Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Wanabodi,

Baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Mkuu "Mstaafu", Edward Lowassa katika two- series za kipindi cha Kipima Joto cha ITV, kwanza nimekubali sana huyu jamaa!, pili kama yeye ndiye angekuwa rais, ile 2005, Tanzania tusingefikia hapa tulifikishwa sasa na utawala wa JK, ila kikubwa zaidi, (kama ni kweli afya yake sio mgogoro kama anavyodai yuko fit, japo he looks sick), CCM ikimsimamisha yeye kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, them matokeo ya urais kwa 2015, ni CCM tena!. Mkubali, mkatae!.

Hizi ni baadhi tuu ya sababu, kwanini CCM itashinda tena, endapo and only if itamsimamisha Lowassa!.

1. Uwezo wa Kupanga, Kusema, Kusimamia na Kutenda.
Viongozi karibu wote waliopo CCM, wana uwezo mkubwa sana kupanga wa kusema tuu, (Mkukuta, Mkumbita, Mkurabita, Mkuza, na sasa Dira 2025), lakini hawana uwezo wa kusimamia na kutenda!, mipango mingi iliyopangwa, inaishia kwenye maneno na vitendo sifuri!. Edward Lowassa sio msemaji, bali ni mtendaji, yeye sio mtu wa maneno mingi, ni mtu wa vitendo virefu, he is an action oriented man!.

Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Elimu, Umasikini na Maradhi, na tulijiwekea misingi yatu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile mising minne tulisahau capital!.

Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo la siasa safi na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Elimu ni adui, lakini we never invested because we had no capital. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana na IMF, WB etc matokeo tunayajua!.

Lowassa na timu yake ya Boys II Men, walipoingia tuu madarakani, akafanya study tour ya tulioanza nao kwanini wamefanikiwa, wako mbali na sisi wametuacha sana!, akagundua wali invest kwenye elimu!. Akarudi akahamasisha kila kata iwe na shule ya sekondari ili kila Mtanzania apate kwanza elimu, mengine yote, yatafuatia!.

Baada ya kujiuzulu, serikali ya JK ikazi abandon zile shule za EL ili kumkomoa!. Jana alipozungumzia umuhimu wa kuwaelimisha kwanza watu wetu, amenigusa sana!. Tungekuwa tumeelimika, tusingeibiwa hivi madini yetu, sasa tumegundua gesi,serikali inakimbilia kugawa vitalu kwa umiliki wa miaka 99 huku Watanzania hatuna hili wala lile kuhusu gesi, kwa kifupi, hutujui lolote na tutaishia kuibiwa tena!. EL ameshauri, lets invest kwenye elimu kwanza ili kuwa empower watu wetu ndipo tuingie kwenye ambitious projects kama za kilimo kwanza gesi etc!.

Kwa hili pekee, CCM ikimsimamisha EL, Tanzania itapata ukombozi wa kweli wa puli wa Mtanzania!.

Nimesema, CCM ikimsimamisha EL, 2015, itakuwa ni CCM tena, kwa sababu katika wapinzani wote, hakuna hata mgombea mmoja anayewa kusimama na Lowassa kwenye urais na bado akaambulia kura!, there is no one!.

Mwenye masikio na asikie!.

2. Dhambi Kubwa ya Lowassa ni Richmond Tuu!.

Najua wapinzani wa ukweli, watakuja na hoja za dhabi kubwa ya Lowassa ni Richmond, then time will tell, hiyo ni mizigo tuu ya watu, alijitolea kuibeba ili kwa kuteswa kwake, wao waokoke, wakati muafaka ukifika, hili litawekwa wazi na Watanzania mtawafahamu wenye zigo lao!. Wenye akili wameshang'amua ile metarmophosis process from Richmond -Dowans -Simbion na kwa msio jua, mkae mkijua Tanesco bado inailipo Simbiaon capacity charge ile ile ya dola 152 kama richmond na Dowans, hivyo tumeruka majivu na kukanya moto, tumerika maji na kukanyaga tope, na kwa usafi tumeruka nyasi, tukakanyaga ma..!.

3. CCM Haina zaidi ya EL na Upinzani hana wa Kushindana Nae!.

Wanabodi ni mimi niliwahi kusema, CCM imechokwa na Chadema Haijajipanga, baadae nikasema CCM imechokwa mpaka basi!, Baada ya Chadema kuanza kujipanga nikasema Chadema, Njia Nyeupe Ikulu, lakini sasa baada ya kumsikia Edward Lowassa, kama ni kweli CCM itamsimamisha, then, 2015, ni CCM tena, kinyume cha hapo, CCM ikimsimamisha mwingine yoyote, 2015, Chadema inachukuwa nchi kiulani kama kumsukuma mlevi!.

Mwisho.

Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM itaukubali huu ukweli mchungu wa kumsimamisha Lowassa ili kuweza kujiokoa?, itakubali kusubiria kifo cha mende huki inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji, kwa kutegemea katiba impya ita provide opportunities za aina ile ile ya miaka ya nyuma, kuwa ita endelea "to fool all people all times?!.

Asante.

Pasco.

NB. Japo Pasco wa JF sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa CCM ni Pro Lowassa, kwa Chadema ni Pro ZZK na kwa CUF ni Pro-Jussa!.

Kama una ushawishi kwa ccm basi washauri wamsimamishe
Hoja namba tatu ni kama unatania,lets wait and see!
 
Pasco unataka kutuaminisha kuwa tatizo kuu la nchi yetu ni kukosa kiongozi mmoja bora wa kutuongoza, hivyo Lowassa ni mtu bora wa kipekee wakuja kutuongoza vema!!

Umechelewa sana, hakuna namna ambayo unayoweza kuwashawishi wanatanzania wa leo ambao wanaendelea kuelimishwa na CHADEMA kwa kasi ya ajabu warudi nyuma wakakueelewa, labda baadhi ya WanaCCM mazezeta ndio watakuelewa.

Kama unabisha muulize vizuri Lowassa ni kwa nini ndugu zake wameru kule Arumeru mashariki waliamua kuikataa CCM mbele ya macho yake pamoja na kupewa hongo za kila namna?
 
....Edward Ngoyai Lowassa fisadi na mbadhirifu aliyekubuhu ndiye Rais wa Moyoni wa Pasco wa JF, ama kweli maisha ni kuchagua na hatuwezi kulingana, go Pasco go....
 
Kwani asiwe Eliakimu Maswi au Mwakyembe au Ezekiel Maige au mimi Ndahani Pasco. Naogopa suprise mwenzio....
 
Last edited by a moderator:
Huyu Lowassa atatuumizia akili za kaka yetu Pasco.

Lowassa, he will never be a President of this Republic hata akigombea na Jiwe ni uhakika kuwa Jiwe litashinda. Lowassa ni mmoja waliomo kwenye list of Shame, alitajwa na rais wetu Dr Slaa kuwa ni fisadi kama Kikwete alivyo, still no difference mwizi ni mwzi tu hata ukimpa manyoya ya kuku bado ataiba hata mavi ya kuku.

Pasco you real need help ASAP
 
Hakuna kazi ngumu kama kumkampenia EL, Pasco you are on MISSION IMPOSSIBLE

attachment.php
 
Attachments

  • Bounce back by Jacob Zuma.jpg
    Bounce back by Jacob Zuma.jpg
    21 KB · Views: 2,695
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

3. CCM Haina zaidi ya EL na Upinzani hana wa Kushindana Nae!.

Wanabodi ni mimi niliwahi kusema, CCM imechokwa na Chadema Haijajipanga, baadae nikasema CCM imechokwa mpaka basi!, Baada ya Chadema kuanza kujipanga nikasema Chadema, Njia Nyeupe Ikulu, lakini sasa baada ya kumsikia Edward Lowassa, kama ni kweli CCM itamsimamisha, then, 2015, ni CCM tena, kinyume cha hapo, CCM ikimsimamisha mwingine yoyote, 2015, Chadema inachukuwa nchi kiulani kama kumsukuma mlevi!.

Nakufananisha na mwanamke asiye na msimamo, maana namimi wa TLP ukinisikia vizuri siku moja utasema njia yangu ya kwenda Ikulu ni nyeupeee peee!!!!!
 
Pasco, umejitahidi kufanya analysis yenye ushawishi, lakini kuna baadhi ya mambo ambayo naona haukuyatilia maanani (sijui kwa ushabiki au ni oversight tu). Kwanza, kwa ujumla, shida ya tanzania sasa hivi sidhani kama ni mtu mzuri wa kuongoza. tatizo kubwa linbaloikabili Tanzania hivi sasa ni mifumoya kiongozi ambayo haifanyikazi vile inavyotakiwa. Labda suala hili ndilo linalotutias giza na kuanza kuwajadili watu badala ya issues kwa sababu lenyewe linahusiana na personality pia.
Lowassa au mtu mwingine anaweza kuonyesha quality za kiongozi mzuri lakini uongozi ni teamwork ambayo inapaswa kusaidiwa na mdumo mzuri. hapo yanaweza kuibuka matatizo mawili makubwa ambayo yanaweza kumfanya Lowassa ashindwe akishinda. Lwanza atakuwa na tiumu ya watu kutoka CCM ambako tayari kuna madonda makubwa na kpiga vita kwa hatari sana. Pili, huku akiwa na tiumu ambayo inatafunana ndani kwa ndani, atakumbana na mfumo ambao umegota kuanya kazi. Kwa kiasi kikubwa hata Kikwete ameshindwa kutokana na sababu hizimbili kuu.
Kwa hali ilivyohivi sasa CCMinapaswa kufa na kuzaliwa upya, na izaliwe mpya kweli, ikiachana na ya kale yote. Hili ni jambo ambalosidhani kama linaweza kutokea lenyewe na sioni uwezo wa Lowassa kulifanyahili litokee.
Lakini pia kwa kiasi fulani Lowassa ameonyesha dalili za kuendeleza malumbano ya kutafunana kwa sababu ajalikana kuwa nimtu wa visasi.
Mbaya zaidi, wakati wakiendelea kutafunana ndaniya CCM, huko nje Chadema, CUF na ADC nazo zitakuwa zikiendelea kuwatafuna. Unadhani Lowassa anaweza kweli kukabiliana na hali hii hasa ukizingatia wasi wasi wakokuwa afya yake inaweza kuwa na mushkeli?
 
Last edited by a moderator:
Hauko serious. Lowasa u-billionea wake ule unafikiri kapatia Richmond? Au unafikiri ni ali-save mshahara wake akawa bilionea wa kutisha? Uliza watu alifanya nini alipokuwa waziri pale wizara ya Ardhi. Kumbuka Nyerere alimkataa Lowasa kwamba hana ethics za uongozi KABLA ya hiyo Richmond. Kumbuka wahindi waliomwambia Lowasa ananuka rushwa KABLA ya hiyo Richmond. Yes, anajua sana kuongea na kupanga hoja, lakini hivi unamjua Lowasa wewe?

Ila Dr ndo ana ethics za uongozi kwa kutembea na mke wa mtu na kula michango ya kanisa.
 
Pasco, umejitahidi kufanya analysis yenye ushawishi, lakini kuna baadhi ya mambo ambayo naona haukuyatilia maanani (sijui kwa ushabiki au ni oversight tu). Kwanza, kwa ujumla, shida ya tanzania sasa hivi sidhani kama ni mtu mzuri wa kuongoza. tatizo kubwa linbaloikabili Tanzania hivi sasa ni mifumoya kiongozi ambayo haifanyikazi vile inavyotakiwa. Labda suala hili ndilo linalotutias giza na kuanza kuwajadili watu badala ya issues kwa sababu lenyewe linahusiana na personality pia.
Lowassa au mtu mwingine anaweza kuonyesha quality za kiongozi mzuri lakini uongozi ni teamwork ambayo inapaswa kusaidiwa na mdumo mzuri. hapo yanaweza kuibuka matatizo mawili makubwa ambayo yanaweza kumfanya Lowassa ashindwe akishinda. Lwanza atakuwa na tiumu ya watu kutoka CCM ambako tayari kuna madonda makubwa na kpiga vita kwa hatari sana. Pili, huku akiwa na tiumu ambayo inatafunana ndani kwa ndani, atakumbana na mfumo ambao umegota kuanya kazi. Kwa kiasi kikubwa hata Kikwete ameshindwa kutokana na sababu hizimbili kuu.
Kwa hali ilivyohivi sasa CCMinapaswa kufa na kuzaliwa upya, na izaliwe mpya kweli, ikiachana na ya kale yote. Hili ni jambo ambalosidhani kama linaweza kutokea lenyewe na sioni uwezo wa Lowassa kulifanyahili litokee.
Lakini pia kwa kiasi fulani Lowassa ameonyesha dalili za kuendeleza malumbano ya kutafunana kwa sababu ajalikana kuwa nimtu wa visasi.
Mbaya zaidi, wakati wakiendelea kutafunana ndaniya CCM, huko nje Chadema, CUF na ADC nazo zitakuwa zikiendelea kuwatafuna. Unadhani Lowassa anaweza kweli kukabiliana na hali hii hasa ukizingatia wasi wasi wakokuwa afya yake inaweza kuwa na mushkeli?

Ndio maana najiuliza kwanini awe yeye na siye mwingine yoyote? Maana CCM ina makundi mengi yenye nia ya kumtoa mgombea urais na sasa yanajipanga kuwa na ushawishi mkubwa kwa wapiga kura. Miaka mitatu si michache maana hata saa moja ni kubwa sana ndani ya mambo ya kisiasa.
 
Naamini hata kule Arumeru mashariki wengi walisema kama sio mkwewe Lowasa (Siyoi Sumari) basi ccm ingelipoteza Jimbo.

Kumbukumbu zangu kama dhaifu vile, kuwa huo wosia uliotolewa kwa ccm kumsimamisha mkwewe Lowasa haukuzingatiwa vile!

Ama kweli utamu upo wa aina nyingi, kwani hata pilipili ina utamu wake! Hongera Pasco kwa kukolewa na utamu!
 
Pasco na analysis zake nyepesi na zenye ufinyu wa kimtazamo hajambo. Umefungwa na nini kiasi kwamba you dont think of any other person except EL? amekupa nini? hebu jaribu kufikiria kama tunavyokufahamu. Achana na EL, sio mtaji mzuri. Utaukosa hata ukuu wa wilaya ukiendelea na tabia hii.
 
Pasco wa JF........Lowassa for president 2015.
Rais 2015 lazima atoke kaskazini.

:spy::spy::spy:

Mimi sikatai obsession ya Pasco kwa Lowassa, kila mtu anayo obsession yake at one point, it is natural. However, it become unnatural and a bit weird kama Mtu huyo anaelezewa kama man alone from a failed system. System ambayo haijaweza kufanya yale yaliyotarajiwa na wengi.

A system where, individuals ndani ya systems are biting each other, sabotaging each other, making deals with devils in and out of that same system.

An individual who was accused of getting across Procurement procedures, altering the process and causing a massive economical shake to the country, accepted the accusation as major and resigned - of-course while :A S cry:, who wouldn't.
Hata waziri wa uchukuzi wa Znz ali-resign juzi huku akinung'unika.

Ukikubali ku-resign, maana yake umekubali kosa. Issue ya kuthibitishwa mahakamani ni swala jingine kabisa. nani asiyejua kwamba kupelekwa mahakamani hapa Tz ni mapaka mkulu aamue?? Hata majizi yanaambiwa yarudishe fedha yazizokwiba.

Mkuu, huyu jamaa hasafishiki.....he has been around for a long long time.....amefanya nini?? usiongelee shule za kata kwasababu that is a disgrace to education system in Tanzania...what else?
 
Last edited by a moderator:
binafsi nimeona kma EL afya yake mgogoro kidogo, alikua anaongea kwa shda shda af design memory yke imekaa kushoto kdg........

reference nyingi za mambo aliyokua akijaribu kupambanua alikua hakumbuki...........

Kwa hiyo Pasco hakuiona hayo!!
 
Kwanza, Edward Lowassa si Waziri Mkuu mstaafu. Ni Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa Richmond. Mawaziri wakuu wastaafu walio hai ni kina Cleopa David Msuya, Salim Ahmed Salim, John Malecela, Joseph Warioba na Frederick Sumaye. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuwa "mstaafu" na yule "aliyejiuzulu" tena kwa kashfa ya ufisadi. Hivyo bora mumuite waziri mkuu wa zamani na si waziri mkuu mstaafu, kwani Lowassa hakuwahi kustaafu bali kalazimika kuachia madaraka.Kama walivyosema wenzangu, Watanzania tupo karibu milioni 50, hivi tumefilisika kiasi hiki mpaka tuendelee kung'ang'ania wanasiasa wenye kashfa za ufisadi na utajiri usioelezeka na wenye mashaka kama Lowassa? Jibu ni kuwa la hasha, kuna Watanzania na wanaCCM wengi sana waadilifu na wenye uwezo. Ila Lowassa anajulikana kuwa na uchu wa madaraka na kuwapanga watu humu JF na kwingineko kwa kuwapa pesa ili wampambe na wajaribu ku-brainwash Watanzania wasahau tuhuma za ufisadi na za ukosefu wa uadilifu dhidi ya Lowassa.Ni upumbavu mkubwa kujaribu kumtakasa fisadi. Mungu hapendi hilo na kamwe halitafanikiwa.
 
Baada ya kujiuzulu, serikali ya JK ikazi abandon zile shule za EL ili kumkomoa!. Jana alipozungumzia umuhimu wa kuwaelimisha kwanza watu wetu, amenigusa sana!. Tungekuwa tumeelimika, tusingeibiwa hivi madini yetu, sasa tumegundua gesi,serikali inakimbilia kugawa vitalu kwa umiliki wa miaka 99 huku Watanzania hatuna hili wala lile kuhusu gesi, kwa kifupi, hutujui lolote na tutaishia kuibiwa tena!. EL ameshauri, lets invest kwenye elimu kwanza ili kuwa empower watu wetu ndipo tuingie kwenye ambitious projects kama za kilimo kwanza gesi etc!.

!
sasa mkuu Pasco, huyo Lowassa anashauri tu invest kwenye elimu kwanza wakati mali zetu zinaendelea kuibiwa, sasa mpaka tukija kuanza ku invest kwenye elimu na mali zetu zinaendelea kuibiwa hao wasomi watakuja kuitumia vipi elimu yao katika ustawi wa taifa letu, ishu kubwa hapa ni CCM ni adui wa maendeleo ya watanzania tumuondoe....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom