Kuelekea hukumu ya J.J Mnyika; nini kitarajiwe...?

Alfred Daud Pigangoma

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,826
966
Habari wanajamvi.

Zikiwa zimebaki saa 48 ili mahakama ya kazi ambayo ndo inaendesha kesi ya kupinga matokeo ya mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John J. Mnyika dhidi ya walalamikaji wake kutoka CCM wakiongozwa na Bi. H. Ng'umbi. Nini kitarajiwe kuonekana siku hiyo au ndo kama kawa ule walaka wetu kutoka pale katika jumba lililopo ukingoni mwa Bahari ya Hindi?

Ki ukweli kama ukifuatilia kesi hizi ni kama kamchezo ka MIZENGWE ya enzi zile za MAX (Kwa sasa ni marehemu) na ZEMBWELA (Ambaye naye kwa sasa ni mtangazaji wa EATV na EA-Redio). Yetu macho na maskio lolote lipo........
 
Daima tutarajie ushindi kwani tunaamini kama mahakama inatenda haki na kwa sababu hiyo mgombea wa CHADEMA asingeweza kusema uongo katika kampeni kwani yeye alikuwa anaomba kura kwa kuwa yeye hakuwa mbunge kabla lakini kwa upande wa CCM yule mama alitumia kila namna ya kujinadi ikiwemo rushwa hatimaye akashindwa na kitu kilichomnyima ushindi ni ile kashfa ya kuuza nyumba ya UWT na aliuza kweli so tutarajie ushindi ndugu!
 
Tuheshimu tu uhuru wa mahakama na tukubaliane na hukumu.
 
Tutarajie Chadema kumpoteza mbunge mahiri mjengoni.
.
"IT WAS GOD WHO CREATED MAN, MAN CREATED MONEY AND MONEY CRAETED MAD, MAD, UFISADI AND MADNESS".
 
Ni ngumu sana kwa ccm kushinda. Tunaamini sisi tuna MUNGU wao wanamtumia shetani!
 
Majaji nao ni wananchi, wazalendo wa nchi hii. Mchango wa Mh Mnyika Bungeni na kwingineko wanauona na kuusikia. Wanajua gharama za kumpoteza ni kubwa kuliko kumbakiza. Mahakama ni muhimili pekee ambao umebakiza angalau kaheshima na kuaminiwa kidogo. Sishawishi lakini tunaifahamu TANZANIA ilivyo. After all Mnyika hana madhara kama alivyokuwa Lema kwa mfano. Hana wafuasi sugu wala makundi ya watiifu wake.
 
WARAKA WA IKULU UTAAMUA MaTOKEO,WANANCHI TUKO NYUMA YA JJ MNYIKA HATA KAMA ATASHINDWA ATAENDELEA KUWA MBUNGE WETU DAIMA NA 2015 SIO MBALI TUTAAWAADABISHA TENA.CHADAEMA TUWE TAYARI KWA LOLOTE MKUU WA KAYA AKIAMUA AMEAMUA KAMA ALIVYOAMUA ARUSHA,SEGEREA NA HATA SINGIDA NA SASA ATAAMUA UBUNGO NA IGUNGA.

MKUU WA KAYA HAKI IKIOMBWA SANA HUDAIWA,USITUFIKISHE HUKO.
 
Baadhi ya hukumu za kesi za kupinga matokeo ya chaguzi mbali mbali ni handout toka Ikulu, mfano ile ya Arusha na Segerea.Kusema kweli mahakama zetu zimenajisika sana.
 
Namuomba Mungu huyo Jaji Upendo Msuya asishikwe na pepo la Kusikiliza amri kutoka Ikulu angalie mwenendo wa kesi yake na amue kwa dhamira ya taaluma yake ,kwa kuzingatia ukweli na haki na Mungu atamsimamia lakini pia isiwe kumkandamiza Mnyika lna kumvua ubunge

Mnyika Kweli, ni kijana anajituma kusimamia maslahi ya nchi yetu: Mnyika jipe moyo uwe tayari kwa lolote Mahakama za CCM hazitabiriki
 
Habari wanajamvi.

Zikiwa zimebaki saa 48 ili mahakama ya kazi ambayo ndo inaendesha kesi ya kupinga matokeo ya mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John J. Mnyika dhidi ya walalamikaji wake kutoka CCM wakiongozwa na Bi. H. Ng'umbi. Nini kitarajiwe kuonekana siku hiyo au ndo kama kawa ule walaka wetu kutoka pale katika jumba lililopo ukingoni mwa Bahari ya Hindi?

Ki ukweli kama ukifuatilia kesi hizi ni kama kamchezo ka MIZENGWE ya enzi zile za MAX (Kwa sasa ni marehemu) na ZEMBWELA (Ambaye naye kwa sasa ni mtangazaji wa EATV na EA-Redio). Yetu macho na maskio lolote lipo........
hebu fafanua kwa nini kesi ya kupinga matokeo ya ubunge iendeshwe na mahakama ya kazi na sio mahakama kuu kwa mujibu wa sheria??
 
Majaji nao ni wananchi, wazalendo wa nchi hii. Mchango wa Mh Mnyika Bungeni na kwingineko wanauona na kuusikia. Wanajua gharama za kumpoteza ni kubwa kuliko kumbakiza. Mahakama ni muhimili pekee ambao umebakiza angalau kaheshima na kuaminiwa kidogo. Sishawishi lakini tunaifahamu TANZANIA ilivyo. After all Mnyika hana madhara kama alivyokuwa Lema kwa mfano. Hana wafuasi sugu wala makundi ya watiifu wake.

Mi kweli kabisa
 
Tutarajie Chadema kumpoteza mbunge mahiri mjengoni.
.
"IT WAS GOD WHO CREATED MAN, MAN CREATED MONEY AND MONEY CRAETED MAD, MAD, UFISADI AND MADNESS".

kwa iyo God made man, man made money and money makes man mad! Ok . Ila hii keshi imekaa kizushi zushi. Ebu tusubiri maamuzi ya mahakama. In latin we say, In cauda venonum,that is in the tail there is poison!cdm wili politically show that we shall poison all parasites who raised rabbish in our good game of politics!
 
Sisi tunaumiza vichwa jukwaani juu ya hukumu yake wakati yupo busy anajiandaa na mkutano wa jmosi na M4C huko kusini mwa nchi.

hebu na sie tufikirie M4C itatuletea mwamko upi hapa bandari ya Salama yenye walalahoi kibao
 
Vyombo vyote vya dola nchini havistahili kuaminiwa katika lolote lile......hivyo chochote kinaweza kutokea katika hukumu hiyo.
 
Back
Top Bottom