Kuelekea 2015, tuna kundi jipya la urais CCM - Kigwangalla

Hakuna cha Mwandyosa wala cha nani 2015 itakuwa kipigo tu. Labda ccm wawa format upya wananchi ili wasahau zile ahadi 99 za trillion 9.
 
mchambuzi umeshtukia Dr Magufuli anakua kwenye siasa sana ziku hizi..hizi ziara ziara za kichama huku na kule nakua na wasi wasi nae (kuhusu kugombea 2015 na vile vile uwezekano wa kua mwanasiasa kama wenzake badala ya mtendaji na technocrat)
 
Hakuna cha Mwandyosa wala cha nani 2015 itakuwa kipigo tu. Labda ccm wawa format upya wananchi ili wasahau zile ahadi 99 za trillion 9.

CCM haiwezi kupoteza uchaguzi ngazi ya urais (ceteris paribus), itapoteza tu majimbo mengi tena sana, lakini urais lazima tutapitia experience ile ile ya CUF zanzibar na hatimaye serikali ya umoja wa kitaifa, lakini hii ni iwapo tu chadema watakuwa consistent kwa miaka 10-15 ijayo. Kumbuka - kwa CCM ushindi ni ushindi - hata matokeo yakiwa CCM 50.1% versus Chadema 49.9%, huo ni ushindi. Vinginevyo mabadiliko yafanyike mapema juu ya hii kanuni.
 
mchambuzi umeshtukia Dr Magufuli anakua kwenye siasa sana ziku hizi..hizi ziara ziara za kichama huku na kule nakua na wasi wasi nae (kuhusu kugombea 2015 na vile vile uwezekano wa kua mwanasiasa kama wenzake badala ya mtendaji na technocrat)

Madaraka ni kilevi kama bia; ukisema unapita baa kupata moja ili uendelee na safari, ni vigumu kujizuia kuagiza bia ya pili, na pengine ya tatu na ya nne; hayo ndio mazingira ya magufuli sasahivi. He is tempted to run that extra mile katika maisha yake ya siasa.
 
mbona mnajadili watu badala ya kubadili masuala yanayoisibu nchi yetu!? Maana watu watapita masuala yataendele kuwapo . Great Thinkers jadilini Tanzania mnayoitaka ili hata raisi awe jiwe abanwe na Tanzania tunayoitaka abanwe
 
Hainihusu sana tena pale ntakapo ongelea loser party au chama mfu kama ccm chadema hata wakisimamisha jiwe ccm ikamsimamisha mtu bado hawatoki salama 2015 ivo hata wamsimamishe nani Hana interest na Mimi wala kizazi changu napita tuu
 
Last edited by a moderator:
CCM haiwezi kupoteza uchaguzi ngazi ya urais (ceteris paribus), itapoteza tu majimbo mengi tena sana, lakini urais lazima tutapitia experience ile ile ya CUF zanzibar na hatimaye serikali ya umoja wa kitaifa, lakini hii ni iwapo tu chadema watakuwa consistent kwa miaka 10-15 ijayo. Kumbuka - kwa CCM ushindi ni ushindi - hata matokeo yakiwa CCM 50.1% versus Chadema 49.9%, huo ni ushindi. Vinginevyo mabadiliko yafanyike mapema juu ya hii kanuni.

Itapoteza,na hautaamini! 'Mark my word bro'
 
Itapoteza,na hautaamini! 'Mark my word bro'

Sitajali CCM kupoteza kwani kama ilivyokuwa kwa Nyerere, CCM sio mama yangu, na isitoshe, itakuwa vizuri sana ikiwa CCM itakuwa chama cha upinzani kwa muda ili kwanza, kijifunze maana ya chama cha siasa katika siasa za ushindani ni nini, lakini muhimu zaidi, tuwe na vyama viwili vikubwa. Hoja yangu ya msingi ni kwamba ili hilo litokee, suala la kanuni ya ushindi lazima libadilishwe.
 
Lipo kundi jipya linalojiita lenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM linalo jipanga kwa kinyang'anyiro cha 2015.

Mohamed,
Binafsi nadhani kundi hili sio jipya, lipo na ni moja kati ya makundi mengine angalau sita:

1. Wapambanaji ufisadi.
2. Watuhumiwa ufisadi.
3. Wenye msimamo wa Mwalimu Nyerere.
4. Wazee wa busara (lile lililojaribu kupatanisha kundi la kwanza na la pili hapo juu).
5. Kundi hili tunalolijadili katika mada husika - yani lililokuwa karibu na regime ya sasa na linajaribu kujipenyeza for 2015.
6. Kundi la liwalo liwe - ambao hawafungamani na upande wowote - hawa ni mawaziri waandamizi wa awamu ya tatu na baadhi katika awamu hii.
7. Kundi linalojengwa na baadhi ya wale walioshindwa 2005.

Nimeyajadili haya kwa kirefu katika uzi wangu mwingine:

https://www.jamiiforums.com/great-t...urais-2015-tujadili-aina-kuu-za-wagombea.html
 
Jamani mbona jembe la jazba hamlitaji?Dr Pombe??au hafai kuwa Pres?anafaa kuwa PM?
 
Kwa faida ya mjadala huu naomba kumnukuu muandishi nguli na mhariri mahiri wa The Guardian kaka Richard Mghamba.
Kwenye mjadala husika nae amesema

"HK na wengine,
Chadema kwa sasa in a makundi ya hatari kuliko hata ya CCM tena ambayo yanajengwa kwa misingi ya ukanda na hata ukabila. Kila anayetaka kugombea nafasi ya juu katika chama, utasikia mizengwe ya hatari inaibuliwa wakati nilitaraji chama kama Chadema-kiruhusu demokrasia itawale na yule anayekubalika-anaibuka mshindi.....
Mbona unachanganya mada? Jibu hoja za wachaangiaji katika thread yako. Mbona unahama haraka.... Endelea na Kigwangalla
 
Back
Top Bottom