Bi. Asha Abdala,
Bibie unajua kuna watu kama sisi ambao kila kinachoandikwa hapa hukigeuza na kukitazama upande wa pili kabla hatujachagia kitu...
Sasa tuseme mimi binafsi sikubaliani na baadhi ya nafasi zilizotolewa hapo juu itakuwaje?..mathlan binafsi sioni kabisa sababu ya kuwa na Kambi ya Wazee ama Wanawake kisiasa, unless hilo la viti vya Wazee utaratibu wake umetokana na mila zetu za kiasili ambayo yanawapa wazee nguvu kubwa kuliko mwenyekiti wa chama (mfano ni maamuzi kuhusiana na Mh. Wangwe).
WHY nasema hivi:-
Kujenga tabaka za Wanawake na Wazee ndani ya chama ni moja ya kuongeza kongamano za kisiasa ndani ya chama ambazo zinatazama na kujenga kundi moja la maumbile ama umri ktk siasa ambazo hazina mtazamo wa makundi au mgawanyiko..
Unapoweka tabaka la Wanawake ni sawa na Muungano wa Tanzania ambapo Zanzibar (Wanawake) iinajulikana kama nchi lakini sii Bara (Wanaume)...na matokeo ya kuwepo mgao kama huu huleta matatizo makubwa kikatiba..Kwa nini wanawake kisiwe chama huru kama vile NGO inayojiendesha yenyewe in support of Chadema!.
Kipengele cha Vijana naweza kukubaliana nacho kwa sababu kinawaunganisha wanawake na wanaume kuwa kitu kimoja na madhumuni ya kuwepo kwake ni dhahiri, lakini hili la Wazee na Wanawake kuwa ndani ya katiba ya chama linanipa shida hasa kutokana na tamaduni zetu!
Mkandara,
Ukiwa na mawazo kama hayo ya kupinga status quo usije ukashangaa ukionyeshwa mlango wa kutokea na kuambiwa ni pandikizi.
Tanzania tunahitaji majadiliano makubwa juu ya hivu vyama vya siasa ambavyo vingi ni kama CCM tu ukiachia majina na rangi katika bendera zao.
Hata muundo wenyewe, kamati kuu, baraza kuu, mkutano mkuu nk. Kwa vyama ambavyo havina pesa za kutosha kuendesha mambo yake, je unahitaji urasimu wote huo?
Nguvu kubwa ya vyama inatakiwa iwe wilayani na sio makao makuu.
Kinachofanyika sasa ni kama ile sura ya Mkapa, juu kavimbiwa, vimiguu vyembamba, matokeo yake vina colapse kama lile jengo lililoanguka juzi. Kinachotakiwa ni kama Pyramid, chini kumejengeka vizuri na hivyo kufanya juu kuwe imara.