Kuelekea Ujamaa Mamboleo - Toward Neo-Socialism

Mwafrika hawezi kukomboka. Kama angekuwa anaweza angekuwa keshakomboka zamani za kale. Au wewe mfuasi wa Ujamaa unadhani ni lini Mwafrika atakomboka?

Saa ya Ukombozi ni Sasa - Usiniulize Nani Mwanzilishi wa 'Falsafa' Hii ya Kukomboka!
 
Nyani Ngabu, Companero na Zakumi
Mkuu nimekuwa nikifuatilia sana hii mada kwa ukaribu sana na hakika nimepata somo zuri tu...
Isipokuwa tukiondoka ktk vitabu na kurudi ktk hali halisi nadhani maneno ya mkuu Ngabu yana uzito mkubwa zaidi kupita elimu zote za dunia hii - Miafrika Ndivyo Tulivyo haiwezi kuondoka kwa itikadi wala uchawi isipokuwa ndivyo tulivyo na tukubali kuwa ndivyo tulivyo..

Nasema hivi kwa kutazama tulikotoka. Ni sisi waafrika tuliodai Uhuru wetu tukaeleza mazuri yote yatokanayo na Uhuru huo, tena basi waasisi wote wa uhuru wa nchi za Kiafrika wameishi Ulaya na kusoma vyuo vikuu miaka hiyo ya 50 na 60 kiasi kwamba revolution ya Ulaya ilikuwa somo kubwa kwao.. Lakini tazama matokeo ya Uhuru huo kwa Mwafirka..Kila nchi ni Maskini hata kama walikuwa Wajamaa, Mabepari au Asilia kina Bokasa naKing Mswati..

Kifupi sioni itikadi, mrengo wala babu yake kuja mkomboa mtu mweusi unless sisi wenyewe tukubali kuwa ndivyo tulivyo na tuanze upya tena kwa roho mbaya kama Wairan..Kila kiongozi wa Kiafrika anapoingia madarakani anataka kuwa King James..zile nadharia za karne ya kwanza hadi ya 17 ndizo zinatumika ktk uongozi wa nchi zote za kiafrika isipokuwa kilichobadilika ni mazingira..

Ukisoma historia ya nchi za Ulaya enzi za falme na nguvu zao kiutajiri ndizo tunazoziona Afrika leo.. Nasaba, kabila, dini, rangi na tofauti zote baina yetu ndizo zinajenga hoja ya maendeleo ya kila mmoja wetu..Nina hakika kila rais wa nchi ya Kiafrika ni TAJIRI kuliko rais yeyote Ulaya, hata Kikwete anaweza kuwa tajiri mtoto ukilinganisha na baadhi marais wa nchi za Ulaya..He has to be..kwani falme zote za Ulaya ziliheshimika kutokana na nguvu ya Utajiri wao na Afrika kama wewe hukuwa tajiri basi wee hufai...

Hii ndiyo Afrika ya leo, Ufisadi na tawala za Kifalme zinazojipa jina jipya la Rais wakati kila rais wa Afrika ni Royal familiy siku hizi, yaani familia ya Mkapa ina nguvu za kutisha kama Mkoloni kuliko familia ya Mangi Sina wa Kibosho kama ipo bado..

Kwa hiyo kilichobadilika ni kutoka mdomoni mwa Mkoloni (Malkia) kuingia kwa mtu mweusi tena basi afadhali wakati wa Queen tulikuwa tunamchangia mfuko wake kwa kodi zetu na ilijulikana ngapi anachukua kila mwaka kuliko watawala wa Kiafrika waovyotumaliza...Hawana hata aibu erbu tazama huyo Bongo wa Gabon kafa tajiri kuliko nchi yake...

Jamani tukubali tu yaishe, kuwa sisi Ndivyo Tulivyo..tupo hapa JF miaka mingapi? je kuna changes zozote zinazoashiria mabadiliko ya mbinu za kiutawala Tanzania..Je, Ujamaa au Ubepari utaweza vipi kufanya kazi ikiwa kiini cha fikra hizo hatuna.. na ukweli unabakia hatufahamu hata tunachokitaka zaidi ya UTAJIRI.. all we pray for, is Tanzania to become one the richest countries in the world...na uikitangaza malengo hayo uta win kura zote hata kama wananchi hawajui utawafikisha vipi huko!
Bottomline, Ndivyo tulivyo!
 
Unaanza kutoka nje ya mada sasa. Sijui ni maboksi au nini....

Kwikwikwi Maboksi mkuu. Najua tu, unataka tubaki kwenye mada ili u-prove points M.N.T (Miafrika Ndivyo Tulivyo!).

Anyway, mimi sina kisingizio cha utumwa, ukoloni au siasa. Kisiasa huwa natoa lawama kwa babu Nyerere kwa sababu ya kiitikadi tu lakini kiujumla hata kama nchi yetu ingekuwa na kiongozi mahiri anayejua ABC za ubepari, matokeo yangekuwa mabaya tu.

Hivyo nimebakiza visingizio viwili tu. Cha mazingira na cha baraka za Mungu.
 
'Nyani' - rejea matumizi ya ' ' katika neno ujijibu swali lako la kukomboka nako kuwa 'falsafa'!

Mkanda - rejea historia ya Waafrika/Weusi toka enzi za Axum na Kemet utueleze lini tulianza 'kuwa tulivyo'!

Zaku - rejea kazi yako ya maboksi kwenye hayo mazingira ya hizo 'dali' za kuyabebea utueleweshe 'nadharia' yako ya 'motisha'!
 
Tukubalini kwanza ndivyo tulivyo, hiyo itakuwa moja ya hatua kubwa mno na ya msingi ktk ujenzi wa uchumi endelevu.
 
Tukubalini kwanza ndivyo tulivyo, hiyo itakuwa moja ya hatua kubwa mno na ya msingi ktk ujenzi wa uchumi endelevu.

Huwezi kuwa 'ndivyo ulivyo' ukategemea kujiletea maendeleo maana maendeleo ni kubadili jinsi ulivyo sasa utajibadilije na ilhali hivyo ndivyo ulivyo? 'Muanzilishi' wa falsafa hiyo humu JF anaitumia hiyo lojiki kuonesha kuwa hakuna haja ya kuhangaika kuleta uchumi endelevu n.k. maana kuwa uchumi duni ndio jinsi tulivyo. Kwa lugha nyingine, maadam hivi ndivyo tulivyo basi angalau tuwaite wengine ambao sivyo walivyo ili watusaidie kutuletea maendeleo ikibidi kwa viboko kama alivyofanya Jerumani!

Tena waumini wa 'falsafa' hii ya kinasaba wananukuu mpaka Biblia inayosema Je Muithiopia anaweza kujibadili ngozi yake au chui kubadili madoa yake. Hivyo wanataka tupate masihi wa kuweza kuja kutuokoa na huo 'ufungwa' wa hulka, tabia na utamaduni wetu ambao 'ndivyo ulivyo'!

It is an essentialist's fatalistic argument - it only lead one to a cul-de-sac, that is, a dead end!

But the 'founder' of 'Classical Ujamaa' reminds us that "the choice is not between change or no change; the choice for Africa is between changing or being changed - changing our lives under our own direction, or being changed by the impact of forces outside our control"!
 
Mkuu
Ndivyo tulivyo, naomba nitoe mifano lakini uichukulie mifano huru na wala usikwazike kwa hiyo mifano.

Mtu alivyo mara zote hawezi kukubali kama yeye ni ndivyo alivyo na kutokubali kwake kuwa ndivyo alivyo kutamchukuwa miaka mingi sana ama karne na karne ama kusitokee kabisa maana anaamini yupo ktk mstari sahihi.

Binadamu anayetambuwa udhaifu na kuukubali udhaifu wake mara nyingi huwa mtu mwenye mafanikio ktk nyenendo zake.

Mwanafunzi mjinga huwa hajitambui kuwa ndivyo alivyo na kinachomsituwa ni MTIHANI baada ya kufeli mara kadhaa,na mwanafunzi anayetambuwa kuwa ndivyo alivyo huwafuata wkongwe na walimu wake ili wampatie njia mbadala na aweze kufaulu.Lakini yule ambaye ndivyo alivyo anapoamuwa kuyakataa matokeo na kutoa visingizio kibao mara kaonewa mara madarasa machache ,mara mwalimu anamwonea huyu huwa hajatambuwa kuwa ndivyo alivyo na mwisho wake ni mbaya zaidi.

Waafrika tumefeili mitihani miaka mingi sasa toka uhuru hadi leo tatizo ni ndivyo tulivyo tulikubali tatizo na tujaribu kulitatua kuendelea kujiaminisha sivyo tulivyo kunatupeleka shimoni,SASA nimeanza kuamini kwa kiasi fulani wasingelikuja wakoloni tungekuwa nyuma sana wenda bado tungekuwa tunakula mizizi.
 
Bravo bravismo my broda
 
Bravo bravismo my broda

Broda NN, swali lifuatalo katika variation mbalimbali tumeshaulizana mara kibao:

Huwezi kuwa 'ndivyo ulivyo' ukategemea kujiletea maendeleo maana maendeleo ni kubadili jinsi ulivyo sasa utajibadilije na ilhali hivyo ndivyo ulivyo? 'Muanzilishi' wa falsafa hiyo humu JF anaitumia hiyo lojiki kuonesha kuwa hakuna haja ya kuhangaika kuleta uchumi endelevu n.k. maana kuwa uchumi duni ndio jinsi tulivyo.

Unaijibu vipi hii hoja iliyoulizwa na Companero hapo juu?
 
Compareno,
Mkuu nadhani bado hujatuelewa vizuri kwa sababu unaonekana kuzipita alama za wakati tunaozungumzia..
Kwa mfano hoja yako hapo juu iliyotangulia inaonyesha wazi hatupo ukurasa mmoja na nadhani MkamaP amekueleza vizuri sana kwa huo mfano wa mwanafunzi..Nami nasema huwezi kutaka mabadiliko ikiwa hujitambui kuwa hivyo ulivyo (una kasoro nyingi) kunakuponza kupata hayo maendeleo unayokusudia kuyapata..Leo hii mtu akiitwa mjinga au maskini wanasema ni tusi wakati lengo kubwa la Kitaifa ni kufuta Umaskini na Ujinga..Huoni kaa hapa tunajifunga wenyewe.. utachukia vipi kuitwa maskini na mjinga wakati unatambuwa kwamba ni mapungufu makubwa kitaifa tunayotakiwa kuyafanyia kazi!..hapa imani hiyo na utekelezaji wake hauwezi kuleta mabadiliko hata kidogo mkuu wangu..

Huwezi kuanza kutafuta changes ikiwa huamini una kasoro fulani... na hapa tunazungumzia hizo kasoro.. wewe ukidai kuwa ni itikadi ambazo zinahitaji changes na sisi tunasema mbali na itikadi, tabia zetu sisi wenyewe ndicho kikwazo kikubwa na pengine yawezekana kutokana na elimu, maumbile, mazingira na hata uchovu wa kufikiria tukiwa maskini wa hali na mali.. hivyo itikadi yoyote ile haiwezi kufanya kazi ikiwa sisi wenyewe hatukubali kubadilika au kubadili mazingira yaliyopo kulingana na mfumo tunaotaka kuutumia..

Ni katika kutoelewa huko ndiko kulikomfanoa Zakumi na wengine wengi wasimwelewe Nyerere na wala wasipende mafundisho yake kwa sababu maendeleo kwa tafsiri ya wengi ni Utajiri.. maadam Nyerere alishindwa kutuletea Utajiri basi hana maana na itikadi zake. Tumebadilisha mfumo na kuiga ule unaotakiwa kwa fikra zetu bado Tanzania ni nchi maskini tena masikini zaidi ya wakati ule wa Mkoloni au Ujamaa. natumia kipimo cha nafasi (ranked position) ya Tanzania ktk nyakati zote..Leo tumesimama kati ya nchi 10 maskini duniani pamoja na utajiri wote tuliokuwa tumeukalia...

sasa nikirudi ktk enzi za Axum na Kemet, mkuu hapo utaona kwamba tulikuwa na tafsiri tofauti ya maendeleo ambayo hayakutokana na viwanda wala fedha isipokuwa falme ziliendelea kwa nguvu ya Majeshi na utajiri wa dhahabu, Watumwa na vito..Lakini utagundua kwamba sisi sote wazungu, wahindi, Waasia tulipitia hatua sawa za tawala tofauti kabla ya kufika hapa tulipo nao walikuwa na akina Alexander - The great na kadhalika..

Sote tulikuwa huru kwanza na tawala zetu za Kifalme..maendeleo ya kila falme yalipimwa tofauti na leo hii.. nadhani sina haja ya kwenda huko..Kisha nchi zote zikaingia awamu ya pili ya Uvamizi na kutawaliwa na wageni - Utumwa ktk ujenzi ukachukua nafasi kubwa ya maendeleo ya kila falme..Na nadhani bila shaka utajiri wa mtu ulihesabiwa kwa umilikaji wa watumwa wengi..Ukiwa na watumwa (mali) wengi basi wewe tajiri..

Misahafu yote inatuonyesha wazi jinsi mitume na falme walivyotumia watumwa ktk kupima utu wao. Na hata agano la kael linatuonyesha wazi jinsi watumwa walivyokuwa hawana haki hata mbele ya Mungu..Kwa mfano Wayahudi hawamtambui mwanamke mtumwa kuwa mke halali wa kizazi chao pamoja na kwamba ktk utukufu wote wa Abraham ni kizazi kimoja tu ndicho kimeweza kuwa na mama Myahudi..Ndio kusema kwamba leo hii hata watoto wa Nabii Musa (Moses) ambaye alioa mke, mtoto wa Phiraun hawana heshima ya Kiyahudi meaning They are not Jews..Hivyo tumetoka ktk Jews kuwa ni dini ya kuwabudu Mungu na kuifanya kama ni society inayotokana na kizazi cha mama Myahudi..Hii yote ni katika kukuonyesha jinsi utumwa ulivyokuwa kipimo cha Ndivyo Tulivyo..

Changes zilizofuata zilitokana na sisi kukubali Udhaifu huo na tukatafuta dawa yake.. Utumwa ukapigwa marufuku na tawala nyingi zilizokuwa na nguvu duniani zikaanza kudhoofika. Warumi, Wayunani, Wareno na Wahispania ambao walikua mataifa makubwa sana yalianguka vibaya kuliko hata Tanzania under Nyerere kwa sababu ujenzi wa maendeleo yao ulitokana na nguvu ya Watumwa..Hivyo mabadiliko yalitokana na kutambua athari za Utumwa..

Ni katika kukubali Utumwa na kutambua kwamba sii haki ya kibinadamu ndipo mabadiliko ya kweli yalipoweza kulenga ile hitlafu iliyopo ktk maendeleo ya jamii zote...hapo hapo nchi zote maskini bado zina watumwa wa ndani kwa malipo yasiyolingana kabisa na utu wa kumuita mfanyakazi..

Kwa hiyo utaona kwamba sote sisi tumepitia mifumo tofauti, toka tuwe huru, tukatawaliwa, tukaingia utumwani, tukajikomboa kuwa huru..Pengine tofauti kubwa kati yetu na wazungu ni kwamba wao walipojikomboa toka utumwani walirudi tena ktk tawala za Asili kabla ya kufanya mabadiliko mengine ya demokrasia.. Sisi tulitoka Utumwani, tukaingia kutawaliwa tena na Mkoloni kabla ya Uhuru wetu.
.
Sasa yawezekana hapo ndipo tulipopiga chini...Lakini pia nikitazama maneo ya MkamaP nikuta kuna mifano ya nchi ambazo zilipata Uhuru mapema zaidi..Nchi kama Ethiopia, Haiti, Chad hizi zote leo hii ndio top of the list ya nchi maskini... hivyo kuwa huru miaka mingi pia siii sababu..Then WHAT is holding us!...

Ndipo napokuja na hoja ya Ngabu, pengine NDIVYO TULIVYO ndicho kielelezo safi cha Ujinga na umaskini wetu, yaani sisi ni wajinga na maskini, we are bound to be poor! kama imani ya Hindu inavyofundisha..bila kutambua hivyo ya nini kupigana kuondoa Ujinga na umaskini ambao baadhi yetu hatukubali tunao?..
Kama sivyo, Je, kuna mtu anaweza kutueleza kinagaubaga kwa nini nchi zetu maskini bado pamoja na kwamba tuna Utajri mkubwa Unaotambulika leo ktk soko la bidhaa kuliko nchi zote duniani.. ELIMU ya darsa? sidhani mbona matajiri wengi duniani hawana elimu kubwa hata nchi kama Saudia, Kuwait, UAE, Brunai, Venezuela hawana kiwango kikubwa cha elimu hiyo lakini wameweza kuzitumia rasilimali walizokuwa nazo kupata maendeleo makubwa.. Sisi tuna excuse gani?
 
Broda NN, swali lifuatalo katika variation mbalimbali tumeshaulizana mara kibao:

Unaijibu vipi hii hoja iliyoulizwa na Companero hapo juu?

Hiyo hoja ya Komredi Companero ni dhaifu. Naijibu hivi hoja yake; kuna mambo mengi sana ambayo kwa imani yangu yako ndani ya uwezo wetu. Kwa mfano usafi wa mazingira. Huhitaji ku solve mahesabu ya trigonometry au calculus kuwa msafi na kuishi kwenye mazingira ya usafi. Sasa kata mbuga kuanzia Abuja hadi Soweto uone jinsi Miafrika tunavyoishi na uchafu. Umewahi babu kwenda pale Mwenge magengeni? Kunanuka. Sasa sehemu chafu kama Mwenge magengeni eti kinauzwa chakula kinacholiwa na binadamu. Kinachotushinda kupaweka pakawa pasafi ni nini? Hatuna pua za kunusa hiyo harufu mbaya inayotoka hapo magengeni? Hatuna macho ya kuona kuwa ni pachafu, pana mitaro ya maji machafu, nyanya zilizooza, n.k. Hatuna mikono na miguu ya kutumia kusafisha hilo eneo? Tatizo letu ni lipi hadi tuone kuwa ni kawaida kuzingirwa na uchafu huo?

Sasa huo uchafu wa Mwenge magangeni ni metaphor ya uchafu wa jamii nzima za kiafrika. Tuna mashida kibao. Kila siku tunalalama. Lakini hatufanyi chochote cha maana cha kuondokana na kero zinazotufanya tulalamike kila siku. Sasa hali kama hiyo utailezeaje ukaeleweka?

Mpaka leo hii karne ya 21 kuna wanafunzi wanakaa chini kwenye sakafu mashuleni kwa kukosa madawati. Kuna wagonjwa wanalala chini mahosptalini kwa kukosa vitanda. SteveD, hebu niambie ndugu yangu. Yaani hata kutengeneza madawati na vitanda tunashindwa? Miti ya mbao si tunayo? Mafundi seremala si tunao? Sasa kigumu ni kipi hapo kuhakikisha watoto wetu wanasoma ktk mazingira yaliyo bora na wagonjwa wetu kutibiwa ktk mazingira nafuu? How do you explain this and actually make sense?

Kama nilivyosema hapo juu. Kata mbuga kuanzia Abuja hadi Soweto au hata ughaibuni kwenye jamii za watu wenye asili ya Kiafrika. Utakuwa wao ndio wa mwisho ktk kila kitu. Hii haingii akilini kabisa. Kuna mtu katolea mfano Haiti. Supposedly walipata uhuru miaka 300 iliyopita. Okay, sasa inachukua muda kuendelea? Miaka mingine 300?

Sisi tuna miaka karibu 50 ya kuwa huru lakini hadi leo hii bado tunapeleka viongozi wetu kwenda kutibiwa kwa hao waliotutawala. What sense does that make my broda? Does it really make sense to you? What in the hell have we been doing in all those years? Dancing sindimba?

Tunaambiwa eti tu matajiri wa maliasili kibao. Sasa utajiri bila ujuzi na akili ya kugeuza hizo maliasili kwa manufaa yetu inasaidia nini. Let's trade places with Wazungus for 50 years and see what they will do that place?

Tumeanza kupewa misaada ya miradi ya maendeleo tokea uhuru lakini hadi hivi leo we have nothing to show for it! Tutaendelea kupokea misaada ya maendeleo bila kuendelea hadi lini? Miaka mingine 50?

If you can convincingly explain to me the cause of our misfortunes, misery, poverty and all that jazz, I will ditch the point of view that I currently hold and accept yours.
 
'Nyani' - rejea matumizi ya ' ' katika neno ujijibu swali lako la kukomboka nako kuwa 'falsafa'!

Mkanda - rejea historia ya Waafrika/Weusi toka enzi za Axum na Kemet utueleze lini tulianza 'kuwa tulivyo'!

Zaku - rejea kazi yako ya maboksi kwenye hayo mazingira ya hizo 'dali' za kuyabebea utueleweshe 'nadharia' yako ya 'motisha'!

Companero:

Wenzetu maendeleo yao yamekuja kwa evolution. Yaani wame-improve kitu kimoja baada ya kitu kingine kwa muda mrefu. Ubunifu kama NN anavyosema.

Kwa upande wetu kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za sisi ndivyo tulivyo, kubarikiwa, mazingira na mambo mengi, maendeleo yetu yatakuja kwa ku-engineer tu. Tatizo linalokuja ni jinsi gani tuta-engineer hayo maendeleo ukiangalia diverse challenges zinazotukabili.

Tukija kwenye incentives (Motisha), watu wengi wanafanya vitu kwa sababu. Na sababu hizi zikirudiwa kwa muda mrefu zinaweza kuzaa utamaduni.

Kwa mfano: Wakurya ni wabantu lakini wamecopy mila fulani za kimasai. Sources zangu zinaniambia kuwa wakurya walikuwa wafugaji waliotulia lakini kwa miaka fulani walikuwa attacked na masai raiders. Hili kujikinga na raiders, ilibidi wacopy baadhi ya mbinu za kijasiri za kimasai kama vile tohara, kutoboa masikio na mambo mengi.

Walifanya hivi kwa sababu kulikuwa na incentives ya kufanya hivyo na baadaye walijenga utamaduni.

Wajerumani wakati wanakuja Tanzania walichukua picha za wachagga. Ukiziangalia baadhi ya picha utaona baadhi ya wachagga walitoboa masikio na kubeba mikuki kama wamasai. Ni incentives za kazi wanazofanya wachagga zilizowafanya kufanya transformation katika kipindi cha muda mfupi.

Ninaamini kuwa kazi wanazofanya watanzania wengi nyumbani hazina incentives yoyote za kufanya watu wafanye transformation ya kimaisha. Watu wanaanza na kufanya kazi wakiwa na low expectations.
 
Ubunifu kama NN anavyosema.

Hizo sababu nyingine mimi naziona ni longolongo tu. Ubunifu ndio kiini cha maendeleo. Huu ubunifu una extend hadi kwenye sera, mipango, na zana za kuleta maendeleo. Watu kama hamko wabunifu, maendeleo mtayaona au kuyasikia kwa walio wabunifu tu. Haiwezekani kukwepa ubunifu katika maendeleo.
 
Kwikwikwi, unajua pride wakati mwingine inanifanya niwe mgumu ku-reconcile with facts.

Kuna posti nilikuwa namjibu Mkandara, nimehamua kutoi-post tu kwa sababu ina-contradict na nadharia yangu ya mazingira na incentives.
 
Yanaendana na ukweli kuwa binadamu wote wametokana na kizazi kimoja.

Hii ni nadharia tu ambayo haina uthibitisho wa kutosha kama ilivyo nadharia ya evolution.

Quote:
12n2_01.png

Hivyo basi level ya ubunifu kwa vizazi vya mwanzo vya binadamu ilikuwa sawa.​

Si kweli kwa sababu hata watoto wawili wenye wazazi sawa wanaweza kuwa na uwezo tofauti katika mambo tofauti.

Quote:
12n2_01.png

Na kama ilikuwa sawa basi wangeweza kusambaa na kuongezeka dunia proportionally kwa sababu walikuwa wana ubunifu wa kukabiliana na mazingira yao.

Kwa sababu haikuwa sawa ndio maana hayo hayakutokea

Quote:
12n2_01.png

Lakini kwa sababu hawakusambaa na kuongezeka proportionally, basi inawezekana maendeleo yao yalikuwa yanaathirika na mazingira yao au maendeleo yao yalitegemea nani kabalikiwa au kalaaniwa na Mungu.

Hapo kwenye nyekundu ndio kiini hasa cha umasikini wetu mtake msitake, mkubali msikubali
[/quote]

Nyani na Zakumi,hapo juu naona kuna mahali ambapo mmechanganya,pitieni upya mijadala yenu mtagundua hilo..Nyani ametolea mfano wa Zakumi hapo juu kwenye red light kwa kusema kuwa hayo ndo hasa kiini cha umasikini wetu tutake tusitake,tukubali tusikubali,yeye anaamini sisi miafrika ndivyo tulivyo kwasababu tumelaaniwa,kwa mana hiyo basi wewe Nyani unakubaliana kuwa asili yetu ni ya Uumbwaji yaani through Adam and Eve.
Hata hivyo Zakumi naye amejichanganya kwa kukubaliana na wewe na wakati msingi wake wa asili ya binadamu ilikuwa kama ana refer to common ancestors na ndio maana Nyani ukadai kuwa issue ya evolution hiana mantiki..So ni bora mkauendeleza mjadala inavyotakiwa na si tu kukubaliana na huku pointi zenu zinapishana.
 
Yanaendana na ukweli kuwa binadamu wote wametokana na kizazi kimoja.

Hii ni nadharia tu ambayo haina uthibitisho wa kutosha kama ilivyo nadharia ya evolution.

Quote:
12n2_01.png

Hivyo basi level ya ubunifu kwa vizazi vya mwanzo vya binadamu ilikuwa sawa.​

Si kweli kwa sababu hata watoto wawili wenye wazazi sawa wanaweza kuwa na uwezo tofauti katika mambo tofauti.

Quote:
12n2_01.png

Na kama ilikuwa sawa basi wangeweza kusambaa na kuongezeka dunia proportionally kwa sababu walikuwa wana ubunifu wa kukabiliana na mazingira yao.

Kwa sababu haikuwa sawa ndio maana hayo hayakutokea

Quote:
12n2_01.png

Lakini kwa sababu hawakusambaa na kuongezeka proportionally, basi inawezekana maendeleo yao yalikuwa yanaathirika na mazingira yao au maendeleo yao yalitegemea nani kabalikiwa au kalaaniwa na Mungu.

Hapo kwenye nyekundu ndio kiini hasa cha umasikini wetu mtake msitake, mkubali msikubali

Nyani na Zakumi,hapo juu naona kuna mahali ambapo mmechanganya,pitieni upya mijadala yenu mtagundua hilo..Nyani ametolea mfano wa Zakumi hapo juu kwenye red light kwa kusema kuwa hayo ndo hasa kiini cha umasikini wetu tutake tusitake,tukubali tusikubali,yeye anaamini sisi miafrika ndivyo tulivyo kwasababu tumelaaniwa,kwa mana hiyo basi wewe Nyani unakubaliana kuwa asili yetu ni ya Uumbwaji yaani through Adam and Eve.
Hata hivyo Zakumi naye amejichanganya kwa kukubaliana na wewe na wakati msingi wake wa asili ya binadamu ilikuwa kama ana refer to common ancestors na ndio maana Nyani ukadai kuwa issue ya evolution hiana mantiki..So ni bora mkauendeleza mjadala inavyotakiwa na si tu kukubaliana na huku pointi zenu zinapishana.[/QUOTE]

Zakumi ndio alikuwa anatoka nje ya mada...
 
Kwikwikwi, unajua pride wakati mwingine inanifanya niwe mgumu ku-reconcile with facts.

Kuna posti nilikuwa namjibu Mkandara, nimehamua kutoi-post tu kwa sababu ina-contradict na nadharia yangu ya mazingira na incentives.

Ahahahahahahaa....ni vigumu sana kupingana na facts babu. Na wengin wanaopinga kuwa Miafrika Ndivyo Tulivyo wanapinga tu kwa sababu ya pride na si kingine. Na wanapinga wakiwa majuu. Mimi nataka wapinge wakiwa kwa Mfuga Mbwa huku wakiwa wamezungukwa na dhiki, uchafu, takataka, mavumbi, joto, njaa, n.k.
 
..Leo hii mtu akiitwa mjinga au maskini wanasema ni tusi wakati lengo kubwa la Kitaifa ni kufuta Umaskini na Ujinga..Huoni kaa hapa tunajifunga wenyewe.. utachukia vipi kuitwa maskini na mjinga wakati unatambuwa kwamba ni mapungufu makubwa kitaifa tunayotakiwa kuyafanyia kazi!....

Duh!

Bob heshima mbele, hii kauli yako imebeba maana nzima ya kwa nini taifa letu haliendelei.

Masanja,
 
Back
Top Bottom