandika niko mitaa ya Sinza eneo la msiba.

Cha kwanza barabara ya Tandale kipande cha mbele ya nyumba ya Kanumba kimefungwa, barabara nzima imeshehenezwa mahema yenye viti watu wamejaa mpaka wamesimama!.

Parking za magari ni kuanzia Kijiweni zikitapakaa mpaka Lion. Kutokana na wingi wa watu, idadi kubwa ya waombolezaji wamejikalia baa za jirani wakijipooza na machungu ya msiba!

Baa zote zimefurika, wahudumu wanalakamika tangu ile juzi ni hakuna kulala, watu wanakunywa usiku kucha na asubuhi ndio kwanza wanaongezeka mpaka wanashangaa hivi hawa waombolezaji wa msiba huu hawana kwao, au ndio wamehamia Sinza!.

Hoteli zote, lodge zote na guest zote za maeneo haya ziko fully booked na waombolezaji toka ugenini japo hawajaja na mabegi ya nguo!

Japo ni tukio la msiba, wengi wa wateja ni waombolezaji, kama kawaida ya masuper stars ni full ubishoo wala nyuso za huzuni hazionekani! Kitu kizuri kuhusu hizi baa zote za jirani, zina make ile mbaya!. Mpaka wanatamani mazishi yangesogezwa mbele kidogo mpaka angalau Jumamosi ijayo!.

Ama kweli kufa kufaana, na jinsi mastaa wa bongo walivyojazana Sinza, wenye baa za hapa wana death wish baada ya Kanumba na mwingine afuatie na mwingine na mwingine alimradi wao waendelee kuzi make!

RIP Kanumba!
 
Alienda akakosa chumba na alikuwa kaiba HG teh teh joke
dili likagonga mwamba siunajua pasaka na ma HG ndo wanapata chance za kutoka

hahaahaaa usinikumbushe hg wangu karudi saa moja moja hivi..... Toka jana loh
 
hahaahaaa usinikumbushe hg wangu karudi saa moja moja hivi..... Toka jana loh
Hahahaaaa huyo we ngoja kama hajabeba na mimba sijui....siunajua wale hawajuagi lolote labda kama shemeji alimsaidia kujua utaratibu wa tamtam lol
Mwambie abadili Tabia
 
Nilitimiza wajinu wangu kwa kumweleza madhara ya mapenzi, utamu na uchungu wake, nikamuasa ajichunge na kumwonyesha condom za kike na kiume na jinsi ya kuzitumia. Akiwa off weekend na sikukuu akili kichwani mwake maana kwa 'mamdogo' anapoaga kwenda pasije kuwa kwa 'mamdoooooooogooooooooo' akarudi kwao na zawadi.....

Hahahaaaa huyo we ngoja kama hajabeba na mimba sijui....siunajua wale hawajuagi lolote labda kama shemeji alimsaidia kujua utaratibu wa tamtam lol
Mwambie abadili Tabia
 
Nyuma ya pazia naskia marehemu SK alikuwa memba wa freemasöns.Anatha tin ni kwamba coy yake ilikuwa inaingiza lots of cash annually,14bil!damn is t true guyz!
 
Nyuma ya pazia naskia marehemu SK alikuwa memba wa freemasöns.Anatha tin ni kwamba coy yake ilikuwa inaingiza lots of cash annually,14bil!damn is t true guyz!

hata mimi nina kawasiwasi maana nikunganisha dots na facts naona kama kuna kaukweli hivi..."usilolijua ni kama usiku wa giza"
 
Wanabodi,
Japo binafsi yangu sii mpenzi wa bongo movies ila huu msiba wa Kanumba umeigusa familia yangu haswa wife na girls wetu watatu ni wapenzi wakubwa wa bongo movies.

Baada ya wife kunisindikiza msiba wa Regia mpaka kwenye mazishi Ifakara leo ni zamu yangu kumkampany kwenye msiba wa Kanumba hivi ninavyoandika niko mitaa ya Sinza eneo la msiba.

Cha kwanza barabara ya Tandale kipande cha mbele ya nyumba ya Kanumba kimefungwa, barabara nzima imeshehenezwa mahema yenye viti watu wamejaa mpaka wamesimama!.

Parking za magari ni kuanzia Kijiweni zikitapakaa mpaka Lion. Kutokana na wingi wa watu, idadi kubwa ya waombolezaji wamejikalia baa za jirani wakijipooza na machungu ya msiba!.

Baa zote zimefurika, wahudumu wanalakamika tangu ile juzi ni hakuna kulala, watu wanakunywa usiku kucha na asubuhi ndio kwanza wanaongezeka mpaka wanashangaa hivi hawa waombolezaji wa msiba huu hawana kwao, au ndio wamehamia Sinza!.

Hoteli zote, lodge zote na guest zote za maeneo haya ziko fully booked na waombolezaji toka ugenini japo hawajaja na mabegi ya nguo!.

Japo ni tukio la msiba, wengi wa wateja ni waombolezaji, kama kawaida ya masuper stars ni full ubishoo wala nyuso za huzuni hazionekani!. Kitu kizuri kuhusu hizi baa zote za jirani, zina make ile mbaya!. Mpaka wanatamani mazishi yangesogezwa mbele kidogo mpaka angalau Jumamosi ijayo!.

Ama kweli kufa kufaana, na jinsi mastaa wa bongo walivyojazana Sinza, wenye baa za hapa wana death wish baada ya Kanumba na mwingine afuatie na mwingine na mwingine alimradi wao waendelee kuzi make!.

RIP Kanumba!.
leo ni kumbukumbu ya miaka 9 kifo cha Kanumba
RIP Stephen Kanumba.
P
 
Back
Top Bottom