Polonium210
Member
- Nov 24, 2011
- 58
- 39
Mfumo wa Urushaji wa Matangazo ya Television katika Mfumo wa Digitali si Mgeni hapa Tanzania. Matangazo ya Televisheni kwa mfumo wa Digtal yanatofautiana tu katika Namna Matangazo yanamfikia Mteja. Katika Mfumo wowote wa Mawasiliana, Taarifa zaweza kwa kutumia njia kuu tatu.
1. Cable ( Coaxial, Fibre Optics Cable, Copper n.)
2. Satelite ( Taarifa zinamfikia Mtumia kwa njia ya Satelite). Mitambo ya Kurushia Matangazo inakuwa imefungwa katika satelite na Mitambo hiyo huitwa kwa Lugha ya Kitaalam Transponder.
3. Terestrial: Katika Mfumo huu wa kurusha Mtanganazo, Taarifa zinarushwa kwa watumiaji kwa Kutumia Mitambo iliyoko hapa hapa Duniani namaanisha Ardhini.
Kulingana na namna Matangazo yanavyorushwa Technolojia Mbalimbali zimeibuliwa
1. DVB-C : Matangazo ya Digital kwa njia ya Cable
2. DVB-S: Matangazo ya Digitali kwa njia ya Satelite
3. DVB-T: Matangazo ya Digitali kwa Njia ya Mianara iliyoko Ardhini ( Ambako nataka Uzi huu Ujikite hapo)
1. Je Matangazo ya Digital ni Mageni hapa Tanzania?
Hapana, Matangazo ya Televisheni kwa Njia ya Digitali yamekuwepo Tanzania kwa Muda Mrefu. Watanzania wamekuwa wakipata Matangazo ya Televisheni kwa mfumo wa Digital kwa Njia ya Cable ( Cable TV) na Satelite.
2. Je ili kuona Matangazo ya Digitali ni Lazima utumie Ving'amuzi wa Star Times au Ting Peke yake?
Hapana. Matangazo ya Digitali yanakuwa katika Standard iitwayo DVB-T au DVB-T2 ( Digital Video Broadcasting over Terrestrial). Kwa Hiyo Mtu yeyote Mwenye King'amuzi chochote ( Si Lazima Agape au Startimes) ambacho ni DVB-T compliance anapaswa kuona zile channel za Bure kama Channel ten, ITV, TBC1, Agape) Ila ili uweze kuona Channel za Kulipia kama TBC2 au Agape 2 ni Lazima upate ving'amuzi husika.
Nakaribisha Mjadala wenye Siha na Maswali ambayo naamini kuna wana JF wataalamu watayajibu mimi nimeanza na hayo mawili ili kila Mmoja afahamu mfumo huu mpya na aweze kufaidika
Niite Polo