Elections 2015 Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

huu wimbo wa kidini utakusaidia nini wakati hauuziki? usingetawaliwa na wazungu na waarabu leo kauli yako ungesemaje?

Utaujua hiyo 2015 kama umeuzika au umedoda ... suiri uone, tuombe uhai na uzima mkuu,
 
Mkuu Pasco kwa muktadha huu tuhesabu Lowasa kesha dondokea pua?
Dah na zile 10m anazotoa bora asitishe tu aendelee kula na wajukuu.
 
Chadema sio rahisi kushinda, kwa sababu imeonesha dhahiri kuwa ni chama cha kanisa, sisi waislamu hatuwapi kura zetu , hilo lazima walijue, sasa watashinda kwa kura za kina nani?

Usiseme sisis waislam.kwanza faham waislam wengi tupo CDM na tunamapenz nacho sasa we utanikataza mim nisipigie kura? kwanza we sio muislam dini yenyew inakataza wiz mbona ssm wanatuibia halaf nijiunge na wez? sitothubutu kuwa CCM au mwana CCM emungu nisaidie.
 
Wanabodi,
Preamble: "Kwa opinion yangu, Uchaguzi wa 2015, Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!"!

Trend za Upepo wa Kisiasa kuelekea 2015, zinavuma kwa Kasi ya Ajabu kuelekea Direction ya Mabadiliko (The Wind of Change, is Sweeping Across Tanzania) na kila dalili inaonyesha na kuelekeza Chadema is gaining momentum and there is to stop it kuchukua nchi mwaka 2015 iwapo...

  • Hakuna ubishi kuwa siku zote, CCM imekuwa ikishinda chaguzi mbalimbali "kihalali" na mtaji wao mkubwa wa ushindi ni "watu".
  • Hakuna ubishi kuwa CCM kama chama, kimechoka, dalili zote za chama kichovu kinachosubiri kifo, tayari, zimeisha jitokeza kwa CCM, kinachosubiriwa sasa its only a matter of time ni lini kitaangwa rasmi, hiyo 2015 naiona kama ni mbali sana!.
  • Hakuna ubishi kuwa wengi wa hao "watu", wamekuwa wakuichagua CCM sio kwa sababu wanaipenda sana!, (waipende kwa lipi?), la hasha!, "watu" wamekuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu!.
  • Hakuna ubishi, kuwa wengi wa hao "watu" waliokuwa kuwa wakiichagua CCM kwa mazoea, sasa wameichoka, hivyo 2015, hawatachagua tena chama kwa mazoea, bali watachagua chama kwa "sababu"!.
  • Hakuna ubishi kuwa Chadema, ndicho chama kinachokubalika zaidi kwa sasa kuliko CCM, hivyo ule mtaji mkubwa wa CCM iliyoutegemea kwa miaka nenda miaka rudi, sasa umehamia Chadema!.
  • Kama ambavyo CCM imekuwa ikichaguliwa kwa mazoea tuu, na sasa CCM imechokwa, vivyo hivyo kwa sasa Chadema haina lolote la kukifanya kipendwe, bali kinapendwa kwa sababu "watu" wameichoka CCM!.
  • Kama utaguzi utaitishwa leo, Chadema itashinda kwa kishindo kikubwa cha ajabu, lakini ukiwauliza hao watakaokipa Chadema ushindi, ni sababu zipi za kuichagua Chadema, hawatakupa sababu yoyote zaidi ya kuichagua Chadema kwa sababu wameichoka CCM!.
  • ili Chadema iweze kupata ushindi wa Tsunami kwa uchaguzi wa 2015, lazima Chadema ikubali kubadilika, isiendelee kuutegemea huu umaarufu wa muda kwa kushangiliwa na umati wa watu walioichoka CCM, bali Chadema sasa lazima iwape Watanzania sababu za kuichagua Chadema.
  • So far so good, Chadema is doing a good job kwa sababu M4C is doing the right thing!. Doing the right thing alone, doesn't guarantee sweet clear victory for Chadema, it got to do things right!. Hii inamaanisha ili Chadema ishinde kwa kishindo kinachotakiwa, lazima ikubali kubadilika and start doing things right besides doing the right thing!.
  • Hivyo ndugu zangu viongozi wa Chadema najua 2015 mmedhamiria kwa dhati kuchukua nchi kwa ushindi wa kishindo!, lakini ili lengo hili litimie, ni lazima kwanza mkubali kusikiliza, pili mkubali kubadilika kwa kuzikiliza hoja zinazotolewa kuhusu Chadema na kuzifanyia kazi!.

Naomba kumalizia kwa nukuu kutoka kwa mmoja wa wanachama wetu humu jf.



Kwa wale wapenzi wa Chadema, ni vema kuwa great expectations on Chadema kuchukua nchi 2015, only if Chadema itabadilika, vinginevyo keep hopping for the best and get prepared for the worst kama Chadema haitabadilika na 2015 itakuwa ni CCM Tena!.

NB. Msiniulize Chadema wabadilike nini, wahusika wameshaambiwa imebaki kusikiliza na kutekeleza!.

Naomba kuwasilisha.

Pasco.




Uko sahihi kiasi fulani lakini tathmini yako imekosa nyama za kutosha. Katika mfumo mgumu kama wetu, mfumo ulioegemea chama kimoja kwa miongo mingi huja muda kikachokwa. Lakini sikubaliani nawe kuwa wapiga kura watakaokichagua CDM hawatakuwa na sababu ya kukichagua. Wanakichagua kwa kuwa CCM imeshindwa kukidhi matarajio yao, na hapa kuna chama mbadala kinacholeta matumaini mapya. Je hiyo siyo sababu kubwa? Ndiyo vyama viko vingi na vyema sera nzuri tu, lakini watu wamekichagua CDM kuongoza ukombozi wa nchi hii, si kwa kubahatisha la hasha, isipokuwa kwa kuwa uongozi umeonyesha dira, kule ambapo watanzania wanatamni tuwe.

Unaposema CDM kibadilike unatakiwa usifiche kitu, ama usituache hewani, kama kweli wewe ni mwenzetu sema unachoona kina shida ili kibadilishwe sio kuweka mafumbo mafumbo na kutuacha sisi tukibashiri
 
Napata tatizo moja, TANU na baadae CCM wametawala tangu 1961 kufikia mwaka 1995 alipong'atuka Nyerere. Wakati huo hawakuwepo mafisadi, wala rushwa,sijui wauwaji, mikataba mibovu and so and so....na nchi haikuendelea na tumeendelea kuwa masikini. CDM wanachoongelea ni matatizo hayo hapo juu kama kwamba yakiondolewa na umaskini utakwisha. Kwa vile siamini hilo, naomba nifahamishwe CDM itafanya nini cha ajabu hapo 2015 kama wataingia madarakani? Naona sasa haziongelewi sera bali kuondoa mambo yanayotokana na matukio yanayojitokeza...! Nipeni ushawishi niichague CDM hapo 2015. (ila sasa hivi siandamani ng'o niko kwenye kujitafutia riziki

Watanzania tunahitaji kuelimika na sio vyeti sasa mbona majibu unayo hapo juu kwenye maandishi mekundu tena sababu nzuri kabisa
 
Chadema ikichukua nchi nahama Tanzania naenda "Malawi"

Subiri 2015 kilio cha mamba, wanahangaika ili wapate ku-negoatiate na ccm kabla ya 2015 maana wanajua ndio kifo chao..

Wanataka kupata deal kama la CUF zanzibar mapema ndio maana maandamano usiku na mchana..bureeeeeeeee.
 
Mwaka 2005 walikuwa wachache mwaka 2010 wakaongezeka mwaka 2015 unatarajia nini ?.

Kwani hao walikuwa wapi mwaka 2005 na 2010? mbona Mbowe aligaragazwa vibaya sana, uchaguzi uliofatia akaona huyu Jakaya Mrisho Kikwete si size yake akamuomba Slaa amsaidie, nae akagaragazwa vibaya sana na hao vibaraka wenu si walikuwepo au umesahau?
 
mkuu Pasco

nimekuelewa hivi "" wanachadema pamoja na viongozi wao huu ndo wakati wa kumwaga sera za chama na kuzinadi kwa sana kadiri ya uwezo wao ili wananchi waelewe ni kwa nini muda ukifika wa uchaguzi wataamua kuichagua chadema.""" inadidi hili vuguvugu la mabadiliko liendane na kuitofautisha CCM na CHADEMA kisela na kiutendaji ili baadaye wapiga kura wote wawe wanajua kwa nini wataichagua chadema. BRAVO BRO,PASCO MKANDARA NA WENGINEO WOTE AMBAO MNAENDELEA KUFICHUA MAPUNGUFU ILI YAFANYIWE MAREKEBISHO NA HUU NDO MUDA MUAFAKA.



SISI SOTE NI NDUGU TATIZO NI CCM
 
Nasikitika kuona umetumia muda wako mwingi kuandika hivi. Binafsi nimehudhuria mikutano ya Chadema. Wanaeleza sera zao na watu wanajua kwanini waichague CDM na si CCM. Binafsi najua sijui mwenzangu umeandika tu bila utafiti?
 
Kwani hao walikuwa wapi mwaka 2005 na 2010? mbona Mbowe aligaragazwa vibaya sana, uchaguzi uliofatia akaona huyu Jakaya Mrisho Kikwete si size yake akamuomba Slaa amsaidie, nae akagaragazwa vibaya sana na hao vibaraka wenu si walikuwepo au umesahau?


zomba, ule sio ushindi ambao jk anaweza kujivunia 60% ya kuchakachua then linganisha na idadi ya waliojiandikisha na waliopiga kura alafu angalia na population ya watanzania wote. BE ANALYTICAL!!!!!
 
Usiseme sisis waislam.kwanza faham waislam wengi tupo CDM na tunamapenz nacho sasa we utanikataza mim nisipigie kura? kwanza we sio muislam dini yenyew inakataza wiz mbona ssm wanatuibia halaf nijiunge na wez? sitothubutu kuwa CCM au mwana CCM emungu nisaidie.

Ha ha ha unanifanya nicheke, nadhani unajifurahisha sana!
 
Tujirekebishe kwa nini? Hizi ni thread za kijuha na kizuzu kweli.

Nimegundua humu jamvini chadema mipewa ushauri mnakuja juu, hata kama una manufaa na chama chenu kwanini? nashindwa kuelewa! ni mtu gani asotaka kushauri? hii ni ishara ya chama kibaya, mnataka kujifanya nyie kama nyerere alokataa ushauri na kujifanya kutawala kwa akili zake yeye tu ! hivi mtafika kweli?
 
Kwani hao walikuwa wapi mwaka 2005 na 2010? mbona Mbowe aligaragazwa vibaya sana, uchaguzi uliofatia akaona huyu Jakaya Mrisho Kikwete si size yake akamuomba Slaa amsaidie, nae akagaragazwa vibaya sana na hao vibaraka wenu si walikuwepo au umesahau?

nani asie fahamu kama slaa alishinda uchaguz wa mwaka2010,ila magamba mliiba kura. kiti ni chakupokezana unataka twende kama CUF ambapo kila uchaguz lipumba na wameshamjua kama anatafuta RUZUku& kumgawia mme wake kura.
 
nani asie fahamu kama slaa alishinda uchaguz wa mwaka2010,ila magamba mliiba kura. kiti ni chakupokezana unataka twende kama CUF ambapo kila uchaguz lipumba na wameshamjua kama anatafuta RUZUku& kumgawia mme wake kura.

Aaaaah! wewe umepata wapi hiyo? slaa ashinde? na ndio maana amehalalisha ndoa kujua atagombea 2015 na kwamba mnajidanganya mtashinda? ha ha ha ha mnachekesha kweli !
 
Back
Top Bottom