Kudoda kwa mazao na njaa tarajiwa miaka ijayo

vmjwahuzi

Senior Member
Aug 25, 2014
163
49
Serikali yetu imetangaza uwepo wa ziada wa uzalishaji mazao ya kilimo na hasa mahindi lakini tumesikia wananchi wakilalamikia kukosa soko la mazao yao.Hata wale wenye kupata soko bei imeshuka kwa kiwango cha kutisha.

TaasisI yetu ya reserve ya chakula imeshindwa kununua mzigo wote wa ziada toka kwa wananchi.

TASFIRI pana ya hali hii ni kuwa wakulima wamehamasika kulima na kweli wamelima na kupata ziada ya kutosha.Lakini kumbe wakati serikali ikihamasisha kulima ikasahau masoko yake.

Matokeo yake wakulima watadodewa mazao yao na kuendelea kuwa maskini.KUMBE jitihada za kuhamasika ili tuondoe umaskini hazijazaa matunda.

Swali hapa ni: JE WAKULIMA HAWA MIAKA IJAYO WATALIMA KWA KASI ILE ILE KAMA YA MWAKA ULIOPITA? NA KAMA HAWATAZALISHA KWA KIWANGO HICHO.

JE, TANZANIA SI ITAOMBA CHAKULA CHA MSAADA MIAKA IJAYO?

TAFAKARI
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom