Elections 2010 Kuelekea uchaguzi: Jeshi lawatisha wananchi

Jeshi la Wananchi lipo nyuma ya harakati za Kikwete, ila hatima ya harakati zao ni kuipasua nchi vipande vipande, maana wako makamanda wanaoiunga mkono CHADEMA, waache wacheza na moto, waache wanasiasa wacheze siasa zao.
najua watu wanalinda vitumbua vyao, Tanzania haina viashiria vya uvunjifu amani ambavyo POLICE wameshindwa kutatua kiasi cha JWTZ KUONA HAJA YA KUTOA tAMKO. hatari iko mbele.

Ni huu ni mkakati maalumu wa kutaka wapinzani waonekane kama wachokozi, wachochezi.

Kama ulimwangalia yule kamanda wa JWTZ wakati anatoa lile onyo, alikuwa na ile gulity concious, alikuwa hawatazami wasikilizaji wake machoni. Ni pale tu alipokuwa anaongelea vyombo vya habari ndipo aliwatazama wasikilizaji. Vitu vya kizushi utavitambua tu, naamini yeye mwenyewe alijua na kuamini kuwa aliyokuwa anayasema hayakuwa ya kweli bali alikuwa anatumika na kikundi cha wanasiasa kuvuruga uchaguzi... WATASHINDWA!
 
Kwa vile Viongozi wa JWTZ wameamua kuingia katika siasa, basi tuwakaribishe, lakini inabidi watueleze mustakabali hasa wa nchi hii unakwendaje -- iwapo tunaeleke pema au pabaya.
Mimi nawaambia kwamba JK na CCM yake ndiye wanaipeleka nchi pabaya na ndiyo wastahili kukemewa kwa kutaka kuleta vurugu.

Nitatoa mfano mmoja tu: Kitendo cha JK kukumbatia na kuwasifia watuhumiwa wa ufisadi, hasa wale ambao kesi zao za ufisadi ziko mahakamani limeleta dharau kubwa kwa mahakama zetu -- na pia kuamsha hasira kubwa miongoni mwa wananchi hasa wale wenye kutambua sheria na haki ni vitu gani.Kamwe si kitendo cha utawala bora.

Wanachi hawa wana hasira sana kwa ukiukwaji mkubwa huu wa sheria. Karibuni jamvini.


Sisi watanzania kama tumelogwa vile........yaani kwa jinsi JK anavyosifia mafisadi, kina Lowasa na Rostam wala halikuwa suala la kuuliza, ilitakiwa civil societies zituongoze wananchi kwenye maandamano makubwa ya kushinikiza Kikwete ang'olewe kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi. Anavunja sheria hadharani....peupeee tena wakati wa uchaguzi kwa kuwa amejiandaa kuiba kura.

Kikwete anachotaka kutuambia kwa sifa hizi za kipuuzi ni kuwa hana tofauti na mafisadi bali yeye ni mmoja wao.....hata hivyo tukumbuke pesa za wizi na ufisadi na hao mafisadi wenyewe ndiyo waliomuweka madarakani.

IKO WAZI KABISA KUWA KUCHAGUA CCM NI KUMCHAGUA SHETANI ATAWALE MOYO WAKO, AGEUZE UBONGO WAKO MALIWATO NA ROHO YAKO AIMEZE UKIWA HAI. HAPO HATA RAIS AKISIFIA WABAKAJI NA WAUA ALBINO BADO ATAPIGIWA KURA YA NDIYO.

CCM NI TAKATAKA ZENYE KIPINDUPINDU.....2010 IWEKE KWENYE QUARANTINE KISHA FUTILIA MBALI!!!!

JK NI WA KUKWEPA KAMA UKOMA!!!!
 
kwanza nikushukuru mkuu kwa kuianzisha ishu hii.Binafsi nimeogopa sana kuskia jwtz wameingia katika kulisemea hili jambo la amani,nakumbuka ni mwenyekiti wa chadema aliyetoa tahadhari ya hatari ya kuvunjika kwa amani ENDAPO kutakuwa udanganyifu au wizi wa kura.
Mosi, nimeogopa kwa sababu nijuavyo mimi kazi ya JWTZ ni kulinda mipaka ya Nchi na inapobidi narudia kusema INAPOBIDI nikiwa na maana pale jeshi la polisi linaposhindwa ndipo jeshi letu hili linasaidia mambo ya ndani ya Nchi.
Kitendo cha JWTZ kutoa kauli ya Polisi naona lina ashiria mabaya zaidi kuliko hata usalama unaosisitizwa kwenye kauli
Yao.
La pili ni kwamba je wameichukuliaje kauli ya Mbowe nadhani ni vema wakaahidi kilinda kura vilevile maana hicho ndicho kilichotahadharishwa kinaweza kuleta vurugu.
Napenda kutoa wito kwa majeshi yetu WAWE TAYARI KUZUIA CHANZO CHA VURUGU ( Yaani uchakachuaji wa matokeo ) WASISUBIRI KUZIMA VURUGU ZITOKANAZO NA UCHAKACHUAJI HUO.
 
Shimbo kuna mfano wa thailand and wafilipino wananchi walipoamua kuchukua nchi yao kutoka kwa wahafidhina na mafisadi hawakujali Jeshi ,

Hesabu rahisi sana zinatuonyesha kuwa mkwara huo hausaidii. Tujiulize kwanza Hivyo wanajeshi na polisi ni wangapi?
Watanzania ni 40,000,000 plus, Shimbo wananchi wakiamua hutakuwa na jinsi ya kuwakatalia utashi wao wananchi wamewazidi mara 1000 hivyo uamuzi wa wananchi uheshimiwe.
 
Fige, nakubaliana na wewe. Mpaka leo sijamsikia saidi mwema akisema kuwa jeshi lake la polisi limeshindwa na hivyo wameomba JWTZ kuingilia kati. Pia jana nilitoa maoni kama ya kwako, wao wanapaswa kuionya CCM na jeshi lao la Green Guard pia kusimamia vilivyo kura ili zisiibiwe na uchaguzi uwe huru na haki. Basi maana katika nchi nyingi duniani ambapo kumetokea vurugu zimeanzishwa na vyama tawala baada ya kuchakachua kura na kulazimisha kubaki madarakani. Hicho ndicho chanzo cha vurugu. Kwa hiyo wasikimbilie kusema vurugu kabla ya kushughulikia kinachoweza kusababisha vurugu. Finished
 
jk amemtumia huyu jamaa std seven kujaribu karata yake ya mwisho. Kiheshi CDF ndiye msemaji wa jeshi. tunategemea aje kukanusha kuwa Shimbo hakuongea kwa niaba ya Jeshi.
 
October 2, 2010

'LIVE' DR SLAA AMPA MTIHANI SHIMBO WA JWTZ ,ASEMA CCM IMEPANGA KUCHAKACHUA KURA


HABARI KWA MSAADA WA FRANCIS GODWIN BLOG


Helkopta ya mgombea urais wa Chadema Dr.Slaa ikitua katika uwanja wa mkutano asubuhi hii
Wananchi wa Njombe wakiipungia mikono Helkopata ya Dr Slaa
Dr Slaa akipokelewa na viongozi wa wilaya ya Njombe mara baada ya kuwasili dakika chache kuanzia sasa
Helkopta ya Mgombea Urais wa Chadema ikiwa hewani ikijiandaa kutua uwanja wa Mdete Njombe mjini

Mgombea urais kwa Chadema Dr Willbroad Slaa amemshukia mkuu wa Mnadhimu mkuu wa majeshi nchini Bw Shimbo kuwa ndani ya siku 10 awe amewakamata wale wote ambao wanatuhumiwa kumwaga damu na vinginevyo hatua itachukuliwa dhidi yake.

Pia Dr.Slaa amesema kuwa CCM imepanga kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu na ndio sababu ya kuanza kutumia vyombo vya habari vya umma ,majeshi na usalama wa Taifa kuweka kinga na kuwa kama CCM imepanga kuchakachua matokeo basi itachakachuliwa yenyewe .

Hata hivyo ameonya jeshi la Polisi kupitia wakuu wa polisi wilaya kuwa kama wanapewa taarifa na kuchanwa mabango ya wagombea bila kuchukua hatua ni mwanzo wa jeshi la polisi kuchochea vurugu na kuwa Chadema kamwe haitafanya fujo labda fujo zitoke CCM.

Dr.Slaa ambaye anaendelea na hutuba yake viwanja wa Mdete mjini Njombe anaema kuwa hatautamani Urais wa Tanzania kama damu ya watanzania itamwagika katika uchaguzi na kuwa Chadema imejipanga kulinda amani na kuwa Green gadi ya CCM ni mwanzo wa fujo katika uchaguzi agiza polisi kuwakamata
 
Nimekuta bandiko kwenye gazeti moja kuwa wakuu wa majeshi wamekutana na kutoa onyo.
Hivi hawa wakuu wa majeshi wameombwa na nani? Ni nani amewaambia kuwa kutakuwa na uvunjifu wa amani. Kwa nini wanaanza kujenga defence na kwa manufaa ya nani?
 
MAPINDUZI MAPINDUZI MAPINDUZI. JWTZ limepindua nchi, watz hawaitaki CCM na KJ, lakini wao wanasema atakaye mkataa JK kukiona cha moto. Kwa mwenendo wa kampeni zinazoendelea sasa ni dhahiri kuwa wananchi wameamua kuipumzisha CCM kwa njia ya amani, lakini mafisadi hawataki kuheshimu matakwa ya wananchi hivyo wameamua kutumia JWTZ kulazimisha watz wakubali matokeo yaliyochakachukuliwa ili kulinda mafisadi.
 
Huyu Shimbo naona kwenye bandiko hili ameitwa "Mnajimu", lakini cheo chake kwa usahihi ni "Mnadhimu Mkuu" wa JWTZ.

Pamoja na hayo, kwa tabia aliyoionyesha jana, hafai kuitwa 'Mnadhimu" bali "Mnajimu" kama alivyo Shehe Yahya. Nasema haya kwa sababu yeye amejuaje kuwa vurugu zitatokea kama siyo kuongozwa na unajimu wa Shehe Yahya?

Yeye angeongelea mambo ya Al Shabab kuliko uchaguzi. Amejivunjia heshima na kuanzia jana, mke wangu hatampigia saluti tena.
 
JWTZ nashangaa wameingiliaje hili bora hata ingekuwa polisi
Elimu inatakiwa itolewe kwa hawa watu jamani.
 
October 2, 2010

'LIVE' DR SLAA AMPA MTIHANI SHIMBO WA JWTZ ,ASEMA CCM IMEPANGA KUCHAKACHUA KURA


HABARI KWA MSAADA WA FRANCIS GODWIN BLOG


Helkopta ya mgombea urais wa Chadema Dr.Slaa ikitua katika uwanja wa mkutano asubuhi hii
Wananchi wa Njombe wakiipungia mikono Helkopata ya Dr Slaa
Dr Slaa akipokelewa na viongozi wa wilaya ya Njombe mara baada ya kuwasili dakika chache kuanzia sasa
Helkopta ya Mgombea Urais wa Chadema ikiwa hewani ikijiandaa kutua uwanja wa Mdete Njombe mjini

Mgombea urais kwa Chadema Dr Willbroad Slaa amemshukia mkuu wa mnajimu mkuu wa majeshi nchini Bw Shimbo kuwa ndani ya siku 10 awe amewakamata wale wote ambao wanatuhumiwa kumwaga damu na vinginevyo hatua itachukuliwa dhidi yake.

Pia Dr.Slaa amesema kuwa CCM imepanga kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu na ndio sababu ya kuanza kutumia vyombo vya habari vya umma ,majeshi na usalama wa Taifa kuweka kinga na kuwa kama CCM imepanga kuchakachua matokeo basi itachakachuliwa yenyewe .

Hata hivyo ameonya jeshi la Polisi kupitia wakuu wa polisi wilaya kuwa kama wanapewa taarifa na kuchanwa mabango ya wagombea bila kuchukua hatua ni mwanzo wa jeshi la polisi kuchochea vurugu na kuwa Chadema kamwe haitafanya fujo labda fujo zitoke CCM.

Dr.Slaa ambaye anaendelea na hutuba yake viwanja wa Mdete mjini Njombe anaema kuwa hatautamani Urais wa Tanzania kama damu ya watanzania itamwagika katika uchaguzi na kuwa Chadema imejipanga kulinda amani na kuwa Green gadi ya CCM ni mwanzo wa fujo katika uchaguzi agiza polisi kuwakamata
samahani , kaka kweli ni Mnadhimu
 
Mimi ni mmoja ya watu wanaowaheshimu sana wanajeshi maana kwa mda mrefu wamekuwa wakifanya kazi nzuri tena kimya kimya bila kupiga piga hivyo kelele.
Jana huyu Gen ameniacha hoi. Inawezekana ubovu tunaouona uko karibu katika kila sehemu umeshaingia mpaka eneo hili nyeti, jeshi. Ukiona Gen anatumia media kutafuta umaarufu ujue huyo general ni muflisi. Au huyu hakukulia kwenye maadili halisi ya JWTZ? Maana wengine hawa walikuwa JKT au Mgambo ndio hivyo tena.
 
Ahsante dk slaa. lkn sidhani watz wapo tayari kufanya vurugu.jee tufanye vurugu kwa manufaa ya nani?
lkn pia nalipongeza sana jeshi letu la polisi kutoa mismamo kama ule . kwani amani iliyopo tz inatakiwa ilinndwe
watz ni watu wa amani kabisa.
lkn pia chadema haina nguvu kisiasa nchini
ikifika 0ctober 31. mpe kikwete kura yako

Ukikosolewa utatishia kuondoka JF?
 
Jeshi limedhalilishwa heshima yake kwa kuingilia mambo ya Polisi, ambayo kwa hakika ni ya chini sana kwake!
 
Mtu akiwa na kiu ya maji atakunywa hata ya Kisima sawa na Mtu akiwa na njaa atakula chochote kijacho mbele yake.

Kwa vile CCM inategemea kura za mazoea na kulazimisha, ni dhahiri JWTZ kutoa vitisho kutawafanya wale wapiga kura za mazoea kuogopa kwenda kupiga kura wakihofu fujo kutokea. Ila wale wakereketwa wa mabadiliko watajitokeza bila hofu mana wana KIU na NJAA ya Mabadiliko. Hivyo naamini vitisho vya JWTZ na vyombo vya habari vinaweza kusaidia CHADEMA.

Wapenzi wa Chadema na Dr. Slaa ni wakereketwa na watu wenye uchu wa mabadiliko kwa gharama zozote. Hii imedhihirishwa na watu kujibeba wenyewe kwenda kumsikiliza kinyume na CCM wanaoshurutisha watu kuhudhuria mikutano yao. Hivyo hawa watajipeleka kupiga kura kwa sababu CCM haitakuwa na uwezo wa kuwapeleka watu kwenye vituo vya kupigia kura!
 
Vyovyote itakavyokuwa, hakuna atakayezuia mabadiliko kwa rangi yake au rangi ya mavazi yake. Hata hivyo nadhani post yako hii ungeiweka katika thread inayoendelea ya "Slaa amjibu Shimbo" ili mjadala uendelee kuliko kupost thread mpya.
 
Shimbo kwa kikwetu ni uchuro, huyu mjinga aache uchuro wake, JK lazima aanguke tuuuuu, Mungu ameshaingilia kati kilio cha mamilioni ya watz kimefika kwa MUNGU, hakuna awezaye kubadili mapenzi ya Mungu
 
Back
Top Bottom