Kuelekea 2015: Changamoto Kuu za CHADEMA ni nini?

MMM sidhani kama kujadili changamoto za CDM kwa uwazi ni tatizo bali tatizo linakuja pale mtu anapotaka mikakati ya CDM ya kutawala kama wakikamata dola mwaka 2015 waanze kuiweka wazi ili kuifaidisha CCM.

mikakati ya kutawala siyo siri vile vile kwani wanaowatala ni Watanzania na wanahitaji kujua watatawaliwaje. Ni katika kujua ndio wanaweza kuweka uamuzi sahihi wa nani aje kuwatawala. Hadi hivi sasa kitu kinachoweza kuwa siri ni mikakati mbalimbali ya kushinda au kuendesha chama lakini siyo ya kutawala wananchi.
 
Kuna vingine siyo vya ccm,sema ,vingi ni vya wananachi.

Wananchi ndiyo wanaotakiwa wa revolt,wakisomeshwa(kama m4c inavyofanya),basi watatambuwa haki zao na watafight for justice.Lakini nadhani wewe hukubaliani na m4c wala maandamano.

Conclusion yako wewe ni nini?

Jiulize maandamano na M4C hadi hivi sasa vimebadili nini katika mifumo, sheria na utendaji wa serikali? Sheria ya uchaguzi imebadilika? Tume ya uchaguzi imebadilika, kanuni za uchaguzi zimebadilika? kuandikisha wapiga kura kumebadilishwa? Maandamano ni mazuri sana na yanastahili kuungwa mkono lakini maandamano yasiyokuwa na matokeo ni ya nini? Isije kuwa watu wanapenda kuona picha za umati wa watu tu halafu zinawafanya wajisikie vizuri kuwa wanakubalika zaidi na kupendwa zaidi and then thats it.
 
Kuhusu kwamba hakuna kilichobadilika,kuna ukweli kwenye hilo kwa upande mmoja na upande mwingine hakuna ukweli.

Kwa mfano ni kweli kwamba tume na kanuni za uchaguzi pamoja na mengineyo,havijabadilika.

Lakini kwa upande mwingine,mawazo ya wananchi yamebadilika na ndiyo maana unaona wengi wanajiunga na chama hicho.Pia kuna mabadiliko ya mwamko wa wananchi na ndiyo maana hata ccm wanataharuki na kuamuwa kutumia dirty tricks ikiwemo dola na kudhibiti shughuli hizo za chadema.Kama kusingekuwa na mabadiliko,basi ccm wangewaachia tu chadema waendelee na shughuli zao bila kujali.

Hivyo kukubalika huko machoni pa wananchi,chadema inatakiwa wacapitalize,kuhakikisha wanajiandikisha kupiga kura pamoja na kuendeleza shughuli za chama.
 
Mmk, cdm ili ishinde uchaguzi;

1. Inabidi ihakikishe inafika kila kona ya nchi na kueneza sera zake.

2. Inabidi ifanye kazi ya Tume ya uchaguzi kuhamasisha na kuhakikisha watu wanajiandikisha kwani wengi hawana vitambulisho (vimepotea) na wengine walishakata tamaa ya kupiga kura kwa dhana ya kwamba upige usipige ccm itashinda kwa vyovyote.

3. Cdm inabidi ifanye kazi ya jeshi la polisi katika kulinda kura. Hapa panachangamoto hasa katika uchaguzi mkuu. Hasa vijijini ambako hamna umeme. Ila kuna vijana wengi sana hasa wa chuo wapo tayari kufanya kazi hiyo...pengine we can try on that.

4. Umoja ndani ya chama. Ikumbukwe ktk uchaguzi uliopita Zitto hakumnadi Dr Slaa Kigoma na sehemu zote alizoenda. Hii ilisababisha Cdm kupoteza kura nyingi za ubunge na rais hasa kigoma na maeneo jirani.

5. Elimu ya uraia juu ya propaganda chafu hasa za chama cha mapinduzi.

Ni hayo tuu kwa sasa.
 
Mushi kama mawazo ya watu na mwamko wao umebadilika sababu ya maandamani lakin mifumo, sheria na miundo mbinu ya demokrasia imebakia vilevile hilo linasaidia vipi kupa CDM ushindi kwenye uchaguzi?
 
Kuhusu kwamba hakuna kilichobadilika,kuna ukweli kwenye hilo kwa upande mmoja na upande mwingine hakuna ukweli.

Kwa mfano ni kweli kwamba tume na kanuni za uchaguzi pamoja na mengineyo,havijabadilika.

Lakini kwa upande mwingine,mawazo ya wananchi yamebadilika na ndiyo maana unaona wengi wanajiunga na chama hicho.Pia kuna mabadiliko ya mwamko wa wananchi na ndiyo maana hata ccm wanataharuki na kuamuwa kutumia dirty tricks ikiwemo dola na kudhibiti shughuli hizo za chadema.Kama kusingekuwa na mabadiliko,basi ccm wangewaachia tu chadema waendelee na shughuli zao bila kujali.

Hivyo kukubalika huko machoni pa wananchi,chadema inatakiwa wacapitalize,kuhakikisha wanajiandikisha kupiga kura pamoja na kuendeleza shughuli za chama.

Well noted, good. Excellent.
 
Mimi naamini CDM bado tunakabiliwa na changamoto lukuki ndani ya kipindi hiki kifupi kabla ya uchaguzi wa 2015,

Kwanza kwa aina ya muundo na na falsafa ya uundwaji wa Katiba Mpya mimi sikubaliani nayo, siamini na kamwe hatutapata katiba ya KIRAI,

Pili, Kutokana na Katiba iliyopo na ijayo kama ninavyofikiri, Tume ya uchaguzi ni kikwazo kingine kwa Chadema kushika hatamu.

Tatu, sera za ndani za Chadema ziangaliwe kwa jicho la tatu.

Nne, Usalama wa Chama uimarishwe hasa kitengo cha intelijesia, hii itasaidia kubaini majasusi wa nje ya chama, vivyo hivyo itasaidia chadema nacho kutuma majasusi waliofundwa ipasavyo kwenda vyama vingine hasa ccm kuviangusha.

Tano, Chadema ianzae sasa kuwajenga baadhi ya viongozi wake wawetayari kushika nafasi za uongozi mathalani uwaziri nk.
 
mikakati ya kutawala siyo siri vile vile kwani wanaowatala ni Watanzania na wanahitaji kujua watatawaliwaje. Ni katika kujua ndio wanaweza kuweka uamuzi sahihi wa nani aje kuwatawala. Hadi hivi sasa kitu kinachoweza kuwa siri ni mikakati mbalimbali ya kushinda au kuendesha chama lakini siyo ya kutawala wananchi.

What if mikakati hiyohiyo ya CDM ya kutawala ikachukuliwa na CCM na ikafanyiwa kazi, kuna maana gani ya CDM kuja kutawala?Ni yaleyale ya kutaka kuigeuza CDM think tank ya CCM. Naamini bado kwenye usiri katika hili. Sioni sababu ya kudisclose mikakati hiyo. The only good thing ni kwa CDM kujikita katika kutoa elimu kwa umma juu ya kufanya mabadiliko makubwa huku wakieleza vyanzo halisi vya matatizo yanayowakabili kuwa ni utawala uliopo.

Kama mwananchi atashindwa kuunganisha matatizo aliyonayo na utawala uliopo baada ya kuwa ameelimishwa vya kutosha then atakuwa si riziki kwa CDM.
 
Unafikiri ni hekima kukubali kuja kutawaliwa na watu ambao hujui wanataka kufanya nini na madaraka watakayoyapata wka sababu ni siri yao? Kwamba, watu wachaguliwe kwa sababu wana ajenda ya siri inayojulikana na wao tu na ambayo wananchi hawajapata nafasi ya kuihoji?
 
Mzee Mwanakijiji mind you CDM haianzi from the grass root kama ilivyokuwa kwa TAA na baadaye TANU.Ndiyo maana hata mimi sikubaliani na hoja ya kuifananisha CDM na TANU. Ni vitu viwili tofauti ingawa vyote vinaweza kuwa na lengo lilelile la kumkomboa mwananchi lakini ni kutoka kwenye makucha ya watu/watawala tofauti sana.

Lazima ieleweke kwamba Watanzania si wajinga kiasi tunachowachukulia sasa,wanajua kila kitu kinachoendelea. Pamoja na elimu mbovu ambayo imekuwa ikisambazwa kupitia elimu za kata, imeweza kuamsha hamasa ya mabadiliko.Kwa maneno mengine elimu hizihizi za kata ni kama kaburi la CCM. Vijana wengi sana huko vijijini pamoja na kutokuwa na mfumo wa kisiasa unaowaunganisha moja kwa moja kutokana na vyama vya siasa kutowafikia directly wamekuwa wakihoji mambo mengi na hata kulazimisha mabadiliko ya kimfumo pale inapobidi.

Wakati Edward Lowassa akiwa Waziri Mkuu aliwahi kuulizwa swali gumu huko Ukerewe kuhusu mfumo mpya wa kurundika vyeo vingi kwa mtu mmoja na kukosesha ajira vijana, akawa mbogo, maafisa usalama wakamsumbua sana huyo kijana. Huyo kijana hakuandaliwa na mtu kuuliza swali hilo, kwa elimu na uwezo wake huko kijijini aliona si sawa, akahoji. Spirit hiyo sasa imesambaa na kuwa movement.Huwezi kuwadrive vijana kijinga, wanajua nini wanataka.

One thing is, wananchi wanajua nafasi ya siasa safi na uongozi bora katika kuwaletea maendeleo, wanajua tatizo la ufisadi na kadhia yake katika kusukuma maendeleo yao. Wanaelewa kuwa huwezi kutofautisha uongozi mbovu na ufukara unaowatesa kwa miongo kadhaa sasa.Nadhani ukiwa mbali pengine hili haliwi feasible, lakini lipo sasa.

Demonizing the enemy is a very good strategy to go with, CDM lazima wajikite katika kukosoa kwa nguvu zote sera mbovu za CCM lakini pia kuwinda maovu na udhaifu unaokuwa unajitokeza katika maamuzi na utekelezaji. Haya pekee yanaweza kuonesha utayari wa kutawala.Kujua udhaifu wa anayetawala maana yake uko tayari kuondoa udhaifu huo na kuleta tofauti kubwa. Muhimu hili ni lazima liende sambamba na maandalizi kabambe katika kuongoza dola.
 
CCM wamechaguana walewale mwaka huu. Sitarajii CHADEMA nao wafanye hivo mwakani. Kilichoongezeka kule CCM ni matumizi makubwa zaidi ya fedha kupata vyeo na kutengeneza vi-political dynasties vya hapa na pale. CHADEMA watayaepukaje haya?
 
Ni vizuri CDM ikaandaa mfumo mzuri wa utendaji serikalini.Matumizi ya kiutawala yaangaliwe upya kwa kuzingatia rasilimali zilizopo na vipaumbele vya Taifa.Nina imani kabisa wakijipambanua kwenye eneo hili la gharama za uendeshaji wa Serikali na kuonyesha dira yao ya Uongozi itakayoongeza Tija ya utendaji Serikalini,basi wapiga kura wengi watawaunga mkono.
 
Hili nalo ni neno.
 
Wakifanya yote haya na kutangaza hadharani then CCM wakayafanyia kazi CDM itakuwa na haja gani tena ya kutafuta kuongoza dola? Maana wanachotaka kuwafanyia wananchi tayari kinafanywa. Nadhani kuna tofauti kubwa ya ilani, sera, mipango mikakati, sheria nk. nk. Haya unayozungumza yanapaswa kubebwa na ilani wakati wa kampeni.
 
Kwa matokeo ya chaguzi ndogo zilizofanyika jana inadhihirisha wazi kabisa CDM tuna safari ndefu na ngumu kuelekea uchaguz wa 2015 kama kweli tumedhamiria kuchukua dola.

Kumekuwepo na hoja nyingi dhaifu juu ya kwa nini CDM wameshindwa angalao kupata nusu ya viti vya udiwani ambavyo vilikua wazi.Wanajaribu kutoa lawama kwa tume ya uchaguzi juu ya uandikishaji wa wapiga kura wapya hii ni dhaifu sana kwa sababu kama sababu ni hii huko tuliposhinda walijiandikisha?

Wakat mwingine ni bora kukiri udhaifu wa uongoz wa CDM juu ya mahusiano yao na viongozi wa mikoani mpaka mashinani.Imedhihirika wazi viongozi wa makao makuu wana mkanganyiko wa kiutendaji na uongozi wa chini hamna mrejesho kuhusiana na shughul za CDM kila siku je wanawajibika kwa wanachama je wanafanya kazi za chama ama wanawasubiri viongoz wa kitaifa ndio waende nao kwa wanachama.

Mabaraza ya chama yamelala usingizi au ni kama hayapo mfano. BAWACHA hata haijulikan na kwanini wameshindwa kuwashawishi wanawake kujiunga na CDM au tatizo ni uongozi kung'ang'ania mfumo dume.

Ukiangalia wengi walioichagu CCM jana ni wanawake ambao ndio wapiga kura wengi na wana mwitikio na hamasa ya kipekee ya kisiasa.

Ni aibu kwa matokeo ya jana tuache unafiki CCM IMECHOKWA LAKINI CDM IMELALA.
 
CCM inajifariji bila kuwa na ushindani wa ukweli ni hatari maana anguko la mtu mzima huwa ni kubwa na la kishindo.
 
Kuna ukweli wa uyasemayo, lakini huwezi kupuuzia hizo sababu nyingine ni za muhimu sana, new voters huwa wanaleta mabadiliko kwenye trend za kisiasa!
 
Nooo haijalala kihivyo mkuu wangu!unarahisisha mno!!kama unategemea chama pinzani kukamata dola kirahisi hivyo utakuwa unakosea sana,japo hairidhishi sana lakini tukubali tu kuwa chadema inakimbia!japo spidi yake bado ni ndogo kuliko tulivyotegemea au kutaka ila lazima mbio tuziite mbio!!haina maana timu iliyoshinda kwa goli moja tuiite kuwa imelala,kwa kuwa tu tulitaka ishinde kwa goli nyingi zaidi,kingine ni kuelewa nafasi ya kila mwanachama,mpenzi,na kila mpenda mabadiliko kuchukua hatua stahili pale alipo au anapoweza kufikia,haina maana kuwa mwanachama huku unasubiria kiongozi wa chama kilekile aje kukubembeleza kukipigia kura chako!!badala ya wewe kuwaelimisha/kuwashawishi/na hata kuwaomba wale wa mrengo tofauti na wako wakuunge mkono kukiunga chama chako mkono!! Ila pia kweli kuna sehemu ambazo nguvu inahitajika zaidi,bahati mbaya sana si sehemu moja au mbili,bali sehemu nyingi tofauti,ambazo bado itakuwa ngumu kwa Dr slaa,Mbowe,Tlissu na wengine wachache wenye ushawishi mkubwa kupafikia na kuweza kutoa special assistance huko,kwa muda upi?kwa uwezo upi?kwa uchumi upi?hapo ndipo panapohitaji subira na umakini wa hali ya juu!!kuna sehemu ambazo chama kinaweza kushinda uchaguzi bila hata ya kutumia nguvu nyingi,ila inahitajika subira na umakini mkubwa kuzijenga sehemu kama hizo ambazo mwisho huitwa ngome ya chama fulani,kama lema aliweza kuwashawishi watu elfu,wewe hushindwi kuwapata watu kumi,anza sasa!!ingia kwenye mbio ili uweze kukosoa kile unachojua ugumu wake,badala ya kujaribu kuufyeka msitu huku ukiwa nyuma ya keyboard,ukinyanyua kichwa ndiyo unagundua kumbe ulikuwa unacheza game,kisha unadai umedhulumiwa heka kumi za msitu ulioufyeka kwenye computer yako,shtuka.
 
Soma tathmini ya Dr kitila,nadhani ndipo uwekee base yako ya kulaumu,ingawaje na kuunga mkono kwamba safari bado ni ngumu lakini inayowezekana kama Tukijipanga
 
Back
Top Bottom