Kuelekea Ujamaa Mamboleo - Toward Neo-Socialism

Kisayansi kama wanadamu hatuna tofauti,wote tunahitaji amino acid block ambayo ndiyo basic form of life,Nyani pointi yake yeye ni kuwa tumealaaniwa na Mungu or something,huo ni uamuzi wa imani yake na ndio maana siwezi kendelea kubishana naye....Na ndiyo maana mjadala huu inabidi tuamue sasa kwamba kama ni Mungu(Rejea red highlits hapo juu) Then muedelee kusema ndivyo tulivyo kwasababu Mungu aliamua kuwapendelea wazungu.

Tukija kwene mazingira nakubaliana kuwa inawezekana ikawa ni sababu iliyowapumbaza wenyeji wa maeneo kama ya Afrika...Lakini ndugu yangu kama umeyataja matatizo yote hao ambayo yameipata Afrika ndio maana halisi kabisa ya how Afrika was shaped,kuanzia utumwa,ukoloni,ukoloni mamboleo,yote hayo yana impact kubwa sana kwa maendeleo ya Afrika.
Chukulia tu mfano rahisi wa utumwa,walibebwa wale wote wenye nguvu,vijana,na wakabakizwa watoto wadogo na vizee viajuza,sasa nani atakaeendeleza jamii na kufanya kazi za kimaendeleo?watoto?maajuza?

Hilo gap hapo lilikuwa ndo mwanzo wa yote hayo kwasababu sasa wazee hao wanakufa kwa njaa na watoto wanabaki hoe hae bila hata ya kupata mafunzo ya namna ya kukabiliana na mazingira. Wakuu kusoma tu history na reality yenyewe ni vitu viwili tofauti,kama kwenye news ambazo bado ziko manipulated na wale wale walotunyima uhuru kuwa sasa tuko huru,in reality hatuko huru na ndo ukweli huo na historia ndio italiweka hilo wazi....Tutaandika hapa lakini historia ikija kuandikwa wataangalia yapi yanamake sense na yapi yamekuwa kweli.

Baada ya matatizo yote hayo ya utumwa ukoloni nk kuwa abolished,je si bado tuna mawasiliano na wale wale waliokuwa wakitutawala?je mawasiliano hayo yamekatwa? Je mawasiliano na hayo yanaendana na uhuru wa kweli na maamuzi fair na yenye faida kwa pande zote? Na mawasiliano hayo yakikatwa kama tusipokubaliana na masharti yao tuta survive? Ni mawazo ambayo viongozi wetu wanatakiwa wajiulize,je tukiacha bakuli tutaendelea? So far hapo ndo tulipo,bakuli na corruption,lakini kuwajumuisha mashujaa wetu waliompiga mkoloni na kusema eti na wao ndivyo walivyo kwangu binafsi hakuna mantiki.

Niko kwenye maboksi hivyo nitajibu kwa kifupi tu. Hii posti inampa points NN bila ya yeye ku-press key yoyote hile.

Kama tungekuwa wabunifu, tungekuwa na silaha za kujilinda wenyewe kabla ya wakamata watumwa kuja.

Wakati wakoloni wanakuja, wakabila mengi yalifanya resistance kubwa kuupinga ukoloni. Tena watu walipigana kwa kutumia primitive weapons.

Kama tuliweza ku-resist wakoloni kutoka Ulaya wenye bunduki zilizokuwa modern, tungeweza kufanya juhudi hizohizo kwa wafanyabiashara ya utumwa ambao walitumia magobore yaliokuwa very primitive.

Hatukuweza kuzuia utumwa kwa sababu tulishiriki. Empires za kina mirambo, Mkwawa zilikuwa kwa sababu ya biashara hiyo. Hivyo hakuna ukweli kuwa aliyekuwa na nguvu ndio aliyechukuliwa. Aliye na nguvu alishiriki na hakuna gap yoyote.
 
Zakumi, vipi Afrika Kusini? Bila wazungu kuwepo kwa wingi na kushikilia madaraka kwa muda mrefu kungekuwa jinsi kulivyo leo hii? Mwakani wana host mashindano ya kombe la dunia kwa sababu ya uchumi na miundombinu waliyonayo. Kwa nini hayo mashindano hayajawahi kufanyika Afrika hata mara moja?

Kuna uwezekano kuwa wazungu ndio gundi ya taifa kule sauzi.
 
Niko kwenye maboksi hivyo nitajibu kwa kifupi tu. Hii posti inampa points NN bila ya yeye ku-press key yoyote hile.

Kama tungekuwa wabunifu, tungekuwa na silaha za kujilinda wenyewe kabla ya wakamata watumwa kuja.

Wakati wakoloni wanakuja, wakabila mengi yalifanya resistance kubwa kuupinga ukoloni. Tena watu walipigana kwa kutumia primitive weapons.

Kama tuliweza ku-resist wakoloni kutoka Ulaya wenye bunduki zilizokuwa modern, tungeweza kufanya juhudi hizohizo kwa wafanyabiashara ya utumwa ambao walitumia magobore yaliokuwa very primitive.

Hatukuweza kuzuia utumwa kwa sababu tulishiriki. Empires za kina mirambo, Mkwawa zilikuwa kwa sababu ya biashara hiyo. Hivyo hakuna ukweli kuwa aliyekuwa na nguvu ndio aliyechukuliwa. Aliye na nguvu alishiriki na hakuna gap yoyote.

Hahahahaha...I'm telling you. This a cakewalk!

Na umesahau kitu kimoja. Watawala wetu wa enzi hizo walisaini mikataba bila hata kujua wanafanya nini..bogus treaties. Kwa hiyo hata kusoma walikuwa hawajui.....need I say more?
 
Jmushi1,
Unajua maendleo yote ya nchi zetu za kiafrika yanatokana na Kuiga wala sii ubunifu.. Hivyo tunaiga ili tupate kwenda mbele hatua moja hivyo maendeleo tunayokusudia sii asili yetu kuwa nayo..
Sasa usipokubali kwamba yawezekana Umaskini na Ujinga wetu unatokana na laana inakuwaje unaamini kwamba Wayahudi walibarikiwa na Mungu.. Kama Wayahudi waliweza kupendelewa na Mungu kwa nini wasiwepo watu ambao Mungu hakuwapendelea!..
 
Jamani hizi historia mnafundishwa na nani?

Kuhusu mababu/mabibi zetu kuwa na elimu mpaka ya vyuo vikuu kabla ya ukoloni Nyani nimeshakupa hii rejea: A Historical Accounting of African Universities: Beyond Afropessimism | The Zeleza Post

Kuhusu utumwa Zakumi yaani tafiti zote za kina Prof. Abdul Sherrif na Walter Rodney bado hazitoshi kukuonesha kuna aina mbalimbali za utumwa na huo wa Bahari za Atlantiki na Hindi katika karne ya Ubepari wa Uchuuzi ulitumia mabavu (kuwachukua vijana wetu rijali na wenye nguvu ibura) zaidi ya ushirikiano na hao machifu?

Kha hivi kumbe ni kweli tatizo letu kuu ni kuwa hatujijui!
 
Kuna uwezekano kuwa wazungu ndio gundi ya taifa kule sauzi.

Hiyo ndio moja ya hoja kuu za Malima Bundara, kitabu chake kina mapicha kibao ya kuonesha kuwa pale ambapo kuna wazungu hapa Afrika ndio pako vizuri - naona unakubaliana naye kabisa kuwa hao ndio gundi ya maendeleo. Kama ni hivyo si tuwaite tu watutawale - tena Frantz Fanon alisema hakuna haja ya kuwaiga maana kama tunataka kuwa kama wao basi wao ndio vinara kwa kuwa wao hivyo tuwaite tu wafanya vyao!

"Emancipate yourself from mental slavery" - Robert Nesta (Bob) Marley
 
Jamani hizi historia mnafundishwa na nani?

Kuhusu mababu/mabibi zetu kuwa na elimu mpaka ya vyuo vikuu kabla ya ukoloni Nyani nimeshakupa hii rejea: A Historical Accounting of African Universities: Beyond Afropessimism | The Zeleza Post

Kuhusu utumwa Zakumi yaani tafiti zote za kina Prof. Abdul Sherrif na Walter Rodney bado hazitoshi kukuonesha kuna aina mbalimbali za utumwa na huo wa Bahari za Atlantiki na Hindi katika karne ya Ubepari wa Uchuuzi ulitumia mabavu (kuwachukua vijana wetu rijali na wenye nguvu ibura) zaidi ya ushirikiano na hao machifu?

Kha hivi kumbe ni kweli tatizo letu kuu ni kuwa hatujijui!

Sherrif na Rodney ni ma propagandist tu hao. Huwezi kuwa na vyuo vikuu enzi hizo halafu uka fall behind kama tulivyo sasa. Ona vya wenzetu, Oxford iko tokea sijui karne ya 11 lakini leo hii ni moja ya vyuo bora sana duniani. Same can be said about Harvard, Cambridge, etc....hivyo vya Afrika bado vipo?
 
Compareno,
Mkuu nadhani bado hujatuelewa vizuri kwa sababu unaonekana kuzipita alama za wakati tunaozungumzia..Kwa mfano hoja yako hapo juu iliyotangulia inaonyesha wazi hatupo ukurasa mmoja na nadhani MkamaP amekueleza vizuri sana kwa huo mfano wa mwanafunzi..Nami nasema huwezi kutaka mabadiliko ikiwa hujitambui kuwa hivyo ulivyo (una kasoro nyingi) kunakuponza kupata hayo maendeleo unayokusudia kuyapata..Leo hii mtu akiitwa mjinga au maskini wanasema ni tusi wakati lengo kubwa la Kitaifa ni kufuta Umaskini na Ujinga..Huoni kaa hapa tunajifunga wenyewe.. utachukia vipi kuitwa maskini na mjinga wakati unatambuwa kwamba ni mapungufu makubwa kitaifa tunayotakiwa kuyafanyia kazi!..hapa imani hiyo na utekelezaji wake hauwezi kuleta mabadiliko hata kidogo mkuu wangu...

Nashangaa umepata asante nyingi mpaka ya Nyani wakati hiyo hoja yako na Mkama iko tofauti kabisa na hoja ya Nyani japo mnadhani zinafanana. Hoja ya Nyani ambayo ndio naidadavua ni hoja ya 'essentialism' yaani 'hali isiyobadilika'. Haongelei kasoro ambazo zinaweza kurekebishwa ambazo wewe na Mkama mnaziongelea na mnataka tuzikubali ili tuweze kuzirekebisha. Nyani anaongelea kasoro za kudumu - irreperable/undoable essence/defects. Ukielewa hii tofauti basi utajua kwa nini hatuko ukurasa mmoja. Ukifuata hoja ya Nyani mpaka mwisho wa mantiki yake (its logical conclusion) basi utaishia na maelezo kama haya ya mzunguko (circular arguments):

Waafrika ni maskini kwa kuwa ndivyo walivyo kuwa maskini
Waafrika ni wavivu kwa kuwa ndivyo walivyo kuwa wavivu
Waafrika ni waoga kwa kuwa ni ndivyo walivyo kuwa waoga

Ukishafika kwenye hilo hitimisho la kimantiki (logical conclusion) la hoja ya Nyani basi maelezo ya kihistoria, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni yanakuwa hayawezi kutumika tena kuelezea kwa nini tumekuwa maskini,wavivu na waoga maana tayari hoja ya kinasaba ya Nyani imeshatoa jibu - ndivyo tulivyozaliwa, ndivyo tulivyokua na ndivyo tutakufa tukiwa maskini, wavivu na waoga maana hivyo ndivyo tulivyo kwa asili - umaskini, uvivu na uoga upo kwenye damu yetu!Sasa utabadili/utarekebisha nini hapo zaidi ya kusubiri kufa katika umaskini wako ewe mvivu na mwoga?

"I AM WHO I AM" - THE UNCHANGING ETERNAL GOD
 
Sherrif na Rodney ni ma propagandist tu hao. Huwezi kuwa na vyuo vikuu enzi hizo halafu uka fall behind kama tulivyo sasa. Ona vya wenzetu, Oxford iko tokea sijui karne ya 11 lakini leo hii ni moja ya vyuo bora sana duniani. Same can be said about Harvard, Cambridge, etc....hivyo vya Afrika bado vipo?

Kwa hiyo vyuo vilivyopitisha Viva za Digrii zao kuhusu hayo navyo ni Vyuo propagandist tu - kumbuka Rodney alisoma SOAS huko UK?

At last na wewe unapingana na facts. Of all the people! Kama hivyo vyuo havipo jiulize kwa nini havipo - jiulize nini kilitokea. Anza kwa kusoma historia ya jinsi Wagiriki/Wayunani walivyoiba makabrasha ya kile chuo cha Misri na kukichoma moto kwenye ule mji ambao waliamua kuupa jina la Jemedari wao Mkuu Megas Alexander. Kisha soma jinsi na makabrasha ya chuo cha Timbuktu yalivyovurugwa. Na pia soma kuhusu ya hapo Kilwa.
 
Wewe nani alikufundisha historia? Dkt.Mishambi? Dkt.Mlahagwa? Prof. Kaijage? Au...?
 
Jmushi1:

Mimi ni mtu very experimental. Evolution and Intelligent design, vyote vina-point out kuwa kuwa asili ya binadamu ni moja. Kama asili ni moja ni kitu gani kilichobadilisha au kudumaza uwezo wa kundi fulani la watu. Na kitu gani kilichoboroshe kundi jingine. Je ni mazingira? Baraka za Mungu? Bahati? au kitu gani?

Kwa upande wangu mimi, kuna sababu nyingi za kudumaza maendeleo yetu. Lakini sababu zingine zikiendelea kwa muda mrefu hazi-make sense at all.

Tunaposema yamedumaa kwa sababu tulitawaliwa. Ni lazima tujiulize je tusingetawaliwa maendeleo yangetokea? Hivyo nina-rule out kutawaliwa kama ni chanzo cha kudumaa kwa maendeleo yetu. Vilevile nina-rule out utumwa. Vilevile nina-rule out vita vya Uganda na kuvunjika kwa jumuia ya EA.

So far, my favourite execuse ni mazingira kwa sababu ninaweza ku-point ABC za kwanini sisi tuko nyuma. Pamoja na hii kuwa my favourite, bado nina swali linalonisumbua. Je mtu akitokea na kuweza kutuboreshea mazingira yetu, tunaweza kuwa wabunifu?

Point za Ngabu nazikubali kwa shingo upande kwa sababu data zipo upande wake. Nchi zote za kiAfrika hakuna zinazofanya vizuri na hii sio coincidency ni pattern.

Tukirudi kwenye mada, kama mambo yetu ni pattern, je itasaidia kuwa na nadharia mpya kama Ujamaa mamboleo?

Kuna mtu anaitwa Diamond Jared, ana nadharia yake ya kijiografia/kimazingira (nadhani inafanana kiasi na ya Hegel) inayodai kuwa hali ya hewa ndio imetufanya tuachwe nyuma - hicho kitabu chake chenye nadharia hiyo kinaitwa 'Guns, Germs and Steel', mcheki/kicheki kwenye tovuti hii: Edge: JARED DIAMOND
 
Kuna mtu anaitwa Diamond Jared, ana nadharia yake ya kijiografia/kimazingira (nadhani inafanana kiasi na ya Hegel) inayodai kuwa hali ya hewa ndio imetufanya tuachwe nyuma - hicho kitabu chake cheny nadharia hiyo kinaitwa 'Guns, Germs and Steel', mcheki/kicheki kwenye tovuti hii: Edge: JARED DIAMOND

Visingizio visingizio viiiiiingi....
 
Wewe nani alikufundisha historia? Dkt.Mishambi? Dkt.Mlahagwa? Prof. Kaijage? Au...?

Mababu na mabibi zangu ambao walifundishwa na mababu na mabibi zao ambao nao walifundwa na mababu na mabibi zao ad infinitum...
 
Visingizio visingizio viiiiiingi....

Umewahi kujiuliza kwa nini leo hatuoni nyani wakibadilika kuwa binadamu? Wana kisingizio gani cha kutobadilika sasa wawe binadamu walioendelea? Au ndio walivyo - manyani wenye unyani? Je, nyani ni nyani tu hata umvike nguo za binadamu?
 
Nashangaa umepata asante nyingi mpaka ya Nyani wakati hiyo hoja yako na Mkama iko tofauti kabisa na hoja ya Nyani japo mnadhani zinafanana. Hoja ya Nyani ambayo ndio naidadavua ni hoja ya 'essentialism' yaani 'hali isiyobadilika'. Haongelei kasoro ambazo zinaweza kurekebishwa ambazo wewe na Mkama mnaziongelea na mnataka tuzikubali ili tuweze kuzirekebisha. Nyani anaongelea kasoro za kudumu - irreperable/undoable essence/defects. Ukielewa hii tofauti basi utajua kwa nini hatuko ukurasa mmoja. Ukifuata hoja ya Nyani mpaka mwisho wa mantiki yake (its logical conclusion) basi utaishia na maelezo kama haya ya mzunguko (circular arguments):

Waafrika ni maskini kwa kuwa ndivyo walivyo kuwa maskini
Waafrika ni wavivu kwa kuwa ndivyo walivyo kuwa wavivu
Waafrika ni waoga kwa kuwa ni ndivyo walivyo kuwa waoga

Ukishafika kwenye hilo hitimisho la kimantiki (logical conclusion) la hoja ya Nyani basi maelezo ya kihistoria, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni yanakuwa hayawezi kutumika tena kuelezea kwa nini tumekuwa maskini,wavivu na waoga maana tayari hoja ya kinasaba ya Nyani imeshatoa jibu - ndivyo tulivyozaliwa, ndivyo tulivyokua na ndivyo tutakufa tukiwa maskini, wavivu na waoga maana hivyo ndivyo tulivyo kwa asili - umaskini, uvivu na uoga upo kwenye damu yetu!Sasa utabadili/utarekebisha nini hapo zaidi ya kusubiri kufa katika umaskini wako ewe mvivu na mwoga?

"I AM WHO I AM" - THE UNCHANGING ETERNAL GOD

Umetafsiri vibaya hoja yangu ambayo inaacha nafasi ya kukubali mabadiliko endapo yatatokea na ndio maana huwa mara kwa mara nasisitiza kwa kusema "hadi hapo mtakaponithibitishia vinginevyo". Lakini hadi hivi sasa sijaona dalili zozote za kubadilika ndio maana hoja yangu bado inasimama.
 
Uzuri wa JF facts zipo zimehifadhiwa, hivyo kabla hujaifuta ngoja nikaiwahi na niinukuu humu ile posti yako unayosema kuwa hivyo ndivyo tulivyo sasa tutabadilikaje ilhali ndivyo tulivyo!
 
Umewahi kujiuliza kwa nini leo hatuoni nyani wakibadilika kuwa binadamu? Wana kisingizio gani cha kutobadilika sasa wawe binadamu walioendelea? Au ndio walivyo - manyani wenye unyani? Je, nyani ni nyani tu hata umvike nguo za binadamu?

Kisingizio kinachotolewa na hao watu wanaonunua hiyo nadharia ya evolution ni kwamba eti inachukua miaka mamilioni kwa manyani kubadilika ndio maana inakuwa vigumu kwetu sisi binadamu kushuhudia mabadiliko hayo.

I don't buy that evolution crap! Na kujibu swali lako, ndio nyani ni nyani tu hata umpake wanja!
 
Uzuri wa JF facts zipo zimehifadhiwa, hivyo kabla hujaifuta ngoja nikawahi na niinukuu humu ile posti yako unayosema kuwa hivyo ndivyo tulivyo sasa tutabadilikaje ilhali ndivyo tulivyo!

Nina mabandiko mengi sana yanayohusu hii mada sasa inategemea ni ipi utakayochagua kuinukuu na ipi utakayochagua kuiacha. The choice is yours.
 
Kisingizio kinachotolewa na hao watu wanaonunua hiyo nadharia ya evolution ni kwamba eti inachukua miaka mamilioni kwa manyani kubadilika ndio maana inakuwa vigumu kwetu sisi binadamu kushuhudia mabadiliko hayo.

I don't buy that evolution crap! Na kujibu swali lako, ndio nyani ni nyani tu hata umpake wanja!

Na mwafrika ni mwafrika tu mwenye tabia za kiafrika tu hata umvike uzungu na kumfunda tabia za wazungu?
 
Na mwafrika ni mwafrika tu mwenye tabia za kiafrika tu hata umvike uzungu na kumfunda tabia za wazungu?

Tabia za kizungu ndio zikoje hizo? Toa mifano ndio nitakupa jibu la uhakika

Unless unawazungumzia akina dada wanaojichubua ili wawe weupe kama wazungu na kuchoma nywele zao ili zinyooke kama za wazungu....
 
Back
Top Bottom