Kudeka/ Kudekezwa

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,227
113,583
Habari zenu mabibi na mabwana,

Kwa kuokoa muda na bila kupoteza wakati, niende moja kwa moja kwenye swali. Eti kudeka ama kudekezwa ndo kukoje jamani?

Mara nyingi nimesikia, iwe kwa inda au nia njema kabisa watu wakisema fulani anadeka sana kwa wazazi wake au fulani kadekezwa sana kwao. Mimi mpaka sasa sijaweza kupata maana yakuridhisha kuhusiana na hilo neno.

Wewe kama wewe unaweza kunipa mfano/mifano ya kudeka na kudekezwa? Natanguliza shukrani zangu kwa wale wote ambao watachangia tajiriba zao na ufahamu wao kuhusiana na hili jambo. Akhsanteni sana
 
KUDEKEZA/KUDEKEZWA ni nadhani ni kuonesha/kuoneshwa kupendwa,kuthaminiwa,kusikilizwa, iwe na wazazi,mume/mke, hata ndugu zako.
Lakin huko kudekezwa huyo anayedekezwa anatakiwa akutumie vizuri na kunatakiwa kuwe kwa kiasi.
Kudekezwa kukizidi sana kunaweza kukufanya mdekezwaji ukabweteka ukawa siyo mshindani au mtu unayeweza,
kujitafutia mwenyewe,kujifanyia maamuzi mwenyewe yenye kukufaa katika maisha yako.
Utapenda kufanyiwa kila jambo au kupewa kila kitu,
Mara nyingi wadekezwaji wanatumia vibaya kudekezwa kwao,
ila mimi binafsi kudeka au kudekezwa sioni kama kuna ubaya kama kutatumia/kutumiwa vizuri na kwa kiasi tu.
ukizingatia kuwa kila jambo likizidi lina athari zake.
 
Kudekezwa ni kusikilizwa zaidi, kupewa kila unachoomba hata kama sio cha msingi. Kutoambiwa lolote pindi unapokosea na huendana ukaribu sana baina ya mdekezaji na mdekezwaji.
 
Je, mtu ambaye amekuwa akijitegemea mwenyewe tokea umri wa miaka 18. Anaishi mwenyewe tena mbali na wazazi wake, anajilipia bills zake mwenyewe. Ambaye kwa kiasi kikubwa (kuanzia mwaka wa pili chuoni na kuendelea) kajisomesha mwenyewe. Kila alicho nacho kajitafutia mwenyewe kwa juhudi, bidii na nidhamu zake mwenyewe. Ambaye wazazi wake wanampenda kwa dhati na bila masharti, na yeye anawapenda vivyo hivyo. Mtu huyo unaweza kusema anadeka/ kadekezwa?
 
cdhan kama tafsiri yako inaukweli ndani yake! Naona kuna haja ya kureview the standard swahili dictionary kwa ufafanuzi zaidi. Otherwise kudeka kuna raha hasa unapopata mtu wa kukudekeza!
 
Mtu anayedeka ama kudekezwa anaweza kujitegemea? Au hawezi na kila apatapo kashida hata kawe kadogo namna gani atakimbilia kwa baba na mama au yeyote yule anayemdekeza?
 
kudeka au kudekezwa kupo kwa aina nyingi inategemea unadeka kwa nani mahali gani na kwa wakati gani! Mfano waweza deka kwa mume/mke lakini kwa wazazi we ndo jembe! Au unadeka kwa wazazi lkn kwa mume au mke we ndo nguzo. Upo mkuu?
 
  • Thanks
Reactions: ggg
kwa tafsiri yangu binafsi
1. kudeka ni tabia ya mtu kujilegeza, kujiona hawezi kufanya/kupambana na vitu vigumu wanavyofanya wengine,
mfano mwanamke mjamzito anapokuwa na mtu wa kuweza kufanya kila kitu kwa ajili yake basi anajiligeza na kudeka
2. kudekezwa. hali ya mtu kufanyiwa kila kitu na watu wengine yeye akiwa anaweza kufanya
mfano mtoto anayefuliwa kufuli zake na kumpikia ile hali ana umri wa miaka 20 hawezi hata kuosha chombo alicholia chakula ni kudekezwa
hata mwanaume anayefuliwa kufuli lake na mkewe pia anadekezwa
 
I like your take on it.
 
Je, mtu ambaye amekuwa akijitegemea mwenyewe tokea umri wa miaka 18. Anaishi mwenyewe tena mbali na wazazi wake, anajilipia bills zake mwenyewe. Ambaye kwa kiasi kikubwa (kuanzia mwaka wa pili chuoni na kuendelea) kajisomesha mwenyewe. Kila alicho nacho kajitafutia mwenyewe kwa juhudi, bidii na nidhamu zake mwenyewe. Ambaye wazazi wake wanampenda kwa dhati na bila masharti, na yeye anawapenda vivyo hivyo. Mtu huyo unaweza kusema anadeka/ kadekezwa?

kudekezwa ni lazima uwe na mtu wa karibu kukudekeza. Anaweza kuwa mzazi au mpenzi. Ukaribu wa hapa sio lazima wa kuonana ana kwa ana. Unaweza kuwa mbali na ukadeka.
Watu wanaojitegemea haimaanishi hawawezi kudeka ingawa mara nyingi watu wanaodeka sana huwa ni wazito kuanzisha maisha yao ya kujitegemea halafu mara nyingi sio wepesi wa kufikiri na kufanya maamuzi.
 
Watu wanaojitegemea haimaanishi hawawezi kudeka ingawa mara nyingi watu wanaodeka sana huwa ni wazito kuanzisha maisha yao ya kujitegemea halafu mara nyingi sio wepesi wa kufikiri na kufanya maamuzi.[/QUOTE]
quite sure! Ndo mana inashauriwa kudeka kucptlize
 
kudekezwa ni lazima uwe na mtu wa karibu kukudekeza. Anaweza kuwa mzazi au mpenzi. Ukaribu wa hapa sio lazima wa kuonana ana kwa ana. Unaweza kuwa mbali na ukadeka.

Unaweza kunipa mfano wa kudeka kwa mtu aliye mbali na mtu au watu wanaomdekeza?

Watu wanaojitegemea haimaanishi hawawezi kudeka ingawa mara nyingi watu wanaodeka sana huwa ni wazito kuanzisha maisha yao ya kujitegemea halafu mara nyingi sio wepesi wa kufikiri na kufanya maamuzi.
Unaweza kunipa mfano au mifano ya mtu anayejitegemea na ambaye anadeka?

Nakushukuru kwa michango yako.
 
hivi kudekezwa/kudeka ina maanisha ''spoiled''?
Anyways,kudekezwa nadhani kuna maana mbili tofauti:
1 Maana nzuri (positive)-kusikilizwa,kupewa raha,kupewa priority etc. some kind gestures and whatever else.kwa ujumla ni kuoneshwa upendo wa hali ya juu kidogo

2 Maana mbaya (negative)-kutokuwajibishwa.mambo ya kujifunza majukumu ya kijamii na kujitegemea ni ya muhimu,kuakosa ni kudekezwa kubaya.mume anaweza kufuliwa kufuli na mkewe (hata mume kumfulia mkewe,raha ya kudeka ni kudekezana banaa:welcome:).kudekezwa kubaya ni sawa na kuharibiwa,manake mwisho unakuwa hujitambui kuwa jamii inategemea nini kutoka kwako katika nafasi tofauti.ndo unakuta jitu haliwezi hata kushukuru au kusalimia!
 
eeeh uko juu kama........
 
Kudekeza mtu ni kumpenda excessively kiasi kwamba ananyimwa nafasi ya kukua kimawazo, kiutendaji, nk. Ni kumfanya mtu tegemezi karibu kwa kila kitu kwa wale wanaomdekeza. Mdekezwa akishatambua hilo, naye anajiachia kabisa na kuogelea huduma za wale wanamdekeza. Kwa kufanya hivo huyu anakuwa anadeka.
 
hivi kudekezwa/kudeka ina maanisha ''spoiled''?

Ndiyo, kudekezwa kwa Kiingereza ndo kuwa spoiled!

Spoil: 3 [+ obj] disapproving a : to give (someone, such as a child) everything that he or she wants : to have a bad effect on (someone) by allowing too many things or by not correcting bad behavior
 
kuna siku tulikuwa na safari ya kikazi tukatumia gari ya work mate wangu.ni mkaka anaejipenda sana,very smart ila mtoto wa mama sana japo hakai na wazazi.yaani buti ya gari imejaa nguo chafu zimetupwa ovyo kabisa!kuna viatu,na underwears chafu!anatembea hadi na pasi(iron box!).sipati picha ya huko nyumbani kwake ni kuchafu kiasi gani!hata kama nguo utasaidiwa kufua shurti zikae kwa utaratibu pia.kama anapika ndio itakuwa balaa.ni mfano tu,japo kwa nje anaonekana smart,ila anadeka

Mtu anayedeka ama kudekezwa anaweza kujitegemea? Au hawezi na kila apatapo kashida hata kawe kadogo namna gani atakimbilia kwa baba na mama au yeyote yule anayemdekeza?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom