Kuelekea 2015: Changamoto Kuu za CHADEMA ni nini?

Kwasababu ndiyo maana niliamini kuwa kupigania katiba mpya ndilo jambo la kwanza na la msingi kabisa.Inavyoonekana,ni kama vile tuko chini ya utawala wa chama kimoja.

Unaamini mchakato ulioanzishwa na CCM, kusimamiwa na wana CCM, ukihakikisha kuwa wajumbe wengi wa baraza la kutunga Katiba ni wana CCM litakuja na kitu kizuri ambacho kitatoa nafasi sawa kwa upinzani kushinda uchaguzi mkuu?
 
...kuondoa mitazamo hasi inajengwa na chama tawala-CCM kwa watu(wengi waishio vijijini ambao ndiyo wanaojitokeza kupiga kura kwa kiasi kikubwa) kwamba CDM ni chama cha ukanda, chenye udini, chama chenye kuleta vurugu, na kikichukua nchi vita itabuka mambo ambayo si ya ukweli: haya yakizibiwa kisawasawa na watu wakajitambua waliko sasa baada ya miaka 50 ya uhuru mwaka 2015 CDM itachukua Nchi.
 
if you have scarcity you can't behave as if you have plenty. The world in fact has scarcity. It is this which is the fundamental prerequisite in understanding of economic theory. Katika siasa ni tofauti zaidi. Kama waliopewa nafasi kusimamia the scarce resources that we have wanaplunder au squander kuwasaidia hawa ili wapate muda zaidi wa kuharibu ni kujiharibu wenyewe. NI jukumu letu kuhakikisha kuwa tunawasaidia kuondoka ili waje wengine.

CCM ilivyo sasa haisaidiki. Isipokuwa kama kunatokea a revolt ndani ya CCM. Siyo uasi huu wa sasa ambao unahusiana na nafasi na maslahi bali uasi unaotokana na tofauti za mtazamo, fikra na maono. Kwa sasa CCM haina tofauti hizo za maono wala fikra; ina tofauti ya nani apate nini na kwanini.

CDM haipaswi hata kidogo kuisaidia CCM kuponya mgongano wake wa maslahi ili wakae vizuri wale zaidi.

Mzee Mwanakijiji, Heshima Mbele! Najua ni Imani na ni vigumu sana kukubadilisha... kwa sababu wako watu wengi pia wanaamini kama wewe hata kule maofisini serikalini wazee hawapendi kuwasaidia vijana kujua kazi kisa wakijua wanaamini wataonekana hawajui kazi... eventually they failed... Lakini wale walioamini wanaweza kuwa-support vijana wadogo wameendelea kupata promotion, kwa sababu wale wazee wanaongoza zile idara wameonekana wanafanya kazi vizuri and eventually they had been promoted kila siku.

So endelea kuamini hivyo kwa sababu kuna kundi kubwa liko kama wewe... the only fact is hilo kundi mara nyingi ni loosers.... "Ukisoma vitabu vya leadership", utayajua haya vizuri na scientific proved facts....

Mimi kwenye hilo kundi hutaniona mzee wangu sana mwanakijiji.

Ubarikiwe.
 
Mara nyingi sana huwa nasoma makala za Jenerali Ulimwengu lakini kinachonigusa zaidi kwenye makala zake ni ile hoja yake kwamba "watanzania tumejipa likizo ya kufikiri". Kimantiki hali hiyo utaiona sana kwenye mabandiko yanayohitaji kufikiri kama hili la Mzee Mwanakijiji kwani mwisho wa siku Yanadoda! Ni rahisi kujaza kurasa kwa kurasa kwa kushabikia au kushutumu chama fulani,kundi au mtu fulani bila kuwa na ushahidi wa kutosha kuliko kujadili kwa kina hoja zenye kuchanganua chanzo cha tatizo. Hata humu tunapenda kujipa raha kwa kuishi kwenye dunia ya kufikirika!!

Kwa mtizamo wangu CHADEMA inakabiliwa sana na vikwazo viwili vikubwa. Katiba ya chama na utendaji wa sekretarieti ya chama pale makao Makuu. Katiba ya CHADEMA ilitungwa juu ya msingi wa imani au Falsafa ya kuondoa mtindo wa kufanya maamuzi toka makao makuu badala yake maamuzi yafanywe kwenye ngazi za chini na Makao kuwe kunafanyika uhakiki tu maamuzi hayo.

Bahati mbaya waandishi wa Katiba ya CHADEMA wakaiandika kwa mtindo wa kurundika maamuzil yote Makao Makuu na kuacha ngazi za chini bila maamuzi. Mfano rahisi ni suala la Madiwani wa Arusha na Mwanza. Kama katiba ingeandikwa kwa mfumo wa kumaliza matatizo ya Majimbo na wilaya kwenye ngazi ya mkoa basi bila shaka Kamati Kuu ya chama isingehusika na migogoro hii ya Mwanza na Arusha.

Lakini Katiba imeandikwa katika mfumo kwamba jambo likishindikana kwenye ngazi ya jimbo ngazi inayofuatia ni Kamati Kuu. Mikoa na Wilaya zenye jimbo zaidi ya moja kazi yao ni kufanya "mashauriano" na katiba inaelekeza kwamba kama maamuzi yakifanywa kwenye ngazi ya Jimbo au wilaya taarifa inapelekwa moja kwa moja Makao Makuu na Mkoa unapewa Nakala!!
Na makao makuu nao wanapeleka maagizo Majimboni na wilayani na Nakala mikoani.

Kwenye ngazi ya mkoa hakuna chombo cha kufanya kazi za kila siku za chama badala yake kuna watu wawili Mwenyekiti na Katibu ambao kwa pamoja na Wenyeviti (waratibu) wa mabaraza ya chama wanaunda kitu kinachoitwa "Baraza la uongozi la Mkoa" na hivyo hivyo kwenye wilaya zenye jimbo zaidi ya moja mfumo ni huo huo. Haya mabaraza ya Uongozi hayana hata mamlaka ya kusimamia kura za maoni kwenye maeneo yao.

Maana yake Uongozi wa Mkoa utapewa tu Nakala ya kujulishwa nani kachaguliwa kwenye kura za maoni kuwa Mgombea ubunge au udiwani bila ya wao kusimamia mchakato huo, lakini kamati kuu ndiyo inayotoa uamuzi wa mwisho nani awe mgombea wa chama. Na viongozi hawa wa MKoa na wilaya zenye jimbo zaidi ya moja kwenye kupiga kura za maoni za kuchagua mgombea ubunge si wapiga kura ingawa kwenye udiwani kuna mwanya wa kuwaingiza wawe wapiga kura.

Wenyeviti wa Wilaya ni wajumbe wa Baraza Kuu la chama lakini Makatibu wa MiKoa si Wajumbe wa Baraza Kuu, Mkutano Mkuu, wala hakuna kikao chochote cha kitaifa kinachowakutanisha Makatibu wa Mikoa. Maana yake Mwenyekiti wa wilaya anakwenda kwenye kikao cha kuagiza Makatibu wa Mikoa wafanye nini halafu unatarajia Katibu wa Mkoa akishapewa maagizo hayo naye amwagize Mwenyekiti wa wilaya ayasimamie!?

Sekretarieti ya chama imejaa watu wengi sana ambao lengo lao kubwa ni kugombea uongozi hasa ubunge kwenye majimbo watokayo. Athari zake kwa chama ni mgawanyo usio sawa wa rasirimali za chama. Watendaji hao wa chama hupeleka vifaa vingi kwenye majimbo watakako wakati sehemu nyingine hakuna vifaa au vilivyopo havitoshelezi.

Kutokana na watendaji hao kuwa wagombea kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 kulikuwa hakuna mtu anayeweza kujibu na kutoa maamuzi kuhusu matatizo mbalimbali yaliyojitokeza kwenye sehemu tofauti tofauti za nchi kwani karibu wote walikuwa kwenye majimbo wanayogombea au kwenye timu ya Kampeni ya Mgombea Urais na Makamu wake.

Huu ni sehemu tu ya mtizamo wangu kuhusu vikwazo vinavyoikabili CHADEMA kuelekea mwaka 2015!!
 
Last edited by a moderator:
Changamoto niionayo kama mkereketwa wa cdm ni bado kutokupenyeza mpaka vijijini na kuweka base nzuri huko.M4C wanajitahidi na wamefanya makubwa lakin zinahitajika jitihada zaid.kwa mfano nko kijijin kwa sasa huku niliko watu wamepata hamasa ya mabadiliko na kuikubal cdm ila kwa sehem kubwa sijaona hata ofc wala tawi lolote la cdm huku so nadhan warekebishe hilo
Sema kamanda wa Chadema, mkereketwa kule pemba, ukilitumia hilo neno shauri yako.
 
Mara nyingi sana huwa nasoma makala za Jenerali Ulimwengu lakini kinachonigusa zaidi kwenye makala zake ni ile hoja yake kwamba "watanzania tumejipa likizo ya kufikiri". Kimantiki hali hiyo utaiona sana kwenye mabandiko yanayohitaji kufikiri kama hili la Mzee Mwanakijiji kwani mwisho wa siku Yanadoda! Ni rahisi kujaza kurasa kwa kurasa kwa kushabikia au kushutumu chama fulani,kundi au mtu fulani bila kuwa na ushahidi wa kutosha kuliko kujadili kwa kina hoja zenye kuchanganua chanzo cha tatizo. Hata humu tunapenda kujipa raha kwa kuishi kwenye dunia ya kufikirika!!

Kwa mtizamo wangu CHADEMA inakabiliwa sana na vikwazo viwili vikubwa. Katiba ya chama na utendaji wa sekretarieti ya chama pale makao Makuu. Katiba ya CHADEMA ilitungwa juu ya msingi wa imani au Falsafa ya kuondoa mtindo wa kufanya maamuzi toka makao makuu badala yake maamuzi yafanywe kwenye ngazi za chini na Makao kuwe kunafanyika uhakiki tu maamuzi hayo.

Bahati mbaya waandishi wa Katiba ya CHADEMA wakaiandika kwa mtindo wa kurundika maamuzil yote Makao Makuu na kuacha ngazi za chini bila maamuzi. Mfano rahisi ni suala la Madiwani wa Arusha na Mwanza. Kama katiba ingeandikwa kwa mfumo wa kumaliza matatizo ya Majimbo na wilaya kwenye ngazi ya mkoa basi bila shaka Kamati Kuu ya chama isingehusika na migogoro hii ya Mwanza na Arusha.

Lakini Katiba imeandikwa katika mfumo kwamba jambo likishindikana kwenye ngazi ya jimbo ngazi inayofuatia ni Kamati Kuu. Mikoa na Wilaya zenye jimbo zaidi ya moja kazi yao ni kufanya "mashauriano" na katiba inaelekeza kwamba kama maamuzi yakifanywa kwenye ngazi ya Jimbo au wilaya taarifa inapelekwa moja kwa moja Makao Makuu na Mkoa unapewa Nakala!!
Na makao makuu nao wanapeleka maagizo Majimboni na wilayani na Nakala mikoani.

Kwenye ngazi ya mkoa hakuna chombo cha kufanya kazi za kila siku za chama badala yake kuna watu wawili Mwenyekiti na Katibu ambao kwa pamoja na Wenyeviti (waratibu) wa mabaraza ya chama wanaunda kitu kinachoitwa "Baraza la uongozi la Mkoa" na hivyo hivyo kwenye wilaya zenye jimbo zaidi ya moja mfumo ni huo huo. Haya mabaraza ya Uongozi hayana hata mamlaka ya kusimamia kura za maoni kwenye maeneo yao.

Maana yake Uongozi wa Mkoa utapewa tu Nakala ya kujulishwa nani kachaguliwa kwenye kura za maoni kuwa Mgombea ubunge au udiwani bila ya wao kusimamia mchakato huo, lakini kamati kuu ndiyo inayotoa uamuzi wa mwisho nani awe mgombea wa chama. Na viongozi hawa wa MKoa na wilaya zenye jimbo zaidi ya moja kwenye kupiga kura za maoni za kuchagua mgombea ubunge si wapiga kura ingawa kwenye udiwani kuna mwanya wa kuwaingiza wawe wapiga kura.

Wenyeviti wa Wilaya ni wajumbe wa Baraza Kuu la chama lakini Makatibu wa MiKoa si Wajumbe wa Baraza Kuu, Mkutano Mkuu, wala hakuna kikao chochote cha kitaifa kinachowakutanisha Makatibu wa Mikoa. Maana yake Mwenyekiti wa wilaya anakwenda kwenye kikao cha kuagiza Makatibu wa Mikoa wafanye nini halafu unatarajia Katibu wa Mkoa akishapewa maagizo hayo naye amwagize Mwenyekiti wa wilaya ayasimamie!?

Sekretarieti ya chama imejaa watu wengi sana ambao lengo lao kubwa ni kugombea uongozi hasa ubunge kwenye majimbo watokayo. Athari zake kwa chama ni mgawanyo usio sawa wa rasirimali za chama. Watendaji hao wa chama hupeleka vifaa vingi kwenye majimbo watakako wakati sehemu nyingine hakuna vifaa au vilivyopo havitoshelezi.

Kutokana na watendaji hao kuwa wagombea kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 kulikuwa hakuna mtu anayeweza kujibu na kutoa maamuzi kuhusu matatizo mbalimbali yaliyojitokeza kwenye sehemu tofauti tofauti za nchi kwani karibu wote walikuwa kwenye majimbo wanayogombea au kwenye timu ya Kampeni ya Mgombea Urais na Makamu wake.

Huu ni sehemu tu ya mtizamo wangu kuhusu vikwazo vinavyoikabili CHADEMA kuelekea mwaka 2015!!
Kwa kifupi tu ni kwamba, katiba ya CDM haijalundika madaraka katika ngazi ya taifa, ila miundo ya CDM katika ngazi za chini bado ni changa, na mara nyingine huwa haipo. Vile vile viongozi wa muda wameonyesha udhaifu katika utendaji katika ngazi za chini, Hii ni kazi inayoshughulikiwa na kitu kinaitwa M4C; yaani kuimarisha organisation structure. Mwanakijiji ananda dep na ana uelewa mzuri, jifunze kutoka kwake.
 
Wewe unafikiri ni kwa nini kamati kuu imeingia kwenye Mgogoro wa madiwani wa Arusha na Mwanza!? Udhaifu wa ngazi za chini unaletwa na nini?
 
1. Taking the power from Party leaders to the People.
Mfumo wa upatikanaji wa wagombea/mgombea urais ndan ya CDM, bado hautoi fursa kwa wanachama wake kwan mgombea bado anapatikana kwa baraka za kamati kuu. Mimi naona hili kama changamoto hasa tunapoelekea 2015.

Utaratibu huu uliozoeleka utazalisha makundi yanayohasimiana hasa baada ya kundi fulani kuona mtu wao hajapitishwa na kamati kuu. Ili kujenga umoja wa chama, kuuza sera za chama, kujua misimamo ya mgombea na kupima namna anavyokubalika, CDM wanapaswa kuiga mfumo unaotoa fursa kwa wanachama wao kuchagua viongozi watakaopeperusha bendera ya CDM 2015. Hili linapaswa kufanyiwa kazi kwenye katiba kwanza ili kuingiza huu mfumo mpya wa 'primary election'
Mfumo huu wa primaries ukisimamiwa vizuri utaongeza mboji katika ule mti wao wa NGUVU YA UMMA, wanaoupalilia kila kukicha
 
Hili linapaswa kufanyiwa kazi kwenye katiba kwanza
Kuna watu humu tukiwaambia kwamba katiba ya CHADEMA ina udhaifu mkubwa hutamani kupasuka. Lakini hata viongozi wa kitaifa wa chama wamekiri na wanajua kwamba kuna mkwamo mkubwa sana unaosababishwa na katiba iliyopo. Tatizo ni Mashabiki ambao wengi wao hata Katiba ya CHADEMA iliyoko mtandaoni hawajawahi isoma!!
 
2. Ushiriki wa viongozi wakuu ktk uchaguzi Mkuu.
Sote tunajua namna viongozi wakuu, kutoka makao makuu walivyokuwa na influence kwenye uchaguzi wa majimbo, lakin 2010 tulishuhudia viongozi wengi kutoka makao makuu wakipigania majimbo yao wao badala ya kwenda kuhamasisha sehem nyingine ili wapate majimbo mengi zaidi (na yangepatikana mengi zaidi kama hili lingetokea).

Kwangu mimi hii bado ni changamoto tukielekea 2015 na linaweza kujirudia tena kama wasipokuwa makini. Hoja hapa si kuwazuia viongozi wa makao makuu wasigombee ubunge, bali kuwalazimisha washiriki ktk chaguzi walau ndani ya kanda wanazotoka. Na hapa nieleze kushangazwa kwangu na kutokuwepo kwa ofisi za kanda/jimbo, kama sera ya CDM inavyohubiri. Nataman CDM ingekuwa na tabia ya kuweka resources zake pale mdomo wake ulipo, mfano ni hii sera ya majimbo (ambayo hata mimi ninaikubali sana). Ni kwa nin hatuon chama kikiendeshwa katika misingi ya sera hiyo? (natambua katiba ya CDM inatambua hili, lakin utekelezaji wake hauonekani). Mimi nadhan viongozi hawa wa majimbo/kanda wangekuwa na mchango mkubwa sana kwenye Uchaguzi Mkuu, katika majimbo yao.
 
kwa cdm kwel inabidi ijipambanue kwa kuishi yale inayotangaza majukwaani.. hapo ndio wataongeza public trust.. maneno matupu hayavunji mfupa.., wamepewa halmashauri moshi, karatu, na mwanza (walioichezea taarab juz wakanyanganywa) wajpime wamefanya nini huko? au wanafanya kama wenzao wa ccm? jingine wajiepushe na vitendo vyote vinavzoondoa trust kwa wananch kama rushwa, kujitofautisha sana na wananch wa kawaida kwa kuendesha magar yakifahar wakat wananch wao wanaish kwenye umaskini uliopindukia mf. singda, kgma etc v2 ambavyo wenzao wanavifanyia kaz! kueleza mipango inayotekelezeka kuhusu kuondoa umaskini., elimu, afya mali asil, uwekezaj , ajira, sera za nje, uhamiaji nk, wafanye utafit wa kutosha cio kupga 2 porojo majukwaani kama ccm.. la muhimu zaid, il kuingoa ccm madarakani unatakiwa uwe mara mbili mbele kwa ubora kuliko ccm.! kimkakat na kiutendaji.
 
Changamoto ni zitto kuutaka urais wakati hana sifa wala vigezo, huku jina lake liko Kwa hosea wa Takukuru, kisa alikula posho mbili yeye pamoja na wabunge wa ccm. CDM wakimpitisha ccm watatoa hadharani ile faili. Hivyo, zitto na kashfa zake kuutaka urais ni changamoto kubwa ya CDM.

Ni ukweli usiopingika kuwa tishio la kutochukua nchi 2015 na tishio la anguko la cdm n ZZK NA KAULI ZAKE ZA URAIS. Kwangu hii n changamoto kuu. handling ya changamoto hii ndo itaamua kama cdm wanaingia ikulu ama la!
 
Kauli za Zitto si changamoto kwa viongozi wanaojua kustratergize, tena inaweza kutumika kama mtaji ndani ya CDM. Cha msingi ni kuja na mfumo mpya utakaowapa wanaCDM nguvu ya kuchagua mgombea wao. Na hii ndio inaitwa 'primary election'
 
Changamoto ni zitto kuutaka urais wakati hana sifa wala vigezo, huku jina lake liko Kwa hosea wa Takukuru, kisa alikula posho mbili yeye pamoja na wabunge wa ccm. CDM wakimpitisha ccm watatoa hadharani ile faili. Hivyo, zitto na kashfa zake kuutaka urais ni changamoto kubwa ya CDM.
Hii kashfa inahitaji ushahidi kamili tuu vinginevyo Hakuna chochote hapa.

Labda cha kufanya kwa CDM kuanza kutoa elimu ya kupokezana madaraka toka chama kimoja kwenda kingine nijuavyo vijijini walilishwa sumu ya upizani ni vitA wakati si kweli hilo tu litaleta utata Wa kukubali kusimamia ushindi Wa chama chetu Chadema

Sent by chescomatunda using JamiiForums
 
Unaamini mchakato ulioanzishwa na CCM, kusimamiwa na wana CCM, ukihakikisha kuwa wajumbe wengi wa baraza la kutunga Katiba ni wana CCM litakuja na kitu kizuri ambacho kitatoa nafasi sawa kwa upinzani kushinda uchaguzi mkuu?
Mkuu,tayari kila kitu kinasimamiwa na ccm,kuanzia uchaguzi na hata "mlezi" wa vyama yule Tendwa,upinzani kwake ni kama watoto wa kambo.So tukianza kuangalia hayo,hakuna kitu ccm isichokisimamia,wao ndiyo wenye dola mkuu.Kama kote huko chadema wanashiriki na kutegemea kupata matokeo flani,why not kwenye katiba mpya?

Kama kuna njia zinazoweza kutumika ili katiba isisimamiwe na ccm peke yao(mchakato),yani tupate katiba inayotokana na wananchi,then kwanini wasi fight for it?
 
wao wanasafiri zaidi kwenda uk na usa lakini wanasahau wana kazi kubwa zaidi nyumbani,hao jamaa wa uk na usa hawapigi kura,huku wanamsema kikwete kwa kusafiri sana.sometimes wanakatisha tamaa sana hawa jamaa

Cant you think much bigger? Misaada kama pickup 40 na ndege mbili (chopper) zimepatikana kutokana na ziara za nje. Huwezi kuwa TOPTHINKER alafu usilione hilo.
 
Ili kiweze kuja kushika madaraka ya utawala wa nchi yetu na hatimaye kuliongoza taifa CDM inahitaji kuaminiwa na wananchi wengi zaidi na zaidi ya kuaminiwa inahitaji kukubaliwa kuwa ni chama cha kisiasa ambacho kinaweza kuwa mbadala wa CCM na hivyo kuweza kushika hatamu ya uongozi wa taifa.

Kuanzia kuanzishwa kwake hadi leo hii miaka ishirini imepita na sasa CDM kina uzoefu mkubwa kuliko ule uliokuwepo wakati TANU inashika uongozi wa nchi. Ikumbukwe TANU kama chama cha kisiasa kiliundwa rasmi mwaka 1954 na miaka saba baadaye kilikabidhiwa nchi. Kimsingi TANU ukilinganisha na CDM kilikuwa na changamoto kubwa zaidi kuliko! Kuanzia utawala wa Kikoloni, ukoloni Afrika, ukosefu wa wasomi, miundo mbinu ya mwanzo wa karne ya ishirini n.k. Ni wazi basi kwa kila kipimo CDM leo kama vilivyo vyama vingine vikongwe vya upinzani nchini imefika mahali ambapo inaweza kupimwa ikapimika.

Wakati maelfu ya Watanzania wakizidi kujitokeza kukiunga mkono na kukiamini maelfu pia wapo ambao hawajakiamini na hawajakikubali. Wale wenye kukubali wanakubali kwa sababu nyingi kubwa yawezekana ikiwa ni imani iliyojengwa ya kuwa CDM imesimama kama chama cha upinzani ikifanya kazi yake kwa umashuhuri na hivyo kuonekana kuwa mwiba kwa watawala. Kuna ambao wanaridhika na CDM kama chama cha upinzani; wakikosoa utawala wa CCM, wakikosoa watawala wa CCM na wakitoa ushauri mbalimbali kwa serikali na hawa hufurahia na kuridhika pale ambapo serikali inapochukua mapendekezo ya CDM. Je inatosha kuwa chama cha upinzani chenye kukosoa na kushauri serikali na taasisi zake? Je inatosha kwa viongozi wa upinzani kukosoa wale wa CCM na kuisaidia serikali itawale?

Niliwahi kuandika huko nyuma mada ya kwamba jukumu la chama cha upinzani siyo kusaidia serikali kutawala bali ni kuhakikisha wanaiangusha serikali iliyoko madarakani ili wao wapate nafasi ya kuingia kwenye uongozi huo na kutekeleza sera zao. Mada hiyo ya Aprili 2011 inaeleza kwa kina kuwa siyo jukumu la CDM kuikosoa serikali ili itawale vizuri. Lengo lolote la kukosoa serikali ni kuidhoofisha ili hatimaye ianguke (collapse) au wananchi waikatae kwenye uchaguzi mkuu.

Wakati naendelea kufikiria maoni yangu mwenyewe kuhusu mwelekeo wa CDM kushika dola mwaka 2015 na changamoto zilizopo natoa nafasi kwa mjadala huru kwa wapenzi, mashabiki, wanachama wa CDM na wakosoaji wengine kujaribu kuanisha changamoto ambazo wanaziona zinaikabili CDM kuelekea kushika dola 2015 na hasa kuangalia zile changamoto ambazo zisiposhughulikiwa kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 zinaweza kuifanya CDM isifanye vizuri sana.

Katika kuangalia changamoto hizo nina presume kuwa watu wanakubaliana katika mengi mazuri ambayo yamekwisha fanya hadi hivi sasa na CDM.

Unaamini kuna changamoto kubwa zinaikabili CDM sasa hivi na ambazo zinaweza kuwa kizuizi kwa CDM hatimaye kuweza kushinda uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge, ule wa Serikali za Mitaa na hatimaye kuiondoa CCM madarakani?

Moja ya changamoto kubwa zaidi ni kuacha kuiba wake za watu kama huyu BABU hapa chini
View attachment 69423
 
Ni kweli sana. Watu wanafikiria kujadili changamoto za CDM hadharani ni kuisaidia CCM; kivipi mimi sielewi bali ni woga usio na sababu.

MMM sidhani kama kujadili changamoto za CDM kwa uwazi ni tatizo bali tatizo linakuja pale mtu anapotaka mikakati ya CDM ya kutawala kama wakikamata dola mwaka 2015 waanze kuiweka wazi ili kuifaidisha CCM.
 
Watafight vipi wakati kila kitu ni cha CCM?
Kuna vingine siyo vya ccm,sema ,vingi ni vya wananachi.

Wananchi ndiyo wanaotakiwa wa revolt,wakisomeshwa(kama m4c inavyofanya),basi watatambuwa haki zao na watafight for justice.Lakini nadhani wewe hukubaliani na m4c wala maandamano.

Conclusion yako wewe ni nini?
 
Back
Top Bottom