Kuelekea baraza jipya "EVERYBODY MARK THESE WORDS"

Mu-sir

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
3,621
1,629
wakuu,
Nilikuwa na hizi information lakini nikawa natafuta uthibitisho kutoka kwa source zangu na nimehakikisha sasa namwaga hapa.
naomba tuanzie na Richmond je, mwajua kwanini maazimio yake hadi sasa hayatekelezeki? Tunafahamu kuwa mtekelezaji mzuri wa maazimio yale ya bunge ni mamlaka ya juu ambayo ni Rais lakini kwa sababu yeye mwenyewe ndiye source na mwenye ile business basi maazimio yale hadi leo ni ngumu kutekelezeka (recall huyu jamaa aliwahi kuwa waziri wa ile wizara kipindi cha mwinyi).
PILI:
Suala la Jairo je, maazimio ya bunge ameyatekeleza kwa kiasi gani? Kumbukeni pia bunge liliwahi kuitaka serikali kuvunja mkataba na TICTS lakini mpaka leo hakuna utekelezaji ni kwa sababu Rais hawajibiki ipasavyo kwa wananchi wake na sababu kubwa ni kuwa yeye mwenye huwa nyuma ya madudu mengine yanayofanywa na viongozi ndio maana alisema Jairo atapangiwa kazi nyingine na mpaka leo anadunda na usafiri wa serikali.
Hayo nilikuwa nataka kuweka base ya hoja yenyewe.
SASA KUELEKEA BARAZA JIPYA:
hizi information ni classified lakini sina jinsi naweka wazi japo mpangilio unaweza kuwa ovyo.

Hapa jamani tatizo sio hawa watendaji wakuu bali ni Mkulu mwenyewe kwa sababu kubwa ambayo ni kwamba yeye anafanya biashara kupitia migongo ya hawa watendaji wake wakuu. Suala la wizara ya miondombinu Nundu yuko right kwa sehemu kubwa lakini mkuu alimtumia Mfutakamba kwa ajili ya manufaa yake ndio maana mlisikia kibali cha kusafiri alikitoa ofisi ya juu na ni State house ndio maana Nundu alisema ule makataba ulikuwa na Interest ya 77% in turn lakini hakueleweka sasa hapa Nundu anaweza kutolewa kafara au naibu akapangiwa kazi nyingine.
Tukija kwa Maige utaona analalamika sana lakini wale wakurugenzi wanafanya madudu na hawachukuliwi hatua yoyote ni kwa sababu wako nyuma ya mgongo wake unafikiri kwanini Kamrani hachukuliwi hatua yoyote? Kiufupi huyu jamaa anfanya biashara na mkulu mwenyewe na an biashara zingine zaidi ya hizo pamoja na KUCHIMBA MADINI NDANI YA HIFADHI ZETU na KUUZA MAGARI YA WIZI KUTOKA NCHI ZA UGHAIBUNI lakini nobody says anything kwa sababu mawasiliano yake anafanya na mkulu ndio maana maofisa wa serikali wanaogopa kwenda kwake.
So, let me end up here today lakini hiyo ndiyo hali halisi kiufupi TUNA RAIS MFANYABIASHARA.

MY TAKE KWENYE BARAZA JIPYA:
Tusitegemee miujiza na wale watakaopigwa chini watapangiwa kazi zingine au hawatachukuliwa hatua zozote zile. Kuhusu watendaji wa wizara wanaweza kutolewa kwenye sehemu zao lakini hatua thabiti hazitachukuliwa kwa sababu kichosumbua nchi hii ni USHAHIDI.
Kumbukeni kuwa washauri wake wameshamshauri sana achukue hatua za kufumua pale palipo na amshaka kuanzia watendaji wabovu hadi mawaziri wao ila tatizo ni je, atamweka nani wa kufanya vile anavyotaka yeye akiwatoa hao waliopo? Ndio maana kumekuwa na kusitasita kutoa maamuzi magumu tunayoota mchana kwamba yatatokea lakini whatever happens itakuwa kiinimacho na mtasikia mengine in few years.
Najua mtauliza source ni my insider wa Ikulu na namwamini.
PIA KUMBUKENI.
kila wizara ambayo waziri na naibu wake wana misunderstanding jueni kuwa mmoja yuko anatekeleza matakwa ya mkulu wa kaya na
mwingine anafuata taratibu kitu ambacho kitawa cost hawa wanaofuata taratibu kuliko wale wanaom-save mkulu.

UPDATES
Wakuu maneno yangu mliya MARK vizuri? compare these words before baraza and what is happening now utakubali kuwa VASCO DA GAMMA wetu ni don't care. More to come as I get confirmation.
 
KAMRAN si ndiye kapewa EPZ yote ya bagamoyo kama muwekezaji?eti atajenga viwanda.sasa naunganisha dots na jk,maige
 
KAMRAN si ndiye kapewa EPZ yote ya bagamoyo kama muwekezaji?eti atajenga viwanda.sasa naunganisha dots na jk,maige

mkuu huyu jamaa nyumbani kwake asubuhu utakuta magari yamejaa uwani halfu jioni yameshauzwa yote na TRA anapeta tu kiufupi ni untouchable! So watu watashangilia baraza jipya wasijue nyuma ya pazia kuna mkulu mwenyewe anafanya great business kimya kimya na mpaka 2015 nchi inaweza kubaki bila kitu.
 
Eeeh Mungu wa mbinguni uirehemu nchi yangu Tanzania na viongozi wake

mkuu Mungu na asikie maombi yako lakini ujue problem ni inner circle na sio hawa wanaotolewa kafara kwa ajili yake.
 
mtu anayetafuta uraisi au kuingia ikulu kwa gharama yoyote hata kwa kununua wapiga kura ni wa kumuogopa kama ukoma. Ikulu ni mzigo mzito sana, ukiwa na lengo la kuhudumia wananchi utaligundua hili. Ikulu ni mahala patakatifu, na wala sio pango la wezi na wala rushwa.
Kiongozi safi halilii kwenda ikulu bali hupelekwa na uma wa watu wake. Sio anayepelekwa na kikundi kidogo cha watu kwa maslahi yao!
 
Sasa hii ya magari ya wizi si aibu? Ndo mana visafari haviishi. Sasa jumlisha na wawekezaji wanavyotetewa!
 
mkuu mu-sir ulichoandika ndicho nilichofikiria miaka yote,mfano wizi wa mabilioni ya bagamoyo ni ridhiwan aliyepiga akishirikiana na watendaji na ridhiwan=jk,..
 
mtu anayetafuta uraisi au kuingia ikulu kwa gharama yoyote hata kwa kununua wapiga kura ni wa kumuogopa kama ukoma. Ikulu ni mzigo mzito sana, ukiwa na lengo la kuhudumia wananchi utaligundua hili. Ikulu ni mahala patakatifu, na wala sio pango la wezi na wala rushwa.
Kiongozi safi halilii kwenda ikulu bali hupelekwa na uma wa watu wake. Sio anayepelekwa na kikundi kidogo cha watu kwa maslahi yao!

nakubaliana na wewe mkuu yule anayetumia gharama kubwa lazima azirudishe kwa njia yoyote ile.
 
mkuu mu-sir ulichoandika ndicho nilichofikiria miaka yote,mfano wizi wa mabilioni ya bagamoyo ni ridhiwan aliyepiga akishirikiana na watendaji na ridhiwan=jk,..

mkuu tena huyu jamaa kamaliza ardhi ya kule Lugoba eti anawapa wahindi ekari nyingi sana waanzishe quarry kumbe na yeye ana crusher yake pale kila jiwe linalopita pale pesa yake. It is likely huyu mkulu kila sehemu kashika yeye.
 
2taanza nae 2kishika nchi,kwanza ktk katiba mpya 2nawaondolea immunity afu ndo utaanza kusikia amekimbilia uhamishoni comoro kwa abdalah sambi na Brazil ktk shamba la maximo kwani ndo washkaji zake.time wil tel
 
Mwisho wa siku izo ela zote atapeleka wapi?
Ni ulafi ulopitiliza na ipo siku atakuja kujuta kwa nini alikuwa raisi wa JMT
Nyerere "IKULU NI MAHALA PATAKATIFU"
 
Mwisho wa siku izo ela zote atapeleka wapi?
Ni ulafi ulopitiliza na ipo siku atakuja kujuta kwa nini alikuwa raisi wa JMT
Nyerere "IKULU NI MAHALA PATAKATIFU"

mkuu Njowepo hata mtu awe na trillions ambazo akila kuanzia leo milioni moja kwa siku haridhiki tu na cha ajabu huyu mkulu hatuonei hata huruma kidogo anazidi ku drill down till he get ousted or retired!
 
Last edited by a moderator:
UFISADI NDANI YA TAIFA LETU: ENYI MA-TOMASO MSIOAMINI HATA ZA 'JIKONI KWAO HAWA JAMAA' - NANI KASEMA ETI SIKU HIZI SAMAKI HUANZA KUOZA KUANZIA MKIANI HAPA???

Ni nani asiyejua kwamba walalahoi wa nchi hii mali zetu zinahamishiwa uarabuni kwa kutumia kila wizara kama wakala wa UFISADI?

Wapi uliwahi kusikia eti waziri anamgomea rais kujiuzulu kwake licha ya KUBEMBELEZWA SAAAANA KUOKOA JAHAZI kimtindo jambo analoonelea kwamba binafsi hajanufaika nayo kama si kutuambia umma wa Tanzania kiaina kwamba 'MIE NILIIBA KWA MAELEKEZO NA FAIDA YAKE YEYE huyu bana halafu leo hii nisulubiwe mimi; HAKA SIJIUZULU KITU NG'O'!!

WaTanzania, kuna tatizo tena zito ajabu pale pale Magogoni kwenyewe hivyo hata waje Waziri Zitto Kabwe au Tundu Lissu chini ya kivuli cha mbuyu huu huu bado UFISADI utaendelea kupaa kwa kasi ile ile!!!

Machimbo ya Uranium hifadhini nani mwingine tena akafanye na kule Bukombe kama si wenye meno ndani ya nchi?? Taifa hili litaendelea kutafunwa na wenye meno huku wenye moyo wakiendelea kuduwazwa na kufanywa kuonekana tu mahayawani kila kukicha.

INAUMA SANA!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom